Madalali wa bongo mna matatizo gani lakini?

Madalali wa bongo mna matatizo gani lakini?

Screenshot_20240607-224404.png

Huyu Professional..
 
Ukiwa unafikiria utapeli kwa mtazamo huo,mjini utapigwa.. refer kesi za Ndama mtoto wa ng'ombe alivyokua anawapiga Wazungu dhaabu fake,

Wakati nasoma,Mimi na Jamaa yangu tulitengeneza website ya kuuza vitu mtandaoni,Mfano,PS3 ilikua na thamani ya laki 8,sisi tunaweka laki 350,

iPhone 5s laki Tisa,sisi tunaweka laki Tano, reasonable sio?? website ilikua FAKE,

Ukitembelea ununue kitu,inakuja form andika hiki,weka hiki,mwisho wa siku unashindwa ku place order,unaona uzushi,unatoka kwenye website,kipindi ushatumia dakika 20..

Umeongeza watembeleaji wa website,pia Umefungua matangazo,

So kuhusu hao wenye magari nahisi wanafanya hivyo ili kuongeza engagement kwenye Instagram handle zao,ili mtu akitaka kuleta Tangazo la kuuza kweli gari ,rahisi kumshawishi kua Page yangu inatembelewa na watu laki tatu kwa Mwezi, Number hazidanganyi..
 
Wiki hii nimekua nafatilia sana pages za madalali wa magari, Kuna gari ya ofisi nataka kununua kutokana na bajeti nimeamua nianze na used kwanza, sasa hao madalali yaani ni vichekesho tu

"Gari ya muhindi, dukani na nyumbani tu"

"Gari ya mdada"

"Gari ya baba mchugaji hii"

"Gari ya mrembo wa kiarabu"


"Chuma Haina kipengere(ni kama wote walishakubaliana kutotumia neno kipengele kabisa wote wanaandika kipengere)

Ukikuta gari zile za zamani namba A na B wanakuambia "chuma imekaza balaa, ni kuweka wese na kuondoka"

" Lete hela haraka tajiri ameshavurugwa akili"


Kuna magari hata hawaweki hata basic information kama yom,cc,odometer ,yaani ni kutia udamvi udamvi
Nafananisha madalalı wa kibongo sawa na walinzi wa bongo movies. Unakuta nyumba nzuri ina thamani balaa ila mlinzi kichaa au hamnazo.....ndivyo walivyo madalali wa kibongo.
 
Kudeal na madalali wa kibongo kunatakiwa kuwa na moyo aisee. Binafsi sidhani kama wanajitambua akili hawa watu, utakuta mtu unamwambia dalali nataka nyumba ya aina fulani na anakuambia ipo, mnaenda kuona hiyo nyumba unakuta siyo kisha anakuambia "hata hii poa tu" haina tofauti sana na ile uliyoitaka. Nakiri kusema kuwa Madalali wa kibongo hawana akili na hawajuwi kazi yao, ni wababaishaji mno.
Mkuu wana njaa sana hawana ajira kama yako. Waonee huruma tu.
 
Nilichojifunza kwa madalali wetu;
👉🏾 Wachache sana ndo wanajua wanachofanya.
👉🏾 Wengi >70% wamevamia hii kazi, yani kujua tu kufungua akaunti fb, ig, x nk tayari washajikuta ni madalali.
👉🏾 Kutokuwa wakweli - ujanja ujanja na uongo, mteja hapati anachotaka kutoka kwa wengi wao hivyo kusababisha watu usumbufu na upotevu wa muda.
👉🏾 Madalali wengi wa magari hawajui na hawana ABCs za magari. Anapost kazi unampigia unamuuliza kitu cha kawaida2 eg. Engine gani? hajui na hapo keshapost mpk na bei. Hawatoi basic information za gari wamekariri tu AC unaganda na ‘kipengere’ au kama yaliyotajwa kwenye posts huko juu. Ni kwa wachache sana utapata details ambazo zitakupa hali halisi ya gari.
👉🏾 Wengine unakuta minibus zote anasema coaster au hiace (hata kama ni nissan), au LC100 zote ni Amazon, LR110 SW old ni puma nk nk
👉🏾 Facelifted cars hawasemi as if ni sirii (au labda hawajui) japo ni lazima wawe na uelewa wa hilo ili kuepusha changamoto.
👉🏾 Overpricing kama wale wa viwanja.
👉🏾 Most of them have same lifestyle.
👉🏾 Big up kwa wale wachache wanaojitambua, watafika mbali sana.

Ushauri wa jumla:
1. Wajifunze kuwa na uelewa wa bidhaa wanazonadi, waache mambo ya mzaha, uongo uongo, kuigana na kukariri.
2. Wajitambue hii ni kazi kama kazi nyingine na inahitaji professionalism. Udalali sio maneno meengiii irrelevant.
3. Waache tamaa, wajifunze kuridhika na kidogo. No wonder anaweza piga kazi moja tu akapata 50M, hii inawaharibu sana akili.
4. Serikali iwatambue kisheria, wasajiliwe na walipe kodi.
5. Nimeshuhudia watu kadhaa wakipoteza fedha zao kupitia kwa madalali. Kwa kuwa wanajuana sana na polisiii wasi entertain sana utapeli cz haki ya mtu haipotei, laana itawaandama daima unless wabadilike.
 
Wiki hii nimekua nafatilia sana pages za madalali wa magari, Kuna gari ya ofisi nataka kununua kutokana na bajeti nimeamua nianze na used kwanza, sasa hao madalali yaani ni vichekesho tu

"Gari ya muhindi, dukani na nyumbani tu"

"Gari ya mdada"

"Gari ya baba mchugaji hii"

"Gari ya mrembo wa kiarabu"


"Chuma Haina kipengere(ni kama wote walishakubaliana kutotumia neno kipengele kabisa wote wanaandika kipengere)

Ukikuta gari zile za zamani namba A na B wanakuambia "chuma imekaza balaa, ni kuweka wese na kuondoka"

" Lete hela haraka tajiri ameshavurugwa akili"


Kuna magari hata hawaweki hata basic information kama yom,cc,odometer ,yaani ni kutia udamvi udamvi
Unataka gari gani nauza hilux na ist yangu
 
Kiufupi dalali=chawa=utapeli unaendana sana ila kuna unafuu ukiktana na dalali mtu mzima 50+ hawezi kukwambiq m 9 ukainunulie bangi
 
Back
Top Bottom