Madeleka kufungua kesi ili ukweli ujulikane kama waliouawa Vingunguti ni panya road

Madeleka kufungua kesi ili ukweli ujulikane kama waliouawa Vingunguti ni panya road

Japokuwa simuamini-amini mtu huyu, lakini kwenye hili naona ana hoja ya msingi. Namuunga mkono.
Endapo kama kweli Polisi wako serious ktk kuwashughulikia wahalifu-wauaji, ni kwa nini basi hawakuwapiga risasi wale Polisi wenzao waliompora na kumuua yule Mfanyabiashara kijana wa madini wa kule Mtwara?????
Waanze Kwanza kumpiga risasi yule Polisi mwenzao muuaji wa kule Mtwara anayeitwa Kalanje.
 
Iki ni kichak cha kuua watoto wetu polisi wanatakiwa kudhibitisha upanya road je wataweza?
Kwanini wawe ni Bakari na Shomari tu ina maana hawakuwa na wengine? Je kwanini hawakuwahoji wataje wenzao wanaoshirikiana nao? Je kwanini hao polisi waliwapiga risasi miguuni wale ndugu wa hao marehemu?
 
Mimi so mwanasheria Ila naisoma walau najua hakuna aliye na haki ya kutoa uhai wa mwenzake kwa namna banana yoyote,Kama Wana makosa ya kujibu watakamatwa na badae mahakama Ndo yenye haki ya kutoa haki kwa mjibu wa taratibu.Vinginevyo Ni kinyume na haki ya kuishi ya kila binadamu.Vinginevyo watenda wa hiki kitu huwa mwisho wao ni mbaya kumbuka kisa Cha Cain na Abel.Cain alikuwa mtu wa kutangatanga na mfadhaiko.Tufanye yote lakini tujue Kuna Mwenyezi Mungu.
 
Alichoandika Peter Madeleka.

Hakuna “PANYA ROAD” anastahili KUULIWA bila kufikishwa MAHAKAMANI kwa mujibu wa KATIBA na SHERIA za nchi yetu. Nitakwenda MAHAMANI ili KUTHIBITISHA UONGO juu ya MAUAJI ya RAIA hao hapo.

Upo USHAHIDI wa KIMAHAKAMA kwamba POLISI waliwahi KUUWA wafanyabiashara wa MADINI kutoka MAHENGE mwaka 2006 halafu wakasema ni “MAJAMBAZI” kumbe ni UONGO.
View attachment 2858737
Ngoja waue awapendao atarudi na taarifa nyingine

Kama hawajakufikia…. Kwa kimya
 
Akili zako ni ndogo sana.Kama huoni makosa kwenye huo ujinga wa polisi iko siku utayaona alafu utakua umechelewa.
Bahati mbaya zaidi ya 99% wakiochangia ni kama huyo uliemjibu. Inasikitisha sana.
 
Ngoja ukweli utajulikana tu kama hawa wahuni ni panya Road au laa maana hao jamaa kukupa kesi sio yako hawaoni tabu walimuua yule dogo huko Mtwara na dhahabu zake wakampa kesi ya mwizi wa boda boda harafu wanaelekeza kabisa jinsi walivyomuua huko kituoni...
 
Mm mwenyewe maelezo ya polisi sijayaelewa maana ndugu wanasema wamekuta maiti zimetobolewa macho lakin polisi wanasema katika harakati za kuwakamata ikatokea majibizano ya siraha japo vijana walikuwa na marungu pamoja na mapanga hivyo kupelekea polisi kuwatandika risasi za miguuni na walivyofikishwa hospital wakawa washakufa.

Swali langu ni hapo kwenye kutobolewa macho hao vijana hilo tukio lilitokea wakat Gani?
 
Jeshi letu ni la kisasa, mwenye rekodi za hao jamaa angesaidia sana. Haiwezi kuwa bure bure tu hao ni wahalifu sugu
Hao ni vibaka waliyokubuhu

Kwa watu wa vingunguti na wanaojuwa mazingira ya huko watakuwa wanajuwa naamanisha nini

Ukiona watu wanachukuliwa hatua hiyo jua system ishakuchokaaa

Ova
 
Akili zako ni ndogo sana.Kama huoni makosa kwenye huo ujinga wa polisi iko siku utayaona alafu utakua umechelewa.
Kwani mambo haya yameanza leo
Kuna watu wakichokwa huwa wanamalizwa tu
Nenda ilala kawaulize wale waliyokuwa wanajiita cha ukucha
Nini kiliwakuta,

Ova
 
Siyo probably ni panya road.
Kuna video Jambo TV walikuwa wanahoji watu mtaani hapo.

Kuna mama analia mtoto wake kafa alichomwa kisu.
Kuna mzee ulinzi shirikishi kakatwa mapanga.
Kuna kijana kachomwa visu mgongoni na mbavuni kwa nyuma wanasema utumbo ulikuwa inaonekana. Huyu kijana aliwasikia wanaitana majina yao wanasema tuondoke ishakuwa jau. Aliwajua hadi kwa sura.

Watu hatari na wapumbavu kama hao lazima wauwawe mapema kabla hawajawatia vilema na kuuwa watu wengi.
Madeleka asilete siasa au kutafuta umaarufu. Tunataka polisi waache kuwaondolea kero raia tuanze kupiga kelele polisi wako wapi hadi watu wanauwawa hivi?
Mimi huko kuna kijana wangu anaishi
Alipigwa mapanga mwili mzima
Watu na wazazi wa huko wanapenda kuwaficha wezi vibaka ambao ni watoto wao
Wakiambiwa wawafichue hawawafichui

Ova
 
Kwani mambo haya yameanza leo
Kuna watu wakichokwa huwa wanamalizwa tu
Nenda ilala kawaulize wale waliyokuwa wanajiita cha ukucha
Nini kiliwakuta,

Ova
Hao chaukucha family walikuwa balaa sana,walikuwa nyuma ya timu ya mpira walikuwa wakicheza mechi wakishinda watu wa barabarani watakoma,na wakifungwa refarii roho yake inawekwa rehani mpira hautafika dakika 90,kitambo sana umenikumbusha
 
Tutashukuru kwasababu ukweli utajulikana. Tena anzia na kazini kwa Marehemu mmoja wapo ambaye aliajiriwa na kampuni ya GS Group Limited na ametekwa muda mfupi toka atoke kazini
Mkuu watu wanafanya kazi 2 mbili kawaida tu.
Mchana kkoo,jioni anashika mapanga kwenda kupora.
Ukiona polisi wamedeal nae kimyakimya Ujue wanamtambua vizuri tu,
Tusiwalaumu.
Raia Wema wanatoa info toka hapo mtaani wanakokaa.
Kesi zikiwa nyingi inakua kero maana wao wataonekana hawatimizi wajibu wao.
Ndio mwisho wanakupeleka kusikoeleweka.
 
Wawe ni panya road au sio, kuna utawala wa sheria. Walipaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria baada ya uchunguzi na sio kuuawa kikatili namna hiyo. Tusitumie hisia kujadili mambo.
 
Back
Top Bottom