Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Hapana Shaka yoyote wengi wetu humu ndani tunajua harakati za DeepPond na mama j, ni mastory ambayo Yana vituko na burudani na mafunzo ndani yake, binafsi huwa sikosi kumsoma huyu mwamba.
Lakini wote tunakubaliana humu jukwaani kwamba Hakika kama mkewe angekuwa mtu WA kufuatilia Simu ya mumewe bilashaka ndoa yake ingekuwa chali siku nyingi Sana.
Lakini mwanamke huyu amechagua kutojihusisha na mambo hayo na ndio maana pamoja na vurugu zote za mama j bado ndoa Yao iko salama na Maisha yanaendelea kama kawaida.
Kwa mfano kisa cha juzi mwamba baada ya kupigwa sound na mama j ikabidi nae ampige sound wife kuwa mlinzi ofisini kanipigia Simu huenda kuna shida, kama wife angekuwa mfuatiliaji basi angeenda ofisini Kwa mwamba na kumuuliza mlinzi mume wangu alikuja Jana saa nane usiku,kulikuwa kuna shida gani? Bilashaka mlinzi angeshangaa na kustaajabu na hapo wife angejua kuna tatizo sehemu.
Lakini amechagua kumwamini mumewe na ndio maana mpaka Leo wako pamoja na Hana presha zisizo na sababu.
Hata mama yangu pia si mtu WA kuchunguza Simu za Mzee wangu,maana kama angekuwa ana chunguza Bilashaka angelipata la kulipata,coz wakati bado nipo home siku moja mdogo wangu yale mambo ya kumwekea vocha mshua, sijui aliwaza nini na kwenda kwenye text za mshua daah sio poa,itoshe kusema ni Noma,ndo akanitonya bro kuna text flani flani humu.
So point yangu ni kwamba mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake mwenyewe Kwa mikono yake,maadam mumeo anakuheshimu na kukupenda na hajakuletea sababu zozote za kukufanya uwe na mashaka,basi usitafute mashaka katika Simu yake,kwani ukiyataka utayapata Tu!
Kaa mbali na Simu yake Kwa mustakabali wa ndoa Yako.
Ni hayo Tu!