Ukwelimtupu00
JF-Expert Member
- Sep 9, 2024
- 289
- 416
Abdul pokea simu za madaraka sio kutwa kufanya udalali wa rasimali za ummaMadaraka Nyerere ambaye ni mtoto wa hayati Mwalimu Julius Nyerere amesema anasikitishwa na baadhi ya viongozi wanaokwenda kutembelea mji wa Baba wa Taifa na kutoa kauli mbalimbali za kumsifu mwalimu, lakini wakiondoka hawapokei tena simu zake.
Madaraka amesema si kila simu anayopiga ni simu ya kulia shida, bali kuna wakati anapiga simu kwa ajili ya mipango ya kuendelea kuyasema mazuri ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.