Madaraka Nyerere: Kiongozi anamsifia Nyerere lakini hapokei simu zetu

Madaraka Nyerere: Kiongozi anamsifia Nyerere lakini hapokei simu zetu

Vitu ingine hatuwezi kuelewa.jamaa anaweza kupiga gongo zake huko butiama kilabuni na Akawaambia "naweza kumpigia simu rais saa hii"
Sasa hilo ni jukumu la wapokea SIMU YA Rais.
na wAache kudeka deka Kila siku eti si watoto wa baba wa taifa.
Kafanyeni kazi,.bona makongoro anapiga comedy zake huko maisha yanaendelea.
 
Madaraka Nyerere ambaye ni mtoto wa hayati Mwalimu Julius Nyerere amesema anasikitishwa na baadhi ya viongozi wanaokwenda kutembelea mji wa Baba wa Taifa na kutoa kauli mbalimbali za kumsifu mwalimu, lakini wakiondoka hawapokei tena simu zake.

Madaraka amesema si kila simu anayopiga ni simu ya kulia shida, bali kuna wakati anapiga simu kwa ajili ya mipango ya kuendelea kuyasema mazuri ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Kwani Madaraka hajui kuwa Mwalimu Nyerere anatumiwa tu na hawa wanaokuja kutembelea mji kama kivutio tu wananchi wawaone kuwa wanayaenzi aliyofanya kiongozi huyo?
Kwani Madaraka haoni matendo ya hawa viongozi yanayo waweka mbali kabisa na Mwalimu?
 
Wabongo kwa kukariri! Huu msemo wa ''wazee/waliosoma Cuba wataelewa'' umekaririwa na watu wengi na wengi walioukariri ni vilaza wanaoelewa mambo ndivyi sivyo.
Na ukimuuliza yeye kaelewa nini huwezi kupata jibu.
Hii ni dalili ya upungufu mkubwa katika elimu yetu kiujumla. Watu hawajui kitu lakini wanajifanya wao ni wajuzi wa mambo kiaina yao pekee mbali ya wengine.
 
uzuri watoto wa Nyerere hawajazaliwa na unafki wala uchawa... Wao nyeupe ni nyeupe damu ni damu na sio blaah blaah
Hawana uchawa na ndio kinachowagharimu,

Wakati hawa wa sasa wanataka kusifiwa.
 
Back
Top Bottom