Mehek
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 7,473
- 10,426
Asilimia kubwa ya daladala za dar makondakta huwa wanakataa kubeba wanafunzi zaidi ya watano.. Akishabeba wawili watatu hataki tena kubeba wengine na nafasi ipo anachukua watu wazima eti kisa wanalipa 400/500 n.k kwa kuwa wanafunzi wanalipa 200 na wapo wengi hawawataki, sasa niwaulize wewe ukikataa kumchukua na mwingine naye akamkataa nani atakae wabeba?
Watafika shuleni/ majumbani mwao saa ngapi??? Na ni watoto bado wadogo kwasababu ni under 18 most of them.
Imagine unakuta mtoto anasoma mnazi mmoja alafu anakaa kinyerezi moja na nusu saa mbili asubuhi yupo kituoni na bado anakataliwa kuingia kwenye daladala jiulize shuleni anafika muda gani?? Je ataacha kufeli?? Na muda was kurudi nyumbani ni vilevile watoto wanafika majumbani usiku jamani acheni hiyo tabia siyo nzuri.
Fikiria angekuwa ni mwanao anakataliwa ungejisikiaje!??
Lakini daladala za Dom wamenifurahisha sana yani unaingia kwenye daladala utafikiri ni school bus kumbe ni daladala na Hamna mwanafunzi anae kataliwaa....
Tuwapende watoto kwani ndiyo taifa la keshoo leo unamkataa wa mwenzio kesho wakwako
Najua makondakta humu tupo wengi nadhani ujumbe umefika!!!