Nami nna swali kama hili hili.Waziri wa michezo hili sakata linamhusishaje au ndio kutaka kick
Nami nna swali kama hili hili.Waziri wa michezo hili sakata linamhusishaje au ndio kutaka kick
nadhani busara utumike tu,Licha ya Waziri wa Michezo (Bwana Paulo Makonda) na Waziri wa Mambo ya Ndani (Bwana Patrobas Katambi) kufanya kikaokazi na madereva wa mabasi yaendayo mikoani jana tarehe 29/09/2026, madereva hao wameshikilia msimamo wao wa kutoingia barabarani hadi warejeshewe pointi zao walizokatwa kihuni. Aidha, wanawataka polisi kuacha kuwalazimisha kurudi kusoma ilhali tayari wanayo elimu ya kutosha.
Pamoja na mambo mengine, madereva hao wamechoshwa na vitendo vya polisi kuwadai rushwa, kuwapiga tochi ovyo na kuwaonea bila sababu za msingi. Pia wanadai serikali iwasaidie kusimamia mikataba kati yao na waajiri wao, ambao wamekuwa wakiwanyonya kwa muda mrefu bila kupatiwa msaada wowote kutoka serikalini. Kuonesha kwamba msimamo wao ni thabiti na hawawezi kurudi nyuma kamwe, dereva mmoja anayesafirisha abiria kati ya Dar es Salaam na Mwanza amesikika akisema: "Hatuingii barabarani hadi turejeshewe pointi zetu na madai yetu yote yapate ufumbuzi. Pia polisi waache kutupiga tochi na kutunyanyasa tukiwa safarini", alisema.
Naye Waziri Katambi amesema kuwa mfumo wa kukata pointi wameuiga kutoka nchini Rwanda na kusisitiza kwamba Tanzania haiwezi kubaki kama kisiwa wakati nchi nyingine zinaendesha mambo yao kisasa.
MAONI YANGU
Ijapokuwa mgomo unawakwamisha abiria wasiokuwa na hatia, nawaunga mkono madereva 💯% katika mgomo huu. Haki siku zote hudaiwa kwa nguvu na kwa gharama, hata ikibidi kumwaga damu au kutoa kafara. Serikali hii haramu ya CCM sio sikivu hata kidogo.
Nitawashangaa sana madereva ikiwa hatimaye watashawishiwa kuingia barabarani kabla madai yao yote hayajapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Serikali ya CCM ni walaghai sana. Wanawalaghai madereva waingie barabarani halafu wayapotezee madai yao. Msikubali kamwe ndugu madereva. Shikilia hapo hapo mpaka kieleweke. Kama nitaitwa mhaini kwa kuwaunga mkono madereva, ngoja tu niwe mhaini na nitakinukisha kweli kweli.
Nawasilisha.
Mimi nalitaka hilo jimbo. Lazima nirushe ndoanoBado yupo eda mkuu. Zimebaki siku chache tu jimbo liwe wazi.
Wanajaribu huku watu wanaumiaMaelezo ya polisi na wizara ni kwamba mfumo ulikua kwenye majaribio
View: https://www.instagram.com/reel/Dd3vphWMP2u/?stkn=OWt0dnZvdXVmMmJ4
Emu sikiliza hii exchange ya dereva na polisi.
Alafu tukubaliane kwanza kama kweli hakuna ubitaji wa dereva kurudi shuleni,
Pili . Kauli ya waziri kasema jana mfumo huo unasimama, mpaka sasa madereva wanagomea jambo gani?
Bado pesa/rushwa ndiyo itaamua ukataji wa points kwa hiyo hakuna cha maana.Hii Sheria ya kukata point ni nzuri sana iwapo itahusisha makosa ya kizembe tu yanayo fanywa na madreva barabarani.
Madreva wanekuwa sababu ya ajali Kwa sababu ya uzembe wa kipumbavu.
Elimu ya kutosha alafu wanasema kwenda mwanza mara moja point zote zinaisha ?
Point zipi wanazodai warudishiwe wizara imesema mfumo rasmi bado
Hao watu sio wajinga jaribu kuvaa matatizo yao ili uone wanachozungumza na kukihitaji watu wazima hawawezi kuacha hela kama mambo yapo sawa mkuu ukiona kuna hizi mambo jua kuna vitu havipo sawa inatakiwa visawazishwe..Elimu ya kutosha alafu wanasema kwenda mwanza mara moja point zote zinaisha ?
Point zipi wanazodai warudishiwe wizara imesema mfumo rasmi bado
Lucas Mwashambwa Tlaatlaah ChoiceVariable MamaSamia2025 KERATO MOMBAA na wapuuzi wengine kutoka Lumumba wanafikiri kwa kutumia matakwo. Hawana jipya ktk dunia hii.N
Ngoja wakusikie akina Mwashambwa!
Nashauri serikali sikivu ya CCM,Lucas Mwashambwa Tlaatlaah ChoiceVariable MamaSamia2025 KERATO MOMBAA na wapuuzi wengine kutoka Lumumba wanafikiri kwa kutumia matakwo. Hawana jipya ktk dunia hii.
Anapenda MAKIKI kama MSANII.Jana amewakusanya madereva akawa anaongea nao. Atakuwa waziri asiyekuwa na wizara maalumu.