Nimependa sana Dr. Tulia (Dr wa kisomo) alivyozungumzia hili bila unafiki.
Itafika wakati tutashindwa kutofautisha yupi ni Dr msomi na Dr aliyenunua utambulisho wa Udaktari kwa pesa.
Hivi kweli Babu Tale anapewa heshima ya Udaktari kwa kitu gani alichofanya? Hiyo taasisi iliyompa kwanza ina watu wenye akili sawasawa?
Huu ni upumbavu,huu ni upimbi, hatuwezi kuwa na taifa la mapimbi kwa kuogopa tukisema wataona tunawaonea wivi wao wamepata udokta bila kiteseka.
Hawa dawa yao ni ndogo tu, ni kutokuwatambua kama madokta, yani kila mahali, iwe bungeni au kwenye hafla yoyote hakuna kumuita Dr fulani, unamuita jina lake Bwana Hamis Shaban Taletale. Maana lengo lao la kununua ni ili waitwe madokta.
Kama unataka kutambulika kama Dokta, ingia darasani piga kitabu, kaa chini andaa andiko na ulitetee ndio ukitoka hapo uone raha kujiita Dokta blah blah.
Kwanza hizo PhD za heshima watu huwa hawajiiti madokta,ni ujinga na ushamba tu.