Sasa kama mfumo rasmi bado kwanini poliCCM wanawakata pointi? Huoni kuwa huo ni unyanyasaji?Elimu ya kutosha alafu wanasema kwenda mwanza mara moja point zote zinaisha ?
Point zipi wanazodai warudishiwe wizara imesema mfumo rasmi bado
Maelezo ya polisi na wizara ni kwamba mfumo ulikua kwenye majaribioSasa kama mfumo rasmi bado kwanini poliCCM wanawakata pointi? Huoni kuwa huo ni unyanyasaji?
Si nasikia wamichezo analuka naye kitambo tuBado yupo eda mkuu. Zimebaki siku chache tu jimbo liwe wazi.
😆Bi mwenda bado yupo eda
Ni uwongo. Tayari madereva wengi wamekatwa pointi na wamelazimishwa kurudi kusoma. Huu ni uhuni.
Ngoja wakusikie akina Mwashambwa!Licha ya Waziri wa Michezo (Bwana Paulo Makonda) na Waziri wa Mambo ya Ndani (Bwana Patrobas Katambi) kufanya kikaokazi na madereva wa mabasi yaendayo mikoani jana tarehe 29/09/2026, madereva hao wameshikilia msimamo wao wa kutoingia barabarani hadi warejeshewe pointi zao walizokatwa kihuni. Aidha, wanawataka polisi kuacha kuwalazimisha kurudi kusoma ilhali tayari wanayo elimu ya kutosha.
Pamoja na mambo mengine, madereva hao wamechoshwa na vitendo vya polisi kuwadai rushwa, kuwapiga tochi ovyo na kuwaonea bila sababu za msingi. Pia wanadai serikali iwasaidie kusimamia mikataba kati yao na waajiri wao, ambao wamekuwa wakiwanyonya kwa muda mrefu bila kupatiwa msaada wowote kutoka serikalini. Kuonesha kwamba msimamo wao ni thabiti na hawawezi kurudi nyuma kamwe, dereva mmoja anayesafirisha abiria kati ya Dar es Salaam na Mwanza amesikika akisema: "Hatuingii barabarani hadi turejeshewe pointi zetu na madai yetu yote yapate ufumbuzi. Pia polisi waache kutupiga tochi na kutunyanyasa tukiwa safarini", alisema.
Naye Waziri Katambi amesema kuwa mfumo wa kukata pointi wameuiga kutoka nchini Rwanda na kusisitiza kwamba Tanzania haiwezi kubaki kama kisiwa wakati nchi nyingine zinaendesha mambo yao kisasa.
MAONI YANGU
Ijapokuwa mgomo unawakwamisha abiria wasiokuwa na hatia, nawaunga mkono madereva 💯% katika mgomo huu. Haki siku zote hudaiwa kwa nguvu na kwa gharama, hata ikibidi kumwaga damu au kutoa kafara. Serikali hii haramu ya CCM sio sikivu hata kidogo.
Nitawashangaa sana madereva ikiwa hatimaye watashawishiwa kuingia barabarani kabla madai yao yote hayajapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Serikali ya CCM ni walaghai sana. Wanawalaghai madereva waingie barabarani halafu wayapotezee madai yao. Msikubali kamwe ndugu madereva. Shikilia hapo hapo mpaka kieleweke. Kama nitaitwa mhaini kwa kuwaunga mkono madereva, ngoja tu niwe mhaini na nitakinukisha kweli kweli.
Nawasilisha.
Joyce Wowowo anahusikaje hapo?Waziri wa Michezo (Bwana Paulo Makonda)
Hii kurudi tena kusoma ilibidi iwe kwa wote madaktari,wauguzi,HR,wafamasia yaani kila sekta haiwezekani sisi madereva .Licha ya Waziri wa Michezo (Bwana Paulo Makonda) na Waziri wa Mambo ya Ndani (Bwana Patrobas Katambi) kufanya kikaokazi na madereva wa mabasi yaendayo mikoani jana tarehe 29/09/2026, madereva hao wameshikilia msimamo wao wa kutoingia barabarani hadi warejeshewe pointi zao walizokatwa kihuni. Aidha, wanawataka polisi kuacha kuwalazimisha kurudi kusoma ilhali tayari wanayo elimu ya kutosha.
Pamoja na mambo mengine, madereva hao wamechoshwa na vitendo vya polisi kuwadai rushwa, kuwapiga tochi ovyo na kuwaonea bila sababu za msingi. Pia wanadai serikali iwasaidie kusimamia mikataba kati yao na waajiri wao, ambao wamekuwa wakiwanyonya kwa muda mrefu bila kupatiwa msaada wowote kutoka serikalini. Kuonesha kwamba msimamo wao ni thabiti na hawawezi kurudi nyuma kamwe, dereva mmoja anayesafirisha abiria kati ya Dar es Salaam na Mwanza amesikika akisema: "Hatuingii barabarani hadi turejeshewe pointi zetu na madai yetu yote yapate ufumbuzi. Pia polisi waache kutupiga tochi na kutunyanyasa tukiwa safarini", alisema.
Naye Waziri Katambi amesema kuwa mfumo wa kukata pointi wameuiga kutoka nchini Rwanda na kusisitiza kwamba Tanzania haiwezi kubaki kama kisiwa wakati nchi nyingine zinaendesha mambo yao kisasa.
MAONI YANGU
Ijapokuwa mgomo unawakwamisha abiria wasiokuwa na hatia, nawaunga mkono madereva 💯% katika mgomo huu. Haki siku zote hudaiwa kwa nguvu na kwa gharama, hata ikibidi kumwaga damu au kutoa kafara. Serikali hii haramu ya CCM sio sikivu hata kidogo.
Nitawashangaa sana madereva ikiwa hatimaye watashawishiwa kuingia barabarani kabla madai yao yote hayajapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Serikali ya CCM ni walaghai sana. Wanawalaghai madereva waingie barabarani halafu wayapotezee madai yao. Msikubali kamwe ndugu madereva. Shikilia hapo hapo mpaka kieleweke. Kama nitaitwa mhaini kwa kuwaunga mkono madereva, ngoja tu niwe mhaini na nitakinukisha kweli kweli.
Nawasilisha.
Kwa hiyo pointi walizokatwa watarejeshewa baada ya majaribio kukamilika?Maelezo ya polisi na wizara ni kwamba mfumo ulikua kwenye majaribio
Waziri ametaka apewe taarifa wote waliokatwa point,Kwa hiyo pointi walizokatwa watarejeshewa baada ya majaribio kukamilika?