Madeni ya Taifa: Kuna kitu very serious CAG amekisema. Hii kitu haiko sawa. Je, tunakwenda wapi?

Madeni ya Taifa: Kuna kitu very serious CAG amekisema. Hii kitu haiko sawa. Je, tunakwenda wapi?

Wanabodi,
Wanabodi, hili ni bandiko kuhusu Kitu Very Serious CAG Prof. Mussa Asad Amekisema!. Kama Hii ni Kweli, This is Not Right At All, Hivyo Kwa Mambo Kama Haya, Jee Tanzania Tunakwenda Wap?!.

Tanzania ni nchi yetu sote na sio mali ya mtu na inaendeshwa kwa misingi ya katiba kwa mujibu wa sheria, taratibu kanuni, haiwezekani jambo lililopitishwa na Bunge kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, halafu lisitekelezwe kama sheria ilivyoelekeza, halafu wakati huo huo kuna jambo jingine ambalo halijajadiliwa, halijatengewa budget, hivyo halijaombewa budget, ikawasilishwa bungeni, ikajadiliwa, ikapitishwa, lakini likatekelezwa. Jee limetekelezwa kwa fedha kutoka vote gani, ikiyoidhinishwa na nani?.

Ninavyofahamu mimi serikali hutekeleza majukumu yake yote kupitia bajeti ikiyoidhinishwa na Bunge kupitia vifungu mbalimbali yaani Vote na Sub Vote. Hizi fedha hutungiwa sheria na kupitishwa na Bunge kama sheria ya fedha/budget.

Kabla fedha zozote za serikali zilizopitishwa na Bunge haziwezi kutumika kwanza Kabla hazijaidhinishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, na hii ndio role ya CAG kama Mdhibiti Mkuu wa Matumizi ya serikali, kudhibiti matumizi ya serikali yaliyoidhinishwa na Bunge, na kisha baada ya matumizi, CAG hurejea kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha hizo kama zilitumika kama zilivyokusudiwa na hii ndio role ya CAG kama Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Naomba umsikilize kwa makini hapa, CAG, Prof. Mussa Assad kuna kitu very very serious anakizungumza kupitia Habari ya Channel Ten. (Nafuatilia video clip).

Nilichokisikia mimi kwa masikio yangu ni... katika bajeti ya serikali iliyopitishwa na Bunge, kuna baadhi ya taasisi mpaka sasa the final quoter of the the budget year, zimeishapewa mgao wa asilimia 18% tuu ya bajeti zake, kwa hoja kuwa serikali haina fedha, lakini at the same time, kuna wizara nyingine zimefanya matumizi ya ziada ya zaidi ya asilimia 200%!.

Hii maana yake kuna maeneo serikali imefanya matumizi makubwa ambayo hayakuwepo kwenye budget ya serikali, hayakuletwa bungeni, hayakujadiliwa wala kuidhinishwa na Bunge na hivyo hayana Vote wala hayakudhibitiwa na CAG, lakini serikali ikafanya matumizi hayo kinyume cha sheria, taratibu na kanuni.

Maswali ni
1. Kama serikali imeshindwa kulipa OC za baadhi ya taasisi kwa hoja kuwa haina fedha, jee hizo fedha zilizotumika kufanya matumizi ambayo they were not budgeted, zimetoka wapi?!. Kama kulikuwa na pot fulani yenye fedha ambazo ziliwafanyiwa ring fencing mapema zikafukiwa na sasa ndio zimefukuliwa, tuelezwe serikali iwe very transparent katika hili kama sehemu ya utekelezaji wa Open Government Initiatives.

2. Matumizi yoyote ya serikali lazima yaidhinishwe na Bunge na kuidhinishwa na CAG katika the Principles of Check and Balance and Separation of Powers. Hii maana yake kuna mtu yeye amejifanya ndio serikali akapanga budget, kisha akajifanya Bunge akaipitisha hiyo budget, akajifanya CAG, akaidhinisha hiyo budget na kuitumia!. How can this be?.

Ingekuwa ni nchi za wenzetu kamwe wasingekubali hili lifanyike huku na wao wapo tuu na wanaangalia!.

To be honest, nina mashaka sana na Ripoti ya CAG itakayotoka kuelezea madudu hayo haswa kwa kuzingatia kabla Ripoti ya CAG haijawasilishwa Bungeni na kuwa ni public document, lazima kwanza ipitishwe mahali mtu fulani aione, aridhike ndipo iende Bungeni. Kwa vile Ripoti hii itaonyesha haya madudu ya jinsi Bunge linavyokuwa undermined na jinsi CAG anavyokuwa
undermined!. Jee Ripoti hiyo ikapitishwa hivyo hivyo ilivyo? ,au itarudishwa na CAG kulazimishwa kuficha madudu haya kwa kuandaa Ripoti nyingine isiyo muonyesha huyo anayejifanya serikali, kisha anajigeuza Bunge na kujigeuza CAG kwa kufanya matumizi bila kuidhinishwa na Bunge na CAG, ningekuwa mimi GAC, baada ya kufanyiwa haya, sijui ningekuwa wapi maana zamani angeishaikuta barua yangu mezani kwake kitambo kulinda heshima yangu.

Ila kama matumizi haya unbudgeted ni ya fedha zake binafsi kutoka mfukoni mwake, then it's ok, lakini kama ni fedha za serikali, fedha za Watanzania, hatuwezi kuacha fedha zetu zikatumika bila kufuata taratibu za matumizi ya fedha za umma no matter how matumizi hayo ni mazuri kiasi gani, unless ni dharura kama Tetemeko la Bukoba, lakini kwa nchi inayojitapa ni nchi yenye kufuata katiba na kuheshimu the rule of law, lazima ifuate sheria, taratibu na kanuni. Sasa kama hili ni kweli, huu nao sio ufisadi?.

NB. Kama matumizi haya yaliyoidhinishwa na Bunge ni yale yaliyotumika kununulia zile Bombardier za ATC na haya yaliyotumika kuhamia Dodoma, then huu ni ufisadi mzuri, ufisadi wa kimaendeleo ambao mimi naaunga mkono kama ninavyounga mkono udikiteta ukifanyika kwa nia njema.

Jumatano Njema.
Pakali
Rejea
Tangazo hili la serikali halimhusu CAG.
Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya Kujenga Nidhamu au Udikiteta Tuu?!.

Prof. Assad amlipua Magufuli kwa ufisadi uuzaji wa nyumba za Serikali
Huyo CAG unayemzungumzia ni wa nchi gani? TZ? Yeye siyo wa kwanza na hata Rais huyu siyo wa kwanza. Hilo bunge pia usilitumaini kabisa! Bajeti za utawala uliopita, kulikuwa na kitu kinaitwa pesa za chai ambazo kila wizara ilikuwa ikijiwekea pesa hizo, kubwa kuliko hata bajeti zao za maendeleo. CAG alikuwepo na mutangulizi wake alikuwepo.

CAG hatakiwi kusimamia matumizi yalivyopangwa na Bunge tu, anatakiwa pia aangalie kama pesa inayopangwa inaleta tija. Value for money. Jiulize iliwezekanaje watu wachote pesa za serikali na kuziita ni za chai. Ukweli walikuwa wakijipangia safari za nje. Unakuta Katibu mkuu ana safari za nje kama kumi. Anapanga bila hata kujua kama atatakiwa kusafiri. RAis naye alisafiri anavyotaka.

Bora rais huyu. hata kama ni nje ya mpango wa bajeti, kinachofanyika kinaonekana maana hata yanayopitishwa na Bunge ni mambo ya ajabu tuuu.
 
Hivi sasa technical hewa wanaongezeka sana. CAG anafanyaje kazi? Wabunge wanapitisha vitu ambavyo havitendewi kazi na vinavyotendewa ni vile ambavyo hata havikujadiliwa. Sijui justification ya wao kuendelea kuwepo ni ipi?. Anyway, bunge linarejea hivi karibuni, watatetea uwepo wao.
Ukitaka vinavyojadiliwa vitendewe haki, lazima tuangalie ubora wa anayejadili kule Bungeni. Kweli kuna ubora wowote ktk hilo bunge, unaotegemea uongoze serikali?

Watu wanajadili posho zao kwa nguvu sanaaa!
 
Hawa si ndio huwa wanapewa rushwa na halmashauri kuzipa hati safi kutokana na ubadhirifu sasa kuna haja gani ya kupoteza pesa kwenye taasisi kama hiyo..siku CAG ni watu wa usalama wa taifa.. Nilichogundua ukiwa na utawala bora hutaitaji hiyo taasisi.
Leta taarifa sahihi halmashauri gani ilitoa rushwa Kwa CAG?USIPOLETA HUO USHAHIDI UTAKUWA HUNA TOFAUTI NA MMBEA..
 
Ni lazima aseme Mkuu anasimamia mamlaka aliyokuwa nayo kama CAG . Huyu dikteta uchwara akiendelea kuogopwa ataendelea kuivuruga nchi yetu katika kiwango cha kutisha na tutabaki tunaulizana wakati huyu dikteta uchwara akiivuruga nchi yetu kiasi hiki Watanzania tulikuwa wapi!? Kwanini tulikaa kimya? Tanzania ni yetu sote huyu hana hati miliki lazima aambiwe kweli bila woga wa kufukuzwa kazi. Atafukuza wangapi!?

Kwa hawa waheshimiwa wanavyosukuma gozi huyu CAG aanze kutafuta kazi.
 
Huyo CAG unayemzungumzia ni wa nchi gani? TZ? Yeye siyo wa kwanza na hata Rais huyu siyo wa kwanza. Hilo bunge pia usilitumaini kabisa! Bajeti za utawala uliopita, kulikuwa na kitu kinaitwa pesa za chai ambazo kila wizara ilikuwa ikijiwekea pesa hizo, kubwa kuliko hata bajeti zao za maendeleo. CAG alikuwepo na mutangulizi wake alikuwepo.

CAG hatakiwi kusimamia matumizi yalivyopangwa na Bunge tu, anatakiwa pia aangalie kama pesa inayopangwa inaleta tija. Value for money. Jiulize iliwezekanaje watu wachote pesa za serikali na kuziita ni za chai. Ukweli walikuwa wakijipangia safari za nje. Unakuta Katibu mkuu ana safari za nje kama kumi. Anapanga bila hata kujua kama atatakiwa kusafiri. RAis naye alisafiri anavyotaka.

Bora rais huyu. hata kama ni nje ya mpango wa bajeti, kinachofanyika kinaonekana maana hata yanayopitishwa na Bunge ni mambo ya ajabu tuuu.
So kuna point gani ya kuwalipa wabunge hela zote kumbe wanajadili tu upupu? basi tusiwe na bunge au tubadili vigezo vya mtu kuwa mbunge??
 
Mengi kama haya yapo nchi hii

na umeweza kugundua kwa sababu ya utashi wako murua

watanzania wengi wako bize na habari za umbeaumbea , ukuda ukuda, wako bize na bashite!!

mambo kama haya huwezi kut wanafuatilia na wanakuwa serious!! haipo
Unataka Watanzania wafanye nini kwa mtu ambaye hashauriki wala haambiliki!! Mtu ambaye kila kukicha ni vitisho kwa wafanyakazi na watumishi wa umma! Mtu ambaye anajifanya kujua kila kitu wakati kichwani ni mweupe!!

Bila shaka wewe ndiye mbea, mkuda na bashite sijui unajikomba nini?!
 
Serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli imekiri kukabiliwa na ukosefu wa fedha, hali inayoathiri utekelezaji wa shughuli zake za kila siku.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Khatibu Kazungu, wakati akijibu hotuba ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Juma Assad, kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

“Ukosefu wa fedha haupo kwenu (CAG) tu, upo serikalini kote; nikubaliane na ushauri wa Prof. (Assad), kwamba tunatakiwa kujiongeza kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato ya serikali na kusimamia vizuri makusanyo yake,” alisema Kazungu.

Prof. Assad, alisema ofisi yake inakabiliwa na wakati mgumu kiutendaji, kutokana na serikali kuchelewa au kutoipelekea fedha zinazoidhinishwa na Bunge kwenye bajeti hivyo kufanya kazi ya ukaguzi wa fedha kwenye halmashauri kuwa ngumu.

Alitoa mfano wa bajeti ya ofisi hiyo katika fungu la OC kwa Mwaka 2016/17, kwamba ilikuwa Shilingi Bilioni 18 lakini mpaka Agosti mwaka jana kiasi kilichokuwa kimepokewa hakikuzidi Shilingi Bilioni 2.

“Nililazimika kuzungumza na Mheshimiwa mwenyewe (Rais John Magufuli), kwamb bila kupata Shilingi Bilioni 10 wataalamu wasingeenda kufanya ukaguzi, akaahidi kulishughulikia,” alieleza.

Prof. Assad, aliongeza kwamba Mwezi Septemba walipatiwa Shilingi Bilioni 5 na baadaye Oktoba wakapatiwa Shilingi Bilioni 4, ambapo wataalamu walianza ukaguzi kwenye halmashauri mbalimbali mwezi Novemba 2016. CAG ameweka bayana kuwa mpaka Februari mwaka huu baadhi yao walikuwa hawajamaliza kazi hiyo, hali ambayo ni tofauti na kawaida, ambapo Desemba hutakiwa wote wawe wamerejea kutoka kwenye maeneo ya ukaguzi, ili waandae taarifa ambayo huwasilishwa kwenye Bunge la Bajeti.

Prof Assad amesema kuwa mikoa na halmashauri zinazokaguliwa na CAG zimekuwa zikiongezeka; kutoka mikoa 25 hadi 26 na halmashauri 170 hadi 173. Pia bajeti inayowasilishwa na ofisi ya CAG Bungeni imekuwa ikiongezeka lakini kiasi ambacho amekuwa akipitishiwa na kupewa kimekuwa kikishuka kila mwaka.

Prof Assad ameweka bayana kuwa miaka mitatu iliyopita, ofisi yake ilianzisha utaratibu wa kuwaongezea ujuzi wataalamu wake ili waendane na matakwa ya kimataifa, lakini sasa utaratibu huo umekwama kwa ukosefu wa fedha.

“Tumeomba msaada kwa baadhi ya nchi, ikiwemo China, zimekubali kutusaidia kusomesha wataalamu wetu kwa awamu, angalau watano watano lakini ikumbukwe hata kusafirisha mtu mpaka China na kuishi huko kuna gharama, bado serikali imeshindwa kumudu gharama hizo,” alieleza Prof. Assad

Alibainisha kuwa hata watumishi 129 walioajiriwa na ofisi hiyo, hawajapatiwa mafunzo elekezi, hali inayosababisha kufanya kazi bila ufahamu wa hakika wa taratibu za kazi zao.

Miradi ya gesi na mafuta inayoendelea kutekelezwa nchini, pia haiwezi kunufaisha taifa kwa kiwango cha kutosha kutokana na taifa kutokuwa na wataalamu waliobobea katika ukaguzi wa rasilimali hizo.

Prof Assad pia ameiomba Hazina ipeleke fedha kwa wazabuni wanaoidai serikali. Bila kutaja majina ya wazabuni wala kiasi wanachodai, Prof. Assad alisema, “Naomba Hazina mpeleke fedha zinazotakiwa kupelekwa ofisini kwetu, hawa watu walipwe na sitegemei baada ya kutoa kauli hii, nipigiwe simu au nifuatwe tena na wazabuni hawa.”

Kwa mujibu wa maelezo ya Prof. Assad, mmoja kati ya wadai amesema akilipwa ndani ya mwezi huu (Machi) atapokea kiasi anachodai lakini zaidi ya muda huo, ataanza kutoza riba ya asilimia 15 ya deni hilo kwa kila mwezi.

Alisema wameshaandika barua tatu Hazina, kuhusu madai hayo bila kujibiwa; huku fedha zilizoidhinishwa na Bunge mwaka jana kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya ofisi hiyo, Sh. Bilioni 8, haijapekwa hata Shilingi moja.
 
Hawa si ndio huwa wanapewa rushwa na halmashauri kuzipa hati safi kutokana na ubadhirifu sasa kuna haja gani ya kupoteza pesa kwenye taasisi kama hiyo..siku hizi CAG ni watu wa usalama wa taifa.. Nilichogundua ukiwa na utawala bora hutaitaji hiyo taasisi.
 
Prof Assad amesema kuwa mikoa na halmashauri zinazokaguliwa na CAG zimekuwa zikiongezeka; kutoka mikoa 25 hadi 26 na halmashauri 170 hadi 173. Pia bajeti inayowasilishwa na ofisi ya CAG Bungeni imekuwa ikiongezeka lakini kiasi ambacho amekuwa akipitishiwa na kupewa kimekuwa kikishuka kila mwaka.

Prof Assad ameweka bayana kuwa miaka mitatu iliyopita, ofisi yake ilianzisha utaratibu wa kuwaongezea ujuzi wataalamu wake ili waendane na matakwa ya kimataifa, lakini sasa utaratibu huo umekwama kwa ukosefu wa fedha.

“Tumeomba msaada kwa baadhi ya nchi, ikiwemo China, zimekubali kutusaidia kusomesha wataalamu wetu kwa awamu, angalau watano watano lakini ikumbukwe hata kusafirisha mtu mpaka China na kuishi huko kuna gharama, bado serikali imeshindwa kumudu gharama hizo,” alieleza Prof. Assad

Alibainisha kuwa hata watumishi 129 walioajiriwa na ofisi hiyo, hawajapatiwa mafunzo elekezi, hali inayosababisha kufanya kazi bila ufahamu wa hakika wa taratibu za kazi zao.

Miradi ya gesi na mafuta inayoendelea kutekelezwa nchini, pia haiwezi kunufaisha taifa kwa kiwango cha kutosha kutokana na taifa kutokuwa na wataalamu waliobobea katika ukaguzi wa rasilimali hizo.

Prof Assad pia ameiomba Hazina ipeleke fedha kwa wazabuni wanaoidai serikali. Bila kutaja majina ya wazabuni wala kiasi wanachodai, Prof. Assad alisema, “Naomba Hazina mpeleke fedha zinazotakiwa kupelekwa ofisini kwetu, hawa watu walipwe na sitegemei baada ya kutoa kauli hii, nipigiwe simu au nifuatwe tena na wazabuni hawa.”

Kwa mujibu wa maelezo ya Prof. Assad, mmoja kati ya wadai amesema akilipwa ndani ya mwezi huu (Machi) atapokea kiasi anachodai lakini zaidi ya muda huo, ataanza kutoza riba ya asilimia 15 ya deni hilo kwa kila mwezi.

Alisema wameshaandika barua tatu Hazina, kuhusu madai hayo bila kujibiwa; huku fedha zilizoidhinishwa na Bunge mwaka jana kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya ofisi hiyo, Sh. Bilioni 8, haijapekwa hata Shilingi moja.

[HASHTAG]#HAPAKAZITU[/HASHTAG]
 
Siku hizi hela zote ziko mfukoni kwa mtu na yeye ndio anayeamua atoe shs ngapi na ziende wapi! akiamua zote zikajenge bandari chato wanafki wanapiga makofi tu.. Tunapitia pabaya sana kama taifa! Tuendelee kucheka na nyani tu, ila tusishangae msimu wa mavuno!
 
Kabla fedha zozote za serikali zilizopitishwa na Bunge haziwezi kutumika kwanza Kabla hazijaidhinishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, na hii ndio role ya CAG kama Mdhibiti Mkuu wa Matumizi ya serikali, kudhibiti matumizi ya serikali yaliyoidhinishwa na Bunge, na kisha baada ya matumizi, CAG hurejea kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha hizo kama zilitumika kama zilivyokusudiwa na hii ndio role ya CAG kama Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Paskali una rejea ya sheria kuhusiana na chapisho lako hili? Unazungumzia CAG au Mkaguzi wa Ndani? Hebu tupia kifungu cha sheria kinachompatia mamlaka CAG kufanya authorization/veto ya matumizi ya pesa za umma kisha arudi ku-audit matumizi yake. Ki maadili na best practices mamlaka husika hayawezi ku-authorize matumizi ya pesa kisha ikaja ku-audit matumizi ya pesa hizo tena. It will be like self auditing!
 
Back
Top Bottom