Madeni ya TALA na Branch

Madeni ya TALA na Branch

Hiii mikopo yao inakatiwa bima kabisa ukishindwa kulipa wanaliowa na bima. Ila mawakala wanao wakikuotea ndo hivyo tena. Ila wana kuripoti kwenye taa sisi zote zinazo husiana na mambo ya fedha, kwamba wewe ni mdaiwa sugu kwahiyo huta weza kukopa popote tena.
LIPA MADENI NDUGU HUO SIYO UJANJA.UNAJUA MAANA YA ALAMA HII!?[emoji117] [emoji614]

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh wananiripoti kwa identity ipi?je nikibadil identity huko wanakoniripot watanijuaje kam mdaiwa sugu? Siijui hio alama nifahamishe mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hofu yangu ni kwamba wanaweza wakaaa wapo kimya lakini wanakupigia hesabu zile interest za mkopo wako wa kila mwezi siku wakikukomalia baada ya kulipa 10000 ukajikuta unalipa zaidi ya hiyo. Na pia sawa wanaweza wasikufunge lakini utapoteza muda wako na mambo ya kesi mahakamani endapo wakachukuwa sheria kikamilifu. Lipa tu mkuu ni haki yao hiyo

.
 
Kiufupi unajiwekea limit, hutakopesheka daima. Kulipa mhimu. Pia ipo siku watakuanika mitandaoni kama mdaiwa sugu. Ni aibu kutorudisha vipesa vidogo dogo ambavyo ukiwa mwaminifu vinasaidia sana kwenye dharula ndogo ndogo ambapo ukimuazima mtu yeyote ni ngumu kukupa. Kwaivo usifurahie kutodaiwa au kufanywa chochote... Ipo siku, maisha ni safari. Nilichelewesha mpawa mkopo wao... Nikaja nikalipa deni Badae... Ona sikopesheki tena ilihali zamani nikiwa na shida nakopa faster. Nimebaki na Tala tu, sifanyi makosa tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tala walikua wananipiia simu kila mara kwa namba ya kenya nikawa sipokei badae wakabadili namba ya kibongo nikastuka, sababu line niliyokopea ni mpya nikaapa sipokei simu kutoka kwenye hiyo namba. Sasa ni mwendo wa sms za mikwara,,, jamaa wana mikwara haijawahi tokea aisee ila nawakomesha sababu mwanzo nilikopa wakati wa kurudisha nikazidisha elf 5 makusudi wakaniambia next mkopo wataijazia ila hawakufanya hivyo so kama walivyoniibia nao wapambane na hali yao.
Ila si ingekuwa poah uwalipe ili next time ukishidika ukope? Kwanini unawakomesha? Vipi ungekuwa wewe ndo unadai? Anyway jamaa wanatusaidia sana wenye shida zetu za dharula, hatuwasumbui tena ndg na jamaa zetu eti nikope 20,000 [emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo lugha za wadaiji wala sio waliokukopesha... Pia ni hata bank wanapodai watakukomalia na maneno ivyoivyo.. Dawa ni kulipa wandugu ili huduma ziendelee
HAKUNA KUKAMATANA WALA NINI WATU WAMEJIANDIKISHIA TANDAHIMBA WANAKOPEA DAR

WANAKUPATIA WAPI WANGEKUA NA UWEZO WA KUKUKAMATA WASINGEKUTISHA NA TEXTS ZAO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu watawezaje kuthibitisha kwamba wananidai 1.5T ilihali wananidai 20K?
Alafu kesi ya madai sio kesi ngumu maana mchakato wake una mambo mengi ambayo anayekudai anaweza kughaili.

Hivi unanidai 20K hukumu ikasema niende jela miezi sita na kisha nilipe pesa yako, je uko tayari kunihudumia chakula kwa miezi sita nikiwa jela ili nikitoka nikulipe 20K?



Sent using Jamii Forums mobile app
Umeona wapi sheria hiyo... Jaribu siku mkope au mdhulumu mtu akufungulie kesi ya madai uone, labda awe hana ufahamu.. Sijui nawewe utapenda kukaa ndani miezi 6 kisa 20,000!!! Yeye anaweza kusucrifice hiyo wewe uteseke tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi hawa hizi namba zao wanazotuma sms haiwezekani kuziblock tu wasitupate yani unikopeshe upo huko kenya afu uanze kunisumbua na vitisho mimi alaaaaaa
Mifumo ya pesa ndg hujaelewa.. Kopa ingia mitini ukidhani Namanyele na Nairobi ni mbali.. La unaishi nje ya dunia sayari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi branch huwa wananipush sana nkiwa na emegence za hapa na pale mpk nw ninauwezo wa kukopa hadi kilo 4,ofcoz huwa nawalipa kwa wakati maana sioni sababu ya kuwadhurumu kwa kutokuwalipa ilihali fedha zao huwa nikiomba tu dk haiishi mzgo unaingia so sionagi inshu ya kutowalipa na ukizingatia kwa mfano laki 3 ukikopa unawalipa kwa miez mitatu kdg kdg,kwa maisha yalivyo taiti kibongo bongo utamkopa nani hela yafasta fasta afu uje umlipe kdg kdgo???

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ndo spirit nzuri ya mkopaji.. Malengo hayaishi siku moja... Pia mikopo easy ni michache sana...hata ndg tu mwambie akupe laki uone? Au nenda kwa wakopesha kwa riba uone shughuli yake, utahama makazi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Check app ya tala, Download, jisajili, maelezo utapata humo.. Ila uhalisi wako watauhitaji kupitia id yako na FB, so kama fb hauna taarifa za kuwasaidia wakujue sio rahisi kupata mkopo... Wengine wanatumia majina ya kizushi, wengine wanapost ujinga jinga tu... So watakujudge kihivyo... Mimi saivi niluanzaga na 10,000 nalipa kwa uaminifu niko mpaka 180,000 ...
Nahitaji kujua zaidi kuhusu TALA, wako wapi? Naomba nifahamu jinsi ya kuwafuatilia, je wana ofisi au ni katika mitandao? masharti ya kukopa ni yapi? asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom