Madeni ya Taifa: Kuna kitu very serious CAG amekisema. Hii kitu haiko sawa. Je, tunakwenda wapi?

Madeni ya Taifa: Kuna kitu very serious CAG amekisema. Hii kitu haiko sawa. Je, tunakwenda wapi?

Tumeula wa chuya.

Pascal alivyokuambia kwamba muhimili mwingine umechimbiwa chini zaidi hukumuelewa?
 
Mengi kama haya yapo nchi hii

na umeweza kugundua kwa sababu ya utashi wako murua

watanzania wengi wako bize na habari za umbeaumbea , ukuda ukuda, wako bize na bashite!!

mambo kama haya huwezi kut wanafuatilia na wanakuwa serious!! haipo

Hata ukifuatilia na kuwa seriuos utafanya nini kwa katiba inayompa nguvu mkuu ya kuwa juu ya sheria ama kizite
Only in TZ hivi ni njaa au waoga?

Vyote kwa pamoja, kumbuka wabunge wote wana mikopo, na rais anajua kabisa wakiacha ubunge hawana ubavu wa kulipa hiyo mikopo. Hivyo anajua hakuna yoyote yuko tayari kukosa au kuingia kwenye hilo janga la kudhalilika kwa kushindwa kulipa mkopo. Tabia hiyo wanayofanyiwa wabunge imekuwa ni fimbo ya kuwachapia walio wengi, na hali hii inawakuta mpaka vyombo vya sheria na dola. Kwa mtindo huu ndio maana unaona mkulu anaweza kuwafanya lolote na wala asiwepo wa kuhoji labda wabunge wa upinzani. Sasa hivi wakuu wa mikoa na wilaya wana nguvu kuliko wabunge na wanaweza kufanya lolote na wala bunge lisifanye lolote.
 
Tulishaomba siku nyingi juu ya ubora wa wabunge. Uganda huwezi kuwa mbunge bila academic degree, Kenya sikumbuki sana lakini hawa ndo tulionao EAC. Wao wanaweka vigezo vya juu sisi tunasema kusoma na kuandika, hata kuhesabu haimo! Watu kama hao ndo watupangie sera za nchi? Watunge sheria za nchi? Wachanganue mitego ya ulaji kama hiyo ya chai maofisini?

sasa eti wakishapitisha wewe mkuu wa nchi ufuatishe hivyo hivyo! NO!

Mkuu wakati mwingine huwa hata siwaelewi wabunge hasa wale walio wengi. Kimsingi kule bungeni ni kusema ndio au hapana basi, wala hawatungi sheria au kupanga bajeti. Kutunga sheria na kuandaa bajeti zote hizo zinafanywa na watu wengine kabisa, wao kazi yao inakuwa kama yale maswali ya kuchagua kwa kusema ndio au hapana tu. Hata hao wabunge wakipendekeza chochote kwenye hicho kilicholetwa ni nadra sana kuwekwa kwenye sheria au bajeti iliyoletwa na serekali. Hapa ndipo ulipo msingi wa dharau za kina Makonda na mkulu kwa wabunge. Kwani kusema ndio au hapana hata mtoto mdogo si anaweza kusema?
 
Siku hizi nchi hii kila kitu hakiko sawa,cheerleaders wanashangilia tu bila hata uhakika wa kesho.
 
Utawala huu hauheshimu sheria na taratibu za nchi kabisa,mtu mmoja anaamua na alipwe, nani afungwe,nani afutwe ,nani abaki hata kama ana kosa linalofanana na aliyefutwa ,mtu anaeamua juu ya bunge au mahakama, mtu anayemwona anaempinga au mpinzani ni adui.
 
Mbona hatutaki kukubari hali harisi,kanunua Bombandiar mkasema ni bajaj mnataka dream liner,akanunua ndege 6 kwa mpigo mkasema tunataka train mwendo kasi,akapiga chini mkandarasi wa kichina akaweletea mturuki mkandarasi wa shoka.
Mkalia hakuna hostel kwa chuo kikuu kikongwe lakini akauliza mbona hicho chuo kinaelekeza kwenye majengo mlimani city?Ina maana hizo sharubu za maprofesa hawajui vipaumbele?Akawajengea hostel za bilioni 10 na zimeishaisha.
Nataka kusema Raisi yupo sahihi asilimia 100 kuipanga bajeti kutegenea na vipaumbele halisi,kwani hiyo bajeti inaopitishwa iko too mechanical,hailengi hali harisi,
Hao wabunge ni kawaida kulalamikia bajeti kila wakisimama kuchangia lakini uishia kuiunga asili mia mmoja.
 
Waswahili wanasema ukikubali kuolewa usichague ukubwa wa machine,utakayoikuta ndio hiyo hiyo,kama ni ndogo sawa kama ni kubwa vumilia.Mungu ndiye atawatenganisha
 
Kajilimbikizia vyeo vingi muhimu nchini yeye ni Bunge, ni CAG, Jaji Mkuu kuingilia mahakama nchini kumbukeni issue ya Lema, Lissu, lijualikali, viongozi wa CUF waliofungwa kule Lindi. Huyu ni mtu hatari sana lazima Watanzania tuwe kitu kimoja kumkabili huyu bila kujali itikadi zetu vinginevyo tutakuja juta sana jinsi atakavyoivuruga nchi yetu na nchi ikishavurugwa huchukua miaka mingi sana kurudi pale pazuri ilipo na wakati mwingine inaweza kabisa kutorudi pale ambapo wananchi wengi walipapenda. Tusikae kimya huku nchi yetu ikiendelea kuvurugwa na huyu mtu.

Kazi za CAG zinafanywa na Raisi.
 
...Tujadili mada ya Pasco and not kumjadili Pasco; honestly ameleta quite convincing argument hapa jukwaani. Kama na sisi hatuoni bunge likipokwa madaraka yake wazi wazi; tukanyamaza kimya; then mwaka 2020 twapanga foleni kuchangua wabunge wengine, wakati tunajua hilo bunge halina kazi hii ni shida kubwa.

Mkuu
Huyu mleta mada sisi tulikuwa tunamuambia kila siku hapa kama TZ sasa imeingia ktk serikali isiyo fuata utawala bora lkn yy akawa anatudharau sana!
Umewahi ona wapi Rais anatumia mabilion kununua ndege bila kupitisha bajeti Bungeni ila yy ana muita tu Gavana wa BOT anachukua mapesa?
Uliona wapi mteule wa Rais analitukana Bunge kama wanalala tu Bungeni tena kwenye media wazi wazi kabisa na hadi sasa yupo madarakani?
Uliona wapi Rais analitishia Bunge na hao wabunge wanaufyata?
Hoja nzuri lkn imeletwa na mramba miguu ya watawala,kaanza kusema sababu anaona muda unapita hapewi u DC!
Pia kumbuka kuwa Mayala ina maana ya njaa!!
 
Muda NDIYO jibu sahihi Kwa haya tunayaoona na bado tutayaona na kuyasikia mengi mbeleni.

Hakuna kitu kibaya Kama kucheza na akili za watu tena kizazi Hiki cha Mwinyi na Mkapa ni hatari sana.

Mbeleni naamini magari ya serikali yatapaki kabisa kukosa mafuta, watumishi wa serikali watakuwa na maisha magumu mara dufu na kazi za serikali zitapigwa sindano ya ganzi.

Ukweli usiopingika morali ya wafanyakazi wa serikalini imeshuka sana, watu hawana Raha na kazi hata kidogo. Halmashauri mambo hayaendi, wizarani ndio usiseme, ofisi za MaRC na MaDC ndio hoi bini taaabani.

Yetu macho muda ndio msemakweli Tuombe uzima!
 
Mkuu ni bora kukaa kimya tu,acha kupotosha!rudi kasome tena katiba pamoja na sheria ya ukaguzi wa umma na kanuni zake,acha maneno maneno
Kipindi hichi cha Mfalme bora nyie mauditor mkae kimya tuu maana hivyo viaudit query vyenu vitakanyagiwa mpaka muisome namba. Huyo boss wenu alkaida atatolewa puta aende akapumzike na hao wake zake wanne
 
Raisi hana mamlaka ya kumg'oa CAG madarakani labda astaafu, afe, awe kichaa au ikibainika mbele jopo la majaji wa jumuiya ya madola kuwa amefanya kinyume na matakwa ya kazi yakee ndio CAG anaweza kung'oka
Subiri muone Mtakatifu atakavyo mtimua huyo jamaa pamoja na hilo jopo la majaji
 
Umeangalia kiwango cha deni la Taifa ukilinganisha deni lililokuwepo na hili la sasa? Shule yako ya jirani watoto wangapi bado wanakaa chini? Ndege si tunazo sasa, je, umegundua nauli ya kukupeleka KIA na kurudi kwa fastjet sasa hivi siyo 1Mil? Nahisi hata mkopo wa bandari mpya ya Bagamoyo umezimwa kinyume na ilivyopitishwa na Bunge. Logical!

Duh!
Za kuambiwa changanya na za kwako!
1. deni walikopa UPDP ? kwanini hatamti kufanya vulue for mopney tujue deni lilitumika wapi na watu wawajibishwe? au ndio wenzenu?

2. kuhsu shule nadhani ujitambui aliyekuambia elimu ni madawati nani kama thamani ya elimu haipo mtu unaweza kuunga unga na ukatusua kama bashite ? kwanini utuambia kuhus mikopo elimu ya juu(hivi muaahidi nini vile?)

3. Ndege inanihusu nini mkazi w akolomije? inaweza kunisaidia kusindika nyanya znagu? je inawezxa kunisaidia kupunguza bei ya sukari? bei ya mahindi, je wajua bei ya mchele ni sawa na unga kwa sasa?

4. hayo ya bagamoyo yamefanya na ACT au? kwanini hamuwajibishi waliofanya hayo?
 
Back
Top Bottom