Madaraka ni dhamana ya muda mfupi sana, kutoka kupigiwa magoti hadi kusindikizwa nje ya Ikulu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu anatajwa kuwa miongoni mwa viongozi wa kiafrika waliopenda kuabudiwa , ilifikia hadi Mawaziri kumpigia Magoti .

1898133_20180906_175821.png

Picha ya Chini akisindikizwa kuondoka Ikulu baada ya kukataliwa na wananchi kwenye sanduku la kura

FB_IMG_1629888254786.jpg

Kwenye maisha ya kila siku tunapaswa kuheshimiana na kuthaminiana .
 
Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu anatajwa kuwa miongoni mwa viongozi wa kiafrika waliopenda kuabudiwa , ilifikia hadi Mawaziri kumpigia Magoti .

View attachment 1909417

Picha ya Chini akisindikizwa kuondoka Ikulu baada ya kukataliwa na wananchi kwenye sanduku la kura

View attachment 1909418

Uko sawa kabisa!

Ila "Kwa Tanzania hii bado safari ndefu sana"
 
Hapa kwetu bila Katiba Mpya hilo haliwezi kutokea kamwe, Zambia walishaachana na huu utumwa tulionao sisi muda mrefu uliopita.

Ndio maana maamuzi ya wengi yanaonekana kwenye sanduku la kura na kuleta mabadiliko ya uongozi kwenye taifa lao.

Hapa kwetu hali ni tofauti, kikundi cha maafisa wachache wa Tume ya uchaguzi kinatuamulia mshindi kila wakati wa ucahguzi unapofika.
 
Uchaguzi wao wa kwanza uliomuondoa baba wa taifa lao madarakani, walitumia katiba hiyo hiyo. Nahisi suala la katiba mpya Tanzania tunalipa sana promo, tatizo Tanzania sio katiba, tatizo la Tanzania ni Watanzania wenyewe, sio katiba. Kama uliufatilia vizuri uchaguzi wa Zambia hu wa juzi, jamaa walitaka kuchakachua matokeo kama hapa kwetu, walifunga hadi mitandao ya simu kama ilivyo fanyika hapa kwetu, wananchi hawakukubali na kilichotokea ni historia, ndio huyo bwana Rungu anaondoka Ikulu bila escort. Tusisingizie katiba, sisi ndio sio
 
Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu anatajwa kuwa miongoni mwa viongozi wa kiafrika waliopenda kuabudiwa , ilifikia hadi Mawaziri kumpigia Magoti .

View attachment 1909417

Picha ya Chini akisindikizwa kuondoka Ikulu baada ya kukataliwa na wananchi kwenye sanduku la kura

View attachment 1909418

Kwenye maisha ya kila siku tunapaswa kuheshimiana na kuthaminiana .
lakini siyo hawa kwa kweli wanatia aibu hata hawajui wanataka nini wangekuwa wameshaiondoa ccm muda mrefu sana tatizo tamaa

1629982573437.png

2878995_images_9.jpeg
 
Hapa kwetu bila Katiba Mpya hilo haliwezi kutokea kamwe, Zambia walishaachana na huu utumwa tulionao sisi muda mrefu uliopita.

Ndio maana maamuzi ya wengi yanaonekana kwenye sanduku la kura na kuleta mabadiliko ya uongozi kwenye taifa lao.

Hapa kwetu hali ni tofauti, kikundi cha maafisa wachache wa Tume ya uchaguzi kinatuamulia mshindi kila wakati wa ucahguzi unapofika.
Wananchi wakiamua itawezekana lakiini historia ya upole wa watanzania ndiyo inayofanya mambo yawe yalivyo. Mambo ya kuudhi ni mengi lakini wanashindwa kuonesha kuwa hawajapendezwa nayo, ni kulalamika tu pasipo actions(vitendo) na hasa hao wa maisha ya chini zaidi. Huwaambii kitu kuhusu watawala, na huwasaidia pia kuwaweka madarakani kwani wao hasa ndiyo hupiga kura kuliko daraja la kati..
 
hatuna wapinzani wenye nia ya kuongoza nchi wakichukuwa hawa kwanza wataanza kugombana wenyewe kwawenyewe kugombania nyazifa
 
Hapa kwetu bila Katiba Mpya hilo haliwezi kutokea kamwe, Zambia walishaachana na huu utumwa tulionao sisi muda mrefu uliopita.

Ndio maana maamuzi ya wengi yanaonekana kwenye sanduku la kura na kuleta mabadiliko ya uongozi kwenye taifa lao.

Hapa kwetu hali ni tofauti, kikundi cha maafisa wachache wa Tume ya uchaguzi kinatuamulia mshindi kila wakati wa ucahguzi unapofika.
Pamoja na katiba mpya, fikra za wananchi zibadilike, wawaze kutumia uwezo na haki yao ya msingi kuwawajibisha waliopo kwenye madaraka inapobidi.
Kwa hali ilivyo, katiba iliyopo haifuatwi wala kuheshimiwa, Kuna uhakika gani kuwa mpya nayo haitakuwa hivyo hivyo?
Tatizo ni uwezo wa raia na watumishi wa uma (hasa tume ya uchaguzi, polisi, mahakama) kufikiri na wala siyo katiba.
 
Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu anatajwa kuwa miongoni mwa viongozi wa kiafrika waliopenda kuabudiwa , ilifikia hadi Mawaziri kumpigia Magoti .

View attachment 1909417

Picha ya Chini akisindikizwa kuondoka Ikulu baada ya kukataliwa na wananchi kwenye sanduku la kura

View attachment 1909418

Kwenye maisha ya kila siku tunapaswa kuheshimiana na kuthaminiana .
Lakini nadhani mara nyingi unasahau tofauti kati ya hao na sisi (Tanzania).

Hapa kwetu ni CCM zaidi ya mtu huyo mmoja. Kuna akina Lungu wengi sana ndani ya CCM ambao wanahakikisha kuendelea kuwepo kwao kuna uhakika mradi CCM iendelee kuwepo.

Sasa tuna akina Pinda huko ndani ya CCMwanaohakikisha hilo. linaendelelea. Na kwa bahati mbaya sana, hawa hawaonekani mbele za macho ya wananchi. Wao wanafanya mambo yao kimya kimya huko huko ndani ya chama. Wanaamua nani awe mbele kuwasulubu waTanzania, huku wao wakiwa nyuma ya huyo msulubishaji, ambaye ndiye sisi sote tunadhani tukimwondoa tutapata nafuu, kumbe wapi.

Si umeona mwenyewe alivyoondoka Magufuli, nafuu sasa ipo wapi?
 
Uchaguzi wao wa kwanza uliomuondoa baba wa taifa lao madarakani, walitumia katiba hiyo hiyo. Nahisi suala la katiba mpya Tanzania tunalipa sana promo, tatizo Tanzania sio katiba, tatizo la Tanzania ni Watanzania wenyewe, sio katiba. Kama uliufatilia vizuri uchaguzi wa Zambia hu wa juzi, jamaa walitaka kuchakachua matokeo kama hapa kwetu, walifunga hadi mitandao ya simu kama ilivyo fanyika hapa kwetu, wananchi hawakukubali na kilichotokea ni historia, ndio huyo bwana Rungu anaondoka Ikulu bila escort. Tusisingizie katiba, sisi ndio sio
Kama huo ujasiri wao hatuna, narudia tena, hapa kwetu bila Katiba Mpya hatuwezi kuwaondoa CCM, wanetapakaa kila mahali, mpaka kwenye vyombo vya usalama.
 
Pale nchi ya
NDIO FC CLUB wananchi wana dozi ya unga wa ndere. Hayo hata uigize sinema zetu wata-forward tu ...
 
Naomba nikustushe/kukumbushe.

Uliwahi kumsoma mtu anayejulikana kwa jina la 'Iboya' hapa JF?

Hii ndiyo timu mpya na mambo mapya!

Hebu angalia #9 hapo juu.
hahahaaaa watanyooka tu mwaka huu
 
Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu anatajwa kuwa miongoni mwa viongozi wa kiafrika waliopenda kuabudiwa , ilifikia hadi Mawaziri kumpigia Magoti .

View attachment 1909417

Picha ya Chini akisindikizwa kuondoka Ikulu baada ya kukataliwa na wananchi kwenye sanduku la kura

View attachment 1909418

Kwenye maisha ya kila siku tunapaswa kuheshimiana na kuthaminiana .

Hata hapa yatawakuta watu fulani. Inshallah
 
Kama huo ujasiri wao hatuna, narudia tena, hapa kwetu bila Katiba Mpya hatuwezi kuwaondoa CCM, wanetapakaa kila mahali, mpaka kwenye vyombo vya usalama.
Sasa mkuu 'denoo', kama wametapakaa kila sehemu, na ninakubaliana nawe juu ya hili, hiyo katiba mpya ambayo wao hawaipendi kabisa itapatikana kwa njia zipi bila ya wao kulazimishwa(kwa njia zipi?) ambazo njia hizo hizo pia zingeweza kuwaondoa kwenye madaraka!

Maoni yangu ni kwamba ni vyema, na sahihi kabisa tukiweza kutengeneza katiba mpya bila ya mashinikizo, lakini ukweli ni kwamba CCM hili hawalitaki kabisa. Lakini na kutolitaka kwao hakutazuia kamwe uwepo wa katiba mpya sasa, kwa sababu hawana uwezo tena wa kulizuia hili.

Sana sana, wanachoweza kufanya ni kukubali katiba mpya itengenezwe, na kwa wingi wao wavungevunge huko huko kwenye mchakato wa kuiandaa hiyo katiba ili wapate pa kujishikizia na kuendelea kushikilia madaraka, hata kama watakuwa wamedhoofishwa kuliko ilivyo sasa.

Katiba mpya haizuiliki tena. CCM wasipochukua tahadhari hili litawafyekea mbali.
 
Back
Top Bottom