Madereva wa Formula 1, ni "Marubani" wa Jet za ardhini

Ahsante, kwa wale tuliokuw hatujui kitu kabisa umetufanya tunaweza tamba hata vijiwe vya kahawa.
 
aah umeeleza vizuri mchambuzi japo umejaribu kufafanua kwenye habari ya pointi ila sijaelewa imekaka vipi ndugu
Sio mbaya narudia mkuu, hope utaelewa.

Tumesema race moja inakua na magari (madereva) 20 kutoka team (constructors) 10. Hapa si tupo pamoja?

Sasa, mwisho wa race, kuanzia dereva namba 1 hadi namba 10 ndio wanaopata point, ila kuanzia 11 hadi 20 wanakula zero.

Ila point hawapewi sawa, zinagawiwa kwa namba 1 anapata nyingi na zinaendelea kushuka, kama hivi:



Kuna point za ziada mtu anaweza pata mfano "Fastest Lap" hii ni dereva aliekimbiza gari katika lap na kutumia muda mdogo kuliko wote, hii utapewa point 1 (ila ni kama tu upo kwenye iyo top 10), hope sijakuchanganya.

Fastest Lap ni kama Player of the Match (Man of the Match) katika kila mechi ya football tuseme.

Sasa izo point, dereva anakua anazikusanya kila mechi (kila race) na mwisho wa msimu mwenye nyingi ndio winner.

Ila constructors (team) nao wana kombe lao, ambalo linatokana na point ambazo madereva wao walizipata kwenye race. Kwahiyo mwishoni unaweza kukuta Dereva kombe kachukua Max Verstappen kutoka team ya Redbull ila kombe la Constructor wakachukua Mercedes Benz.
 
Hivi ile Circuit ya Monaco walishaitoa?
No ipo. Na last time ndio race ilikua uko. Moja kati ya GP kali na ngumu sana. Max alivomaliza alisema Monaco GP ilikua inaboa, yeye hakua ana race.. "F**k me, this is boring. Should have brought my pillow.”

PS: alishika namba 6. Namba 1 mtoto wa Monaco, Lecrec.
 
apo nimekupata meku
 
Nilikuaga sielewi, nilidhani majamaa yanakula pesa ndefu kilaini aloo kila kazi ni kazi aisee.
Mbona kama ni shurba hivi..😂😂

Pia enzi za utoto nilikua nadhani mpira ni rahisi sana. Zile warmup wanazofanya kabla ya mechi nilidhani ndo mazoezi yenyewe hufanywa kila siku. Aloo kumbe sivyo jamaa wanahenyeka kuna mwanangu alikimbia kambi kwenye timu daraja la kwanza kisa tizi kali na ratiba kama mko shule/jeshi.
 
😂😂😂 Na hamna pombe, hamna mademu.. ni gym gym gym kula
 
😂😂😂 Na hamna pombe, hamna mademu.. ni gym gym gym kula
Acha kabisa mkuu, ratiba unapangiwa kila kitu unapangiwa ka roboti vile.
Ni kama hao wa mbio za magari, muda mwingi almost robo tatu ya maisha yao wanaitumia kazini tuu.
 
Uzi mzuri, mimi pia ni miongoni mwa niliodhani huu mchezo ni wa starehe, kumbe sikujua mpaka pale nilipoamua kuwafuatilia kiundani. Hamilton anaelezea kuwa uzito wa dereva ni kitu muhimu sana kwenye race, na unakuwa calculated. Usizidi wala usipungue. Pia wanafanya sana mazoezi ya shingo, misuli ya shingo zao mostly ni mipana na imejaa, inawasaidia sana kuresist gravity kwenye kona kali.

Pia wanatrain sana reflex action (pengine kuwazidi magolikipa wa mpira wa miguu), inatakiwa uwe sharp sana kwenye kufanya maamuzi. A minor delay in decision making can cause fatal accident.

Pia jambo la weightloss umelielezea naye pia alieleza, in a single race unapoteza bodily fluids za kutosha kutokana na joto la engine kupelekea kupungua uzito hadi 3kg per race. All in all athleticism sio kitu rahisi, michezo yote katika level ya pro ni migumu. Inahitaji devotion na discipline ya kiwango cha juu sana. Imagine dereva anafanya mazoezi zaidi ya mwanajeshi wa kawaida. Asante kwa uzi mzuri mkuu.
 
Pia wanatrain sana reflex action (pengine kuwazidi magolikipa wa mpira wa miguu), inatakiwa uwe sharp sana kwenye kufanya maamuzi. A minor delay in decision making can cause fatal accident.
Shukrani mkuu.

Hapa umegusa pazuri sana. Yaani hakuna kublink. Hawa jamaa ukiangalia wanavoendesha, overtake, utafurahi. Sana. Hakuna kufikiria x2 ukitoa maamuzi excute chap.
 
Ukiona mikataba ya wachezaji professionals... wanaenda kazini kila siku, Jumatatu mpaka Ijumaa
 
Baada ya kupata hii elimu ntaanza kufuatilia boss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…