Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakili Peter Madeleka amesema kuwa hakuna sheria yoyote inayolipa Jeshi la Polisi mamlaka ya kutoa au kuzuia vibali vya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa. Akifafanua kuwa, kwa mujibu wa sheria za nchi, jukumu la vyama vya siasa vinapotaka kufanya mikutano hiyo sio kuomba kibali, bali ni kutoa taarifa tu kwa jeshi hilo ili liweze kuratibu ulinzi na usalama.
Soma: Madeleka: Katambi amekosea, hana mamlaka ya kumwamrisha IGP Madeleka
Madeleka alibainisha kuwa kifungu cha 43 cha Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi (Sura ya 322 ya Sheria za Tanzania) kimeeleza wazi utaratibu huo na hakuna mahali popote panapotaja neno "kibali".
"Hakuna sheria yoyote ile Tanzania ambayo imelipa mamlaka Jeshi la Polisi kutoa vibali.
Naomba nirudie. Hakuna sheria yoyote ile ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imelipa mamlaka Jeshi la Polisi liwe linatotoa vibali kwa vyama vya siasa ili viweze kufanya mikutano ya hadhara.
Hakuna mahala popote kwenye sheria ile pametajwa neno kibali. Kwamba Polisi wana mamlaka ya kutoa kibali au wana mamlaka ya kutokutoa kibali kwa chama chochote cha siasa kinachotaka kutoa... kufanya mikutano ya hadhara."