Madereva: Hatuingii barabarani hadi turudishiwe pointi zetu

Madereva: Hatuingii barabarani hadi turudishiwe pointi zetu

Licha ya Waziri wa Michezo (Bwana Paulo Makonda) na Waziri wa Mambo ya Ndani (Bwana Patrobas Katambi) kufanya kikaokazi na madereva wa mabasi yaendayo mikoani jana tarehe 29/09/2026, madereva hao wameshikilia msimamo wao wa kutoingia barabarani hadi warejeshewe pointi zao walizokatwa kihuni. Aidha, wanawataka polisi kuacha kuwalazimisha kurudi kusoma ilhali tayari wanayo elimu ya kutosha.

Pamoja na mambo mengine, madereva hao wamechoshwa na vitendo vya polisi kuwadai rushwa, kuwapiga tochi ovyo na kuwaonea bila sababu za msingi. Pia wanadai serikali iwasaidie kusimamia mikataba kati yao na waajiri wao, ambao wamekuwa wakiwanyonya kwa muda mrefu bila kupatiwa msaada wowote kutoka serikalini. Kuonesha kwamba msimamo wao ni thabiti na hawawezi kurudi nyuma kamwe, dereva mmoja anayesafirisha abiria kati ya Dar es Salaam na Mwanza amesikika akisema: "Hatuingii barabarani hadi turejeshewe pointi zetu na madai yetu yote yapate ufumbuzi. Pia polisi waache kutupiga tochi na kutunyanyasa tukiwa safarini", alisema.

Naye Waziri Katambi amesema kuwa mfumo wa kukata pointi wameuiga kutoka nchini Rwanda na kusisitiza kwamba Tanzania haiwezi kubaki kama kisiwa wakati nchi nyingine zinaendesha mambo yao kisasa.

MAONI YANGU
Ijapokuwa mgomo unawakwamisha abiria wasiokuwa na hatia, nawaunga mkono madereva 💯% katika mgomo huu. Haki siku zote hudaiwa kwa nguvu na kwa gharama, hata ikibidi kumwaga damu au kutoa kafara. Serikali hii haramu ya CCM sio sikivu hata kidogo.

Nitawashangaa sana madereva ikiwa hatimaye watashawishiwa kuingia barabarani kabla madai yao yote hayajapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Serikali ya CCM ni walaghai sana. Wanawalaghai madereva waingie barabarani halafu wayapotezee madai yao. Msikubali kamwe ndugu madereva. Shikilia hapo hapo mpaka kieleweke. Kama nitaitwa mhaini kwa kuwaunga mkono madereva, ngoja tu niwe mhaini na nitakinukisha kweli kweli.

Nawasilisha.
​
Sio hawa tu, hata Waalimu,Madaktari na watu wa kada zingine wanapaswa kuwa na msimamo katika field zao Sheikh...bila hivyo wataendelea kunyanyaswa tu siku zote
 
Hiyo style ndio iliyomtajirisha, tangu kipindi cha Magufuli.
Ndipo alipopata UBILIONEA ,kinachosikitisha bado tu haridhiki ,anaendelea na UPIGAJI, ila Mwamba alikuwa GSM kidogo ampasue MAKALIO alivyotaka kumtapeli NYUMBA Ursino Regent Estate.
 
Shida ya sisi wananchi tumewazoesha watawala kututawala watakavyo ndio maana tumefika hapa. Siasa chafu imechukua nafasi kila kona ya nchi na sisi wananchi tupo kimya kwa uzezeta wetu. Ndio maana tumefika hapa tulipo. Serikali kila siku inabuni utitiri wa vitasisi, tozo, na sheria ili kupata fedha toka kwa mwananchi kwa njia yeyote haswa rushwa. Madereva wamevumilia hatimaye wamewasha moto. Sasa huu moto unatakiwa kila kona ili tuirudishe nchi kwenye mstari ulionyoka kwa maslahi mapana ya taifa letu. ndio maana tunaona wakina Chacha wakiongea kwa kujivuna kuwa vyombo vya dora ni vya CCM.
 
Na kitu kizuri kwao ni kwamba kila mwaka wanaendelea kutengeneza mamilioni ya mazezeta kupitia mfumo mbovu wa elimu.
 
Back
Top Bottom