Mkoroshokigoli
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 14,593
- 5,581
Taratibu ndugu usiwaingize waliofariki kwa sababu hawapo nasi na hawawezi kujitetea dhidi ya tuhuma zako.
Kitu kingine ni kwamba, Mimi binafsi sifagilii matumizi, mauzo/manunuzi na wala usafirishaji wa madawa ya kulevya. Lakini hali kadhalika, sielewi hii hali ha furaha sana kwa baadhi yetu kufurahia kusikia mtanzania mwenzetu amepatwa na matatizo kama haya. Nadhani ni vyema kutazama athari zinazosababishwa kwa jamii yetu sisi watanzania kabla ya kufikiria athari zinazosababishwa kwa "mabwana zenu" wa huko Ulaya. Mimi binafsi ningefurahi sana kama Joseph Kaniki au Matumla yoyote angekamatwa akiingiza unga/sembe nchini mwetu, Tanzania. Sababu ya furaha yangu ingekuwa ni kuokolewa/ kuepushwa kwa vijana wetu na madawa ya kulevya. Lakini kama Joseph Kaniki au Matumla amekamatwa akiingiza madawa ya Kulevya nchi za Ulaya kwa wazungu, basi mimi sioni sababu yoyote ya kusherehekea kukamatwa kwao. Kwa sababu hilo ni tatizo la wazungu na wazungu wana nyenzo zote za kukabiliana na matatizo yao.
Najua kuna wajinga humu, narudia kwa herufi kubwa pasipo kuomba msamaha, (KUNA WAJINGA NA WAPUMBAVU HUMU JAMII FORUM) wenye hoja hafifu kwamba; eti wabeba sembe wanalichafua jina la Tanzania. Wabeba sembe wanachafua majina yao binafsi, na siyo jina la Tanzania. Kwa mfano. Mimi binafsi nimeishi ughaibuni kwa miaka mingi na Wa-Nigeria wanajulika kwa miaka mingi sana katika fani ya kusafirisha madawa ya kulevya, kusafirisha malaya "prostitute", kusafirisha mipesa mingi haramu "money laundering" na kadhalika. Na baadhi ya nchi nyingine zinazojulikana kwa tabia hii ni Senegal na Jamaica. Lakini wananchi wa Tanzania au Malawi hawapewi umuhimu wowote ambao wananchi wa Senegal, Nigeria na Jamaica hawapewi. Na kwa wale ambao wanaangalia TV za ughaibuni vipindi kama "UK Border" au "Nothing to declare"; kila siku kwenye vipindi vile huonyesha kukamatwa kwa wabeba sembe "drug mules" na mataifa yao huwa ni Uingereza (wazungu); Wachina, Nigeria na kadhalika. Sijawahi kuona Mtanzania kakamatwa kwenye kipindi kile.
Kwa ufupi, Watanzania ni "wachezaji wapya" katika mchezo huu haramu na hawajulikani kabisa katika fani hii.
Waingereza ni miongoni mwa wabeba sembe wakuu duniani. Najua wengi wenu humu pale kwenye neno "Mzungu" ile herufi "z" huwa hamuioni na akili zenu katika neno Mzungu inasoma neno Mungu. Kwa hiyo haingingii akilini mwenu kwamba wazungu (waungu wenu) ni wabeba sembe.
Kwa mfano hapa chini kuna link mbili ambazo zinaonyesha wabeba sembe wa kizungu, na wahalifu hawa hupewa msaada wote wa kidiplomasia na nchi yao Uingereza kwa sababu Waingereza wanatambua kwamba watu wa aina hii wapo.
1. Peru 'drugs mules' Melissa Reid and Michaella McCollum 'had a good offer' - Home News - UK - The Independent
2. Lindsay Sandiford loses final appeal against drug trafficking death sentence in Bali - Telegraph
Lakini hata siku moja hutosikia watu wakisema kwamba eti watu hawa wanachafua jina la Uingereza.
Kwenye za karne nyingi na biashara hii kama Uturuki, ugiriki na Pakistani; katika sheria zao wana adhabu tofauti kwa muhalifu anayetoa sembe au kuingiza sembe katika nchi zao. Wakikumata unaingiza sembe nchini mwao adhabu yake ni sawa na kubondwa bondwa na nyundo na wakikukamata unatoka na sembe adhabu yake ni sawa na kunaswa kibao tuu.
Kwa ufupi, tuangalie wabeba sembe wanaoliingiza nchini mwetu na tuachanane na wanaolisafirisha juu kwa juu. Kama m-beba sembe alitumia msuli wa walet lake akakupokonya demu; hilo ni kosa la demu wako na usilete nongwa zako hapa. Na kama tukiangalia katika "economic perspective"; kama mbeba sembe wa kibongo akibeba na kuuza sembe lake juu kwa juu (kwa mfano kutoka kwa pele kwenda sweden) kisha akaja kufanya matanuzi Bongo; ni wajinga tuu ndiyo wasioweza kuuona mchango wake katika uchumi wa bongo. Huyu mtu ameliingizia taifa fweza za kigeni, kama amejenga nyumba atakuwa ametoa ajira kwa mafundi adamu, na kadhalika.
Hitimisho. Mimi siyo mbeba unga na ninafanya kazi kama Engineering Consultant Ughaibuni (kwa wale mtakaosema, kwanini unawatetea bana, wewe ni mbeba sembe ninii?) Lakini maisha na wazungu wamenifundisha kuangalia yanayonihusu na kuachana na yasiyonihusu. Sitetei wabeba unga, lakini kama mtu haingizi unga bongo, mimi sioni sababu ya kuwashwa na pilipili. Lakini akikamatwa anaingiza unga bongo basi mimi binafsi nipo radhi kukata shingo yake afe.
Kwa herini.
Injinia,tunamhurumia mtu kwa matatizo ya kujitakia,awe anatoa au anaingiza,biashara hii haifai,na kuhusu kuchafuliwa,ni kadhia ambazo watz wanatoa ushuhuda wa kukumbana nazo kwenye viwanja vya ndege huko ughaibuni,pindi waoneshapo Pass za TANZANIA