Madereva 9 Wakenya waliotokea Tanzania wagunduliwa kuwa na Corona. Visa vyafikia 700

Madereva 9 Wakenya waliotokea Tanzania wagunduliwa kuwa na Corona. Visa vyafikia 700

Kama hamtaki korona mnaingia kufata nini huku?

Huko kwenu si kuna lokidauni Sasa mbona raia zenu zinatapatapa huku?

Mi naona kuna namna mnaitumia kuipiga tz maana nikiangalia na mkulu wetu kukaidi hivyo vikao ni kama kuna kitu kinaendelea na inatafutwa namna ya kuichapa tz kiuchumi na kitalii si bure maana hizo takwimu zenu na huku mtaani ni vitu viwili tofauti kabisa!

Nahisi kuna kitu kinaendelea baina ya serikali yetu na ukanda tuliopo kuna kitu si cha kawaida.
Umeongea vyema sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hii kitu inahitaji a coordinated regional effort yaani kwa mfano Uganda ametoa kafara uchumi na kupiga lockdown halafu huku Tanzania tunadunda na kupiga kazi mwisho wa siku tunategemeana lazima corona itatoka Tanzania kuelekea Uganda, kazi mnayo maana ni mkaidi na hamna mwenye uwezo wa kumbadili mawazo akishaamua hata wafe 50% ya population kazi zitapigwa na hiyo 50% iliyobaki.
 
Dah! Sasa mnafanya huku kwetu Tz ionekane Corona ni kama kahawa tu [emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
Corona kila sehemu. Yani ukivuka boder ukavuta hewa ya TZ ukirudi kwenu tayari umeshaukwaa. Mamlaka za ndani ya nchi zichukue hatua mapema kabla hali haijazidi kuwa mbaya.
 
Binafsi mimi sina mtu nayemjua ambaye amekufa au ana covid19 ambaye naweza nikamtolea ushahidi kwa uhakika kabisa ila nabaki kusikia tu huku na kule.

Kama una ndugu, jamaa au rafiki aliyekufa au ana covid19 ambaye ni mtu wako wa karibu naomba nikupe pole. Ila kama na wewe katika watu ambao wamekuzunguka huna mtu wa karibu ambaye unamjua kwa 100% kua ana covid19 fikiria mara mbili mbili.
 
Mkuu wetu alituambia corona tutaendelea kuishi nayo kama tunavyoishi na TB, ukimwi n.K
So eti tusiogope corona
 
Tatizo hii kitu inahitaji a coordinated regional effort yaani kwa mfano Uganda ametoa kafara uchumi na kupiga lockdown halafu huku Tanzania tunadunda na kupiga kazi mwisho wa siku tunategemeana lazima corona itatoka Tanzania kuelekea Uganda, kazi mnayo maana ni mkaidi na hamna mwenye uwezo wa kumbadili mawazo akishaamua hata wafe 50% ya population kazi zitapigwa na hiyo 50% iliyobaki.

Nimecheka sana ila duh!

Yaani huu ndio ukweli wenyewe, kuna aina ya viongozi akiamini la kwake yaani hata upige bomu mlangoni habadili ktu.
Ndicho kiliiponza Ujerumani kwenye vita vya pili vya dunia, yaani Hitler aliambiwa kitambo kwamba Ujerumani inaelekea kupoteza vita, jamaa akawa anatokwa mipovu na kuamuru vita viendelee, akaambiwa mabomu sasa yameanza kutua hadi Ujerumani lakini wapi, yaani jamaa alikaidi na alivyo mbishi hakukubali akamatwe hai, kajipiga risasi kichwani.
 
Hatuja waleta kwetu. Walifata nini huku kwenye corona yetu? Mipaka yao imefungwa, wao waliingiaje Tz na mpaka wao umefungwa? Kenya mnataka kuufadhaisha ulimwengu kuwa, sisi hatujafunga mpaka ndo maana corona inaongezeka. Hizo mbinu za kitoto sana. Kama kutangaza kufunga mipaka ni dawa, corona inafikaje kwenyu?
 
Taarifa yako haijataja madereva wabongo sita waliopatitaka na korona
korona.jpeg
wakakatazwa kuvuka
 
Kuna kitu kidogo kinatuponza "ukaidi"

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi tahadhari wanazochukua wenzetu na sisi tofauti ipo wapi au sisi tatizo kubwa ni kutangaza takwimu hili sawa kabisa halina ubishi.

Hebu kwanza tuangalieni hili hapa kwa mjadala mrefu zaidi kuna sehemu ambayo hatujatofautiana sana na wao.
 
Kwa hiyo katika Corona kuna mkono wa Mungu?

Ishu kubwa ni kusema kwamba kuna kitu nyuma ya hili,hiko kitu pia tujiulize ni kitu gani,ni kitu mtu, ni kitu Mungu,ni kitu shetani, ni kitu silaha, ni kitu janga, ni kitu kutoka mbinguni, ni kitu kutoka maabara,ni kitu kutoka wapi, ni kitu kama adhabu, ni kitu kama gharika, ni kitu kama mkono wa shetani, kuna kitu nyuma ya hili gonjwa, nyuma hiyo ni ipi, ni siri, ni dhahiri, au nini? Ndio maana ya kujihoji kwanza kuna nini nyuma ya hili kuna kitu gani.

Kama ni ugonjwa umeanzia wapi, kwa wanyama au kwa binadamu, kama ni wanyama kwanini leo na siyo mwaka 1978, nyuma ya hii ni nini, kuna nini kilichofichwa, kimefichwa kwanini, na nani, lini ili iweje.

Tutafute pa kuanzia kwanza kabla ya kutafuta tuliopo.
You're smart

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! Sasa mnafanya huku kwetu Tz ionekane Corona ni kama kahawa tu [emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
Lengo lenu wakenya tunalijua mnadhani mkisema hivyo itaonyesha watz wote tuna corona ,sawa kama ni kweli mbona sasa ni miezi miwili inaenda kama waelfu tunaugua tunge jaa malaki hospitalini au sivyo basi huu ugonjwa unapenda damu zetu maana tunaishinao bila kuugua wa kufa kwa maelfu.

Send by APOLO 1
 
Kama hamtaki korona mnaingia kufata nini huku?

Huko kwenu si kuna lokidauni Sasa mbona raia zenu zinatapatapa huku?

Mi naona kuna namna mnaitumia kuipiga tz maana nikiangalia na mkulu wetu kukaidi hivyo vikao ni kama kuna kitu kinaendelea na inatafutwa namna ya kuichapa tz kiuchumi na kitalii si bure maana hizo takwimu zenu na huku mtaani ni vitu viwili tofauti kabisa!

Nahisi kuna kitu kinaendelea baina ya serikali yetu na ukanda tuliopo kuna kitu si cha kawaida.
Serikali ya Kenya inafanya chokochoko kama za idi amini.

Send by APOLO 1
 
Back
Top Bottom