Kiranga
-Una kubali hao panya road wapo?
-Pasipo kujali unajua furani na furani wanafanya, kama jibu lako ni hapana, naishia hapa. Ila,kama jibu lako ni ndio,
-umewahi shuhudia athari za matokeo yao?
-kama imetokea wakamshambulia mtu na kumuumiza, nani anaechangia matibabu na maisha yake na ya familia yake kwa ujumla?
-kwa hiyo unamaanisha una akili sana kuliko vyombo vya usalama?
-wanaokamatwa na kupelekwa mahakamani,umewahi kufatilia wakitoka wanafanya kazi gani?
-Haya,polisi wamekosea kushambulia na kuua. Je,unafikilia bila kufyatua lisasi,wao ndo wangekubali kukatwa mapanga?
-kwa kifupi unamaanisha vyombo vya usalama ndo vina makosa, raia hawana hatia?
-usitumie hisia,kubali. Kwani hapa ukikusanya watu mji mzima,nani atakili kuwa ni panya road?
-Kikubwa uelewe kwamba wakikuibukia,si kwamba hawana taarifa za uhakika.
Ni kweli mtu wa mtu anauma,kila mtu ataongea weeee,kama ilivyo hujawahi sikia jambazi anasemwa kwenye mazishi kwamba alikuwa kauzu, na ujambazi wake hauzuii familia yake kumlilia, hivyo acha wafanye kazi yao.
Mbona hawakukupiga lisasi wewe? Ni kwamba wale ndo walikuwa maarufu jiji zima?
Katibu unayoyisema, inaruhusu watu kuwaumiza wenzao? Anayeilinda ni nani? Mbona hata viongozi hawaishi kulalamikiwa kuwa hawailindi?
Damu zote sawa,usiwaonee huruma waharifu
Hata kama Panya Road wapo, Polisi hawana haki wala jukumu la kuhukumu. Haki na jukumu la kuhukumu ni mambo ya mahakama.
Polisi hawatakiwi hata kusema "huyu ni Panya Road". Hiyo ni kazi ya mahakama. Polisi wanaweza kusema "huyu tunamtuhumu kuwa ni Panya Road".
Habari za kama nimeshuhudia Panya Road wanachofanya na athari zake nani anaingia gharama kutibu ni irrelevant.
Hata tukisema tumpe huyo Panya Road jukumu la kulipia gharama, itabidi kwanza tuhakikishe mtu ni Panya Road na hakusingiziwa. Sasa, uhakiki unafanywa mahakamani, polisi hahukumu. Polisi anatuhumu.
Suala si mimi kuwa na akili sana kuliko vyombo vya usalama. Suala ni, vyombo vya usalama vinafuata sheria? Vyombo vya usalama kama polisi vunekatazwa kutia hukumu, vinatakiwa kutuhumu tu. Kazi ya kutoa hukumu ni ya mahakama, sasa, hata kumuita mtuhumiwa kuwa ni Oanya Road tu ni makosa. Huyo ni mtuhumuwa, tuiachie mahakama ihukumu kama anachotuhumiwa ni sawa, kama yeye ni Panya Road ama la.
Unauliza kama nimefuatilia wakitoka kwenye mifumo ya mahakama na sheria wanafanya kazi gani. Kama kuna tatizo kwenye mifumo ya mahakama, au mifumo ya sheria, badilisheni huko. Kama mnataka kuongeza vifungo, ongezeni huko. Kama mnasema hawa Panya Road hawakomi, wakitoka jela wanarudia, dawa tuwaue tu, tungeni sheria ya kunyonga Panya Road wote. Halafu wakishikwa na polisi, wapelekwe mahakamani, wakanyongwe baada ya kushindwa kesi mahakamani, sio wauliwe kwa summary execution na polisi bila hata ya kupata nafasi ya kujitetea.
Unauliza kama polisi wangekubali kukatwa mapanga, wewe unajuaje kuwa kweli polisi walikuwa wanataka kukatwa mapanga? Unawapaje polisi kuwa watu wanaokupa ushahidi na wanaohukumu kesi yao wenyewe? Tutajuaje kuwa walitaka kukatwa mapanga kweli, na hawajawaua tu watu ambao hata hawakutaka kuwakata mapanga, bila ya kuwa na uchunguzi ambao unafanywa na chombo tofauti na polisi wenyewe?
Yani ni hivi, polisi uliyegombana naye mtaani kwa sababu umemzidi katika kutongoza mwanamke, polisi huyo akakuchukia, akakuvizia usiku, akakupiga risasi na kukuzushia uongo kuwa wewe ni Panya Road ulitaka kumkata mapanga, akikufanyia hivyo bila hata ya kukupa nafasi ya kujitetea, utaona jambo hilo ni sawa?
Unauliza kama namaanisha vyombo vya usalama ndiyo vina hatia, raia hawana hatia. Simaanishi hivyo. Kuna raia wana hatia. Lakini, mahakama ndiyo inatoa hukumu raia ana hatia, polisi wanatuhumu tu. Polisi hawatakiwi kuhukumu na kuua.
Unaniambia nisitumie hisia. Mimi situmii hisia, natumia sheria. Sheria inakataza polisi kutia hukumu. Kutoa hukumu ni kazi ya mahakama. Hata kwenye kuripoti tu, polisi hatakiwi kusema "huyu ni Panya Road". Polisi anatakiwa kusema "huyu ni mtuhumiwa wa kuwa Panya Road". Mahakama ndiyo inaamua.
Wewe ndiye unatumia hisia. Mimi natumia sheria.
Katiba inasisitiza utawala wa sheria. Itawala wa sheria maana yake polisi wasihukumu, polisi wanatuhumu tu, kuhukumu ninkazi ya mahakama.
Mbona somo hili rahisi tu linakuwa gumu kueleweka?