Madeni ya Taifa: Kuna kitu very serious CAG amekisema. Hii kitu haiko sawa. Je, tunakwenda wapi?

Pascal kuna tabia za ajabu sana zinafanyika nchi hii kwa kuendekeza sifa. Baada ya ile kesi kule Afrika kusini kutupwa kutokana na errors katika ufunguaji wa shauri, tulipaswa kurudi hapa na kujipanga jinsi ya kumalizana na Mkulima hata kwa kulipana kidogo kidogo.
Lakini kwa ujinga wetu eti tukaanza matambo na majidai hadi bungeni.
Kwamba timu yetu ya watu wenye ma PhD ya sheria imemgalagaza mzungu na hawa makuwadi wa mabeberu waliopo hapa nchini. Mpaka raia wenzetu wakatuhumiwa, kubezwa na kutukanwa. Na tulitamba kweli kweli. Rais akachekelea, Kabudi akacheka na kukejeli, PM na Spika wakatamba. Hata hao mawakili wa serikali walio kuwa SA wakapokewa kama mashujaa kwa kuzima moto wa mkulima. Kumbe moto wameuzima kwa kuufukia na majivu bado unawaka.
Rais alilishwa matango pori akayala sasa tumbo limevurugika lakini KABUDI YUPO TU OFISINI.
Mawakili wakiongozwa na yule naibu waziri walio tulisha nasi ubuyu na hawakutoa ushauri wapo tuu ofisini kwa sababu walikuja na mapambio ya kumsifu Rais.
Kwa mwendo huu Rais (hili ni lake mwenyewe asituhusishe) ataendelea kuaibishwa na hao waimbaji wake wa mapambio.
 
Kuna watu hawatabaki salama kufuatia kukamatwa tena kwa ndege. Najua rais atabeba point 3. Kama sio jumapili ya kesho trh 24.11.2019 sijui. Labda vile yupo dodoma.
 
Kudos Bro kwa caution uliyoitoa way back before. You deserve my compliments.

Naomba ili kujitendea haki fani yako wakumbushe na award aliyonayo Symbion Power na Standard Chatered HongKong dhidi ya TANESCO.
Bahati mbaya sana, JK alituingiza kwenye Open Government Partnership Initiative, OGP, ambapo serikali inakuwa transparent kwenye kila kitu cha public interest, lakini awamu hii Tanzania tukajitoa, hakuna yoyote anayeuliza zile bombardier ziliposhikwa kwa mara ya kwanza Canada, tulilipa kiasi gani, imefanywa siri!. Ile tozo ta Dowans, pia tulilipa kwa siri, Watanzania hatukuambiwa, na waliotushauri tuvunje tuu mikataba, hatutadaiwa, wapo!. Tulipodaiwa wakajiapisha "over my dead body", hatulipi!, ukweli ni kuwa tumelipa kwa siri na wahusika bado wapo tuu, hivyo hiyo tozo ya Simbion na Stan Chart HGK, tutalipa tuu kimya kimya kwa siri.
P
 
Umeandika with deep feelings!!
 
Acha tulipe tuu. Uongozi huu unaufagilia sana sana wala huhitaji kulalamika. Unataka nani aondoke ofisini?
 
Acha tulipe tuu. Uongozi huu unaufagilia sana sana wala huhitaji kulalamika. Unataka nani aondoke ofisini?
Spika, waziri wa fedha, waziri wa Mambo ya nje,AG, waziri mkuu na yeye mwenyewe kwa kukubali kufanyia kazi ushauri mbovu na kutumia Kodi zetu bila kutushirikisha!
 
Kuna wanaosema Rais anaonewa Wivu na mabeberu, ila sijawahi kuelewa ni kwa lipi hasa. Nasikia Nyerere naye alikuwa halipi madeni,alikuwa mbishi kweli kweli, labda naye Rais Magufuli anafanya kama Nyerere.
 
Mkuu Capt Tamar ,
Asante,
Ubarikiwe
Japo sina uhakika, kwavile siwezi kusoma mabandiko ya watu wote humu, lakini humu JF, mimi ni miongoni mwa tuliomuongelea sana CAG, Ofisi ya CAG na Ripoti za CAG!.
Nakutakia Jumapili Njema
P
 
ATC hasara bilioni 60!.
Taarifa ya CAG.
Kuna vitu kuna watu tulisema humu, tukanyooshewa vidole vya kukosa uzalendo!. Sasa ukweli umethibitika!.
60 billions kwa mwaka!, it's not a joke!
Duh...!.

P
 
Mnhhh!!! Mbona ni hatari mkuu
 
Bilion 60 kwa Mwaka mmoja na limekuwa likiingiza hasara nchi kwa miaka mitano mfululizo.[emoji35]
 
Mkuu Bashir Yakub , kwanza asante kwa hii. Vipi uliwahi kumsikia Prof. Asad hapa?.
Msikilize kwa makini sana, na maneno haya tena aliyasema akiwa CAG

P.
 
Kati ya wana CCM waliojitokeza kugombea kuteuliwa kugombea usipika, kuna mgombea mmoja tuu akipitishwa, upuuzi kama ulivyo zungumzwa humu, hauwezi kujirudia.

P
 
Wampe Chenge hakuna mwingine !!
 
Mkuu Petro E. Mselewa, kwanza asante kwa bandiko hili Ripoti ya CAG: Bunge limehitimisha mjadala leo, nini kitafuata? Waliohusika na ufisadi na ubadhirifu watafanywaje?
Very objective, mimi msimamo wangu kuhusu Bunge letu, kwenye hoja ya bunge kuisimamia serikali, bado haujabadilika ni ule ule wa bunge lililopita Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?
Na hapa Je, Bunge letu ni Bunge Butu?. Angalia Bunge la Uingereza lenye meno linavyong'ata Serikali. Je, Kuna ubaya tukiiga?
Japo Rais Samia ametoa maelekezo makali kwa maofisa masuhuli, hii ni kesi ya nyani kumpelekea ngedere!.
Kilichopaswa kufanywa on the first place ni kila aliyetajwa kwenye ripoti ya CAG, alipaswa apishe kwanza, akiwa cleared ndipo arudishwe!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…