Madeleka kufungua kesi ili ukweli ujulikane kama waliouawa Vingunguti ni panya road

Madeleka kufungua kesi ili ukweli ujulikane kama waliouawa Vingunguti ni panya road

Naona tunashindwa kuelewana. Kama mtoto wa mtu anakamatwa na polisi, mzazi anakuja anamfhamini mwanae kwa maana ya kuenda kumkanya na anasisitiza ataacha. Polisi wanampa nafasi mzazi ya kufanya hizo. Miezi mitatu mingi anafanya tukio lingine na lingine. Anakamatwa akapelekwa jela kifungo kinaisha anatoka anakuja kulianzisha upya, unataka polisi wanafanye tena labda.
Nataka polisi wamkamate na kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

Mahakama imhukumu kwa mujibu wa sheria.

Wananchi wafuatilie mchakato.

Na kama wananchi wanataka jambazi akihukumiwa mara mbili, mara ya tatu auawe, basi wawashinikize wabunge wao itungwe hiyo sheria.

Ili hao Panya Road wanaorudia ujambazi wakikamatwa mara ya tatu, polisi wawapeleke mahakamani, mahakimu na majaji watumie sheria iliyopitishwa na bunge la wananchi kuwanyonga hao Panya Road.

Tusiwape polisi uwezo wa kufanya summary execution, kuua kwa kujiamulia wenyewe tu, kwa sababu wanaweza hata kukuua wewe ikiwa mmegombea demu na polisi tu kwa mfano.

Ukabambikwa u Panya Road, ukauawa bila hata kupewa nafasi ya kujitetea.

Usichoelewa nini hapo?
 
Nataka polisi wamkamate na kumfikisha mahakamani.

Kama imethibitika na wakazi wa mtaani na ndiyo wamepeleka malalamiko polisi basi nasema wauwawe tu.
Tukisubiri milolongo mirefu ya sheria na kusameheana kuna watu wasio kuwa na hatia watateseka na wengine kuuwa na Hawa wahalifu.
Huo muda wa kubembelezana na wahalifu watu wanauwawa huko mitaani.
Haki ya mhalifu kuishi isichukue au isinyime haki ya watu wasio kuwa na hatia ya kuishi.
 
Kiranga
-Una kubali hao panya road wapo?
-Pasipo kujali unajua furani na furani wanafanya, kama jibu lako ni hapana, naishia hapa. Ila,kama jibu lako ni ndio,
-umewahi shuhudia athari za matokeo yao?
-kama imetokea wakamshambulia mtu na kumuumiza, nani anaechangia matibabu na maisha yake na ya familia yake kwa ujumla?
-kwa hiyo unamaanisha una akili sana kuliko vyombo vya usalama?
-wanaokamatwa na kupelekwa mahakamani,umewahi kufatilia wakitoka wanafanya kazi gani?
-Haya,polisi wamekosea kushambulia na kuua. Je,unafikilia bila kufyatua lisasi,wao ndo wangekubali kukatwa mapanga?
-kwa kifupi unamaanisha vyombo vya usalama ndo vina makosa, raia hawana hatia?
-usitumie hisia,kubali. Kwani hapa ukikusanya watu mji mzima,nani atakili kuwa ni panya road?
-Kikubwa uelewe kwamba wakikuibukia,si kwamba hawana taarifa za uhakika.
Ni kweli mtu wa mtu anauma,kila mtu ataongea weeee,kama ilivyo hujawahi sikia jambazi anasemwa kwenye mazishi kwamba alikuwa kauzu, na ujambazi wake hauzuii familia yake kumlilia, hivyo acha wafanye kazi yao.
Mbona hawakukupiga lisasi wewe? Ni kwamba wale ndo walikuwa maarufu jiji zima?
Katibu unayoyisema, inaruhusu watu kuwaumiza wenzao? Anayeilinda ni nani? Mbona hata viongozi hawaishi kulalamikiwa kuwa hawailindi?
Damu zote sawa,usiwaonee huruma waharifu
Hata kama Panya Road wapo, Polisi hawana haki wala jukumu la kuhukumu. Haki na jukumu la kuhukumu ni mambo ya mahakama.

Polisi hawatakiwi hata kusema "huyu ni Panya Road". Hiyo ni kazi ya mahakama. Polisi wanaweza kusema "huyu tunamtuhumu kuwa ni Panya Road".

Habari za kama nimeshuhudia Panya Road wanachofanya na athari zake nani anaingia gharama kutibu ni irrelevant.

Hata tukisema tumpe huyo Panya Road jukumu la kulipia gharama, itabidi kwanza tuhakikishe mtu ni Panya Road na hakusingiziwa. Sasa, uhakiki unafanywa mahakamani, polisi hahukumu. Polisi anatuhumu.

Suala si mimi kuwa na akili sana kuliko vyombo vya usalama. Suala ni, vyombo vya usalama vinafuata sheria? Vyombo vya usalama kama polisi vunekatazwa kutia hukumu, vinatakiwa kutuhumu tu. Kazi ya kutoa hukumu ni ya mahakama, sasa, hata kumuita mtuhumiwa kuwa ni Oanya Road tu ni makosa. Huyo ni mtuhumuwa, tuiachie mahakama ihukumu kama anachotuhumiwa ni sawa, kama yeye ni Panya Road ama la.

Unauliza kama nimefuatilia wakitoka kwenye mifumo ya mahakama na sheria wanafanya kazi gani. Kama kuna tatizo kwenye mifumo ya mahakama, au mifumo ya sheria, badilisheni huko. Kama mnataka kuongeza vifungo, ongezeni huko. Kama mnasema hawa Panya Road hawakomi, wakitoka jela wanarudia, dawa tuwaue tu, tungeni sheria ya kunyonga Panya Road wote. Halafu wakishikwa na polisi, wapelekwe mahakamani, wakanyongwe baada ya kushindwa kesi mahakamani, sio wauliwe kwa summary execution na polisi bila hata ya kupata nafasi ya kujitetea.

Unauliza kama polisi wangekubali kukatwa mapanga, wewe unajuaje kuwa kweli polisi walikuwa wanataka kukatwa mapanga? Unawapaje polisi kuwa watu wanaokupa ushahidi na wanaohukumu kesi yao wenyewe? Tutajuaje kuwa walitaka kukatwa mapanga kweli, na hawajawaua tu watu ambao hata hawakutaka kuwakata mapanga, bila ya kuwa na uchunguzi ambao unafanywa na chombo tofauti na polisi wenyewe?

Yani ni hivi, polisi uliyegombana naye mtaani kwa sababu umemzidi katika kutongoza mwanamke, polisi huyo akakuchukia, akakuvizia usiku, akakupiga risasi na kukuzushia uongo kuwa wewe ni Panya Road ulitaka kumkata mapanga, akikufanyia hivyo bila hata ya kukupa nafasi ya kujitetea, utaona jambo hilo ni sawa?

Unauliza kama namaanisha vyombo vya usalama ndiyo vina hatia, raia hawana hatia. Simaanishi hivyo. Kuna raia wana hatia. Lakini, mahakama ndiyo inatoa hukumu raia ana hatia, polisi wanatuhumu tu. Polisi hawatakiwi kuhukumu na kuua.

Unaniambia nisitumie hisia. Mimi situmii hisia, natumia sheria. Sheria inakataza polisi kutia hukumu. Kutoa hukumu ni kazi ya mahakama. Hata kwenye kuripoti tu, polisi hatakiwi kusema "huyu ni Panya Road". Polisi anatakiwa kusema "huyu ni mtuhumiwa wa kuwa Panya Road". Mahakama ndiyo inaamua.

Wewe ndiye unatumia hisia. Mimi natumia sheria.

Katiba inasisitiza utawala wa sheria. Itawala wa sheria maana yake polisi wasihukumu, polisi wanatuhumu tu, kuhukumu ninkazi ya mahakama.

Mbona somo hili rahisi tu linakuwa gumu kueleweka?
 
Mnaanza kutetea ujinga pumbavu,panya road hastahili kuishi
 
Basi, ndo wameshauliwa, wengine walisha uliwa, na wengine bado watauwawa. Ni vizuli kufikilia kisheria, lakini haiwezekani kila jambo liende kisheria. Hata wewe ni shahidi,mambo yako yangekuwa chini ya sheria,hakika kuna vingi usingepoteza.
 
Kama imethibitika na wakazi wa mtaani na ndiyo wamepeleka malalamiko polisi basi nasema wauwawe tu.
Tukisubiri milolongo mirefu ya sheria na kusameheana kuna watu wasio kuwa na hatia watateseka na wengine kuuwa na Hawa wahalifu.
Huo muda wa kubembelezana na wahalifu watu wanauwawa huko mitaani.
Haki ya mhalifu kuishi isichukue au isinyime haki ya watu wasio kuwa na hatia ya kuishi.
Haya ndiyo mambo yaliyopelekea bibi wazee kuuawa miaka ya sabini kwa sababu wana macho mekundu wakaitwa wachawi, mpaka Waziri wa Mambo ya Ndani wa wakati huo, Ali Hassan Mwinyi akajiuzulu.

Kumbe wale bibi wazee wamekuwa na macho mekundu kwa sababu wamechochea moto wa kuni zenye moshi mkali kwa miaka mingi tu.

Kuna siku mzee mmoja msomi alipata funzo kubwa maishani mwake.

Alikuwa anawaona vijana wakikaa kijiweni karibu na kwake.

Akawa anawachukulia wale vijana kama wavuta bangi wahuni tu.

Siku moja, wakati anatoka kwake na gari lake, gari likazimika.

Mzee hajui chochote kuhusu gari zaidi ya kuendesha.

Wale vijana wakamuona mzee jirani kakwama, wakamsaidia, wakamtengenezea gari, mpaka likapona. Tena alitaka kuwalipa wakakataa, wakasema wewe mzee wetu tunakujua.

Yule mzee alijisikia vibaya sana kwamba kawachukulia wale vijana wahuni wavuta bangi, kumbe ni vijana poa tu, tena wengine mafundi magari huwa wanakuja kukaa maskani baada ya kazi zao.

Sasa hapo utaona kuna perception na reality. Jamii yetu inaenda sana na perception. Ndiyo maana wezi wakubwa washatujulia wanavaa suti na kutuibia sana. Na unaweza kukuta mtu roho safi kavaa jeans ya kuchanika na ana dreadlocks, anaonekana Panya Road.

Sasa, katika jamii yenye utata mwingi kama huu, ni muhimu mambo yachambuliwe kimahakama ili kujiridhisha nani Panya Road na nani si Panya Road.

Vinginevyo, tutaua vijana wengi wasio na hatia wakati majambazi wenyewe tunawasifia.
 
Wale vijana wa vingunguti mimi nilikuwa mzito sana kuwalaumu au kuwaunga mkono polisi.
Sababu jeshi la polisi lina historia mbaya rejea kesi ya kijana wa madini aliyeuwawa Mtwara mikononi mwa polisi, pia rejea wafanya biashara wa madini wa Mahenge kesi ya akina Zombe.

Ilibidi nifuatilie ukweli juu ya hao vijana wa Vingunguti. Kila kitu kipo wazi na Madeleka angeweza kupata taarifa.
Sidhani kama jeshi la polisi limekodi waandishi wa habari walio hoji wahanga wa hao vijana. Video za maoni yao zimejaa mitandaoni.

Yupo kijana mmoja mkoa wa Pwani alikuwa kibaka muuwaji akafikishwa polisi anaachiwa mara kadhaa sababu za ushahidi au anatoroka, na mara ya mwisho alipelekwa na mama yake polisi wakamuachia.
Kijana akauwa watu wengi zaidi aliporudi mtaani mpaka mara ya mwisho mwaka jana nadhani August aliuwa watu wawili girlfriend wake, na rafiki yake huyo kibaka. Polisi na wananchi wakamchoka akaishia kama hao madogo. Wananchi walipolaumiwa wanaficha mhalifu wakajibu huyo mtu amefikishwa kwenu mara kadhaa anatoka.

Mlitakata na hawa madogo wa Vingunguti waachwe uraiani wauwe watu wengi zaidi au wawatie vilema watu? Kuna mama kapiteza mtoto alichomwa kisu, kuna jamaa kapigwa mapanga, Kuna kijana kachomwa visu mgongoni na mbavuni utumbo ulionekana. Matukio yote hapo mtaani kwa hao vijana.
Watu wanawaona wanawajua kwa sura na wanasikia wanaitana kwa majina wakati wa matukio.

Watu kama hao wanastahili kuondoshwa mapema, wanao uwawa kimakosa na polisi haipiti siku 5 ungesikia polisi nao wako matatani kama kesi ya Mtwara au ya akina Zombe.
Mimi siongelei vijana wa Vingunguti tu.

Mimi naongelea tatizo katika suala zima la polisi kufanya summary execution na matatizo yake kifalsafa, kisheria, kwenye utawala wa kikatiba, kwenye jamii inayofuata due process bila kutaka shortcut.

Hata jambazi ana haki ya kuhukumiwa mahakamani kwa due process.

Hii haimpi faida jambazi tu, hii inamlinda polisi katika kuhakiki kuwa kafanya kazi yake kwa haki, hii inakulinda hata wewe mwananchi usiye na hatia kuhakikisha kuwa polisi wanatuhumu wahalifu kweli na hawatuhumu au kuhukumu raia wasio na hatia.

Watanzania wengi hata wasio na hatia wanaotetea polisi kuua kiholela hawaelewi kuwa kutetea due process ni kutetea haki zao za kutobebeshwa hukumu za summary execution na polisi bila kufuata due process.

Ndiyo maana wengi bado hawaelewi umuhimu wa kesi ya Peter Madeleka.
 
Basi, ndo wameshauliwa, wengina walisha uliwa, na wengine bado watauwawa. Ni vizuli kufikilia kisheria, lakini haiwezekani kila jambo liende kisheria. Hata wewe ni shahidi,mambo yako yangekuwa chini ya sheria,hakika kuna vingi usingepoteza.
Sawa.

Basi na wewe waje kukuua bila kufuata sheria, kwa sababu haiwezekani kila kitu kifuate sheria.

Utakubali?
 
Mnaanza kutetea ujinga pumbavu,panya road hastahili kuishi
Hata ikiwa kweli Panya Road hastahili kuishi.

Basi, weka sheria ya kuua Panya Road wote. Pitisha muswada bungeni, upate saini ya rais na kuwa sheria.

Wahukumu watuhumiwa mahakamani, wakishindwa kesi, waue kwa mujibu wa sheria.

Ukiwapa polisi ruhusa ya kuua mtu kwa sababu ya tuhuma tu kuwa huyu ni Panya Road, tuhuma ambazo hazijahakikiwa na mahakama, tunaweza kugombana mimi na wewe hapa, halafu mimi nikakukodishia polisi tu, nikawalipa hela, nikawaambia "Huyu hapa Nandiaye, nataka mumuue kwa kumsingizia kuwa ni Panya Road".

Wakakuvizia sehemu usiku, wakakumiminia risasi kwa kisingizio kuwa wewe ni Panya Road, ulitaka kuwapiga mapanga.

Ukafa bila hata kupata nafasi ya kujitetea.

Utafurahia kifo hicho?
 
Sasa hivi huyu pimbi Madeleka anatafuta umaarufu , si aingie kwenye siasa tu??nyoko zake.
Hii ni logical fallacy ya ad hominem.

Umeshindwa kujibu hoja za Madeleka, umeishia kumshambulia yeye kama mtu binafsi.

Hii ni dalili ya mtu asiye na hoja.
 
"Those who would give up essential Liberty, to purchase a little temporary Safety, deserve neither Liberty nor Safety."

Benjamin Franklin.
 
Kama hawa watu ni Panya Road au si Panya Road si issue.

Issue ni kwamba wameuawa kwa summary execution bila kupata nafasi ya kujitetea mahakamani na mahakama kuwahukumu.

Na hili linatoa nafasi kwa mtu yeyote, aliye au asiye na hatia, kuuawa hivyo hivyo.
Unaonaje haya malalamiko yako ukiyapeleka kituo cha polisi kilichohusika na maumivu uliyonayo!?
 
Kama sio panya road mtueleze walikuwa wanajishughulisha na nini
 
Kama sio panya road mtueleze walikuwa wanajishughulisha na nini
Kama hawa watuhumiwa ni au si Panya Road si issue.

Issue ni kwamba wameuawa kwa summary execution, bila kuhukumiwa na mahakama, kwa namna yenye utata, ambayo inawafanya polisi kuwa ndio mashahidi, washitaki na mahakimu wa kesi yao wenyewe, na kwa namna ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya raia yeyote mwingine, mwenye hatia au asiye na hatia.

Tukihalalisha polisi kuua kiholelaholela, kesho unaweza kugombana na shosti kwenye biashara zenu, akakukodia polisi wakutafute usiku na kukumiminia risasi kwa tuhuma za mchongo kwamba wewe ni Panya Road.

Ukose hata nafasi ya kujitetea na kutoa ushahidi wako kuwa wewe ni mfanyabiashara halali, si Panya Road.
 
Unaonaje haya malalamiko yako ukiyapeleka kituo cha polisi kilichohusika na maumivu uliyonayo!?
Kituo cha polisi cha wapi mkuu? Unaishi kwa kukariri kuwa kila mtu yupo kwa Bi Mkubwa?

Mimi sina maumivu, naeleza point za msimamo wangu wa kifalsafa.

Watanzania wengi kama wewe mna tatizo la kufanya abstract thinking.

Hamna uwezo mkubwa wa kuelewa hoja ya kifalsafa, hamuelewi abstract thinking.

Mimi nilishapiga kura kwa miguu enzi za utawala wa Mkapa na kutabiri haya yote yatakuja kama mistari ya Nostradamus.

Nakula lasagna kwa umma.

Maumivu yataanzia wapi?
 
Nimesikiliza na kusoma mengi kuhusiana na tukio hili ila nilichogundua Binadamu wengi tumejaa unafiki
mfano rahisi
Kamanda wa polisi alieleza namna walivyowakamata watuhumiwa
yan waliwataka wasimame ila wakamatwe ila wao walikataa na kutaka kutumia silaha zao za jadi yan mapanga kuwadhuru polisi. polisi wakatumia risasi za moto kuwazuia.
kisharia hii inaruhusiwa kabisa

Sheria inasema unaweza tumia bunduki kujilinda ama kulinda mali zako. sasa pale polisi walipiga risasi juu kuwaonya ila wao wakakaidi,polisi wakatumia nguvu kuwatuliza.

swali nalojiuliza
Tulitaka polisi wapigwe mapanga na hao vijana alafu leo tuwatukane kuwa walikuwa na silaha ila wameshindwa kuzitumia kujilindaaa?

je polisi tulitaka wasijilinde ilihali wahalofu walitumia mapanga kujihamii?

Sala la polisi kutumia bunduki mimi naona hao vijana ndo waliwashawishi.
laiti wasingekuwa na mapanga naamini wangekamatwa vizuri.

NAELEZA KISA KIMOJA KWA UFUPI
jirani kwetu kulikuwa na mwiz mbabe sana yan alikuwa anaogopwa sana mtaani na alikuwa akija kwako lazma achukue kila kilicho chale ila alipokufa

Risala au wosia ulikuwa hivi
Alikuwa mtu mcheshi na mtu wa watu, pengo lake halitazibika.

Unafiki mkubwa Binadam tuko nao.
kitu kama ni cheusi kisemwe na kama chekundu kisemwe kwa dhamira ya kuionya na kuielimisha jamii.
Nachukia wahalifu maana nimeshapata madhara makubwa sana na hao ndugu zenu wahalifu mnaowapaka mafuta na kuwapulizia marashi
 
Back
Top Bottom