Madereva wa Formula 1, ni "Marubani" wa Jet za ardhini

Aisee upo deep Sana kwenye ulimwengu wa magari hasa Kwa Sisi car enthusiast huwa tunafurahi Sana tukisoma habari za magari hasa kuhusu mambo mbalimbali ya magari..
Kama hapa Tanzania tungekuwa na kart racing games ningemlipia Mtoto wangu Kwa gharama yeyote ningeuza Hadi shamba ilimradi Mtoto wangu akasomee hiyo fani, huyu dogo anapenda magari Hadi analala nayo kitandani yeye ni MTU wa magari Tu kwenye michezo yake ya utotoni Hadi amekuwa darasa la Saba bado yupo na magari tu
 
Mku
Mkuu mkuze humo humo uyoo
 
Yeah kama alivosema kelphin ebu jaribu kuishi nae humo humo. Ata kama hatakuja kua racer but atleast afuate passion yake. Atakuja fanya makubwa.
 
Kabla sijaanza na Mimi kufuatilia kiundani kuhusu huu mchezo, nilivyokuwa nikiangalia tu nilihisi tu huu mchezo utakuwa ni mgumu si mrahisi kama wanavyohisi watu kuwa ni kukimbiakimbia tu, inahitaji maandalizi ya kweli.
Yaan ukiwaona wanapiga tizi gym utajiuliza hawa wanajeshi Navy SEAL au madereva?
 
Kwa zaidi ya miaka ishirini nimejaribu kuufuatilia huu mchezo bila mafanikio yoyote. Sikuweza kuuelewa, kuupenda au kuufurahia. Sijui ni kwanini.
Nadhani ndio mchezo nisioupenda kuliko yote.

Asante mleta mada kwa kutuelezea kwa kina, umenifungua macho kuufahamu huu mchezo.
 
Ebu jaribu tena. Chagua team kwanza kabla haujachagua dereva.

Ukisema uchague dereva itakua mbaya akihama. Ni kama kwenye mpira, Uchague kumshabikia mchezaji akihama team unahama nae. Basi na huku madereva wanahama.

L. Hamilton msimu ujao hatakuwepo na Mercedes Benz atakua anaedesha Ferrari.

Ukishachagua team tu utaanza ushindani. Sio lazima uchague team kubwa, chagua ata team ndogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…