Madereva wa mabasi Nyegezi wakimbia kupimwa ulevi na macho

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, linawasaka Madereva zaidi ya 10 wanaoendesha magari ya mikoani na nje ya nchi waliokimbia kupimwa ulevi pamoja na macho katika kituo kikuu cha mabasi cha Nyegezi.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza Sunday Ibrahimu ametoa kauli hiyo mapema alfajiri baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwapima ulevi na macho madereva zaidi ya ishirini akiwa ameshirikiana na madaktari kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa huo ya Sokou toure na kusema zoezi hilo ni endelevu na kwamba waliokimbia watatafutwa.

"Unaona zoezi hili lipo serious lakini baadhi ya madereva wamekimbia, unapokimbia kimbia inaonekana umepiga maji jana na unashindwa kuja kupimwa lakini hautatoka humu ndani tutaruhusu madereva waliopimwa ulevi waliokimbia hatutakubaliana nao" amesema Sunday

Dkt. Elizabeth Makamba ni Daktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure anaeleza umuhimu wa kuwapima macho madereva, "Tumeamua kufanya zoezi hili ili kuangalia afya ya macho ya madereva sababu tunahisi kwamba mojawapo ya sababu ya ajali ni matatizo ya macho hivyo tupo hapa kwa ajili ya kuwapima macho kama dereva haoni vizuri ni rahisi kupata ajali".

Source: EATV
 
Kweli leo nimewaona asubuhi maana Jana usiku nilikesha Bar asubuhi naenda kuchukua bus nianze safari ya Dar nawakuta wakuda wanapima madereva wenzangu pombe, ila nimefanikiwa kuwatoroka naitafuta dodoma sahiv
 
😂😂😂
 
Sasa itakuwajeee[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]???
 
Linatakiwa liwe zoezi la lazima kila siku.
Madereva wapimwe kituo cha mwanzo na mwisho wa safari
 
Safi sana Hilo zoezi liende na mikoa mingine maana kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kuna ajali nyingi za kizembe
 
Kweli leo nimewaona asubuhi maana Jana usiku nilikesha Bar asubuhi naenda kuchukua bus nianze safari ya Dar nawakuta wakuda wanapima madereva wenzangu pombe, ila nimefanikiwa kuwatoroka naitafuta dodoma sahiv
Umekosa posho kwahiyo utakua unapata posho zakufikisha basi ulikokimbia Leo asb
 
Hii kitu imechelewa sana kuanza. Liwe zoezi la.nchi nzima.
 
Sasa itakuwajeee[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]???
Acha tu nilitoroka stand nikarud dakika 5 kabla ya gar kuanza kutoka kidogo wazuie gar maana ni lazima kuwe na madereva wawili sasa nikawa natafutwa sionekan ila mwenzangu alifanikiwa kutoa gar nikapandia nje
 
Inabidi upunguzeee nyqgii kpnd hk wakiwepoo[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]c unajua wanakujaga kwa mihemko ,mihemko ikikataa unaendelea kula nyagi kama kawaa[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Wanaonewa sana madereva wa mabasi. Wapimwe watu wote wakiwamo polisi, madaktari, mawaziri, wabunge nk, kwa nini madereva wa mabasi tu? Na zoezi liwe endelevu.
 
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, linawasaka Madereva zaidi ya 10 wanaoendesha magari ya mikoani na nje ya nchi waliokimbia kupimwa ulevi pamoja na macho katika kituo kikuu cha mabasi cha Nyegezi.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza Sunday Ibrahimu ametoa kauli hiyo mapema alfajiri baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwapima ulevi na macho madereva zaidi ya ishirini akiwa ameshirikiana na madaktari kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa huo ya Sokou toure na kusema zoezi hilo ni endelevu na kwamba waliokimbia watatafutwa.

"Unaona zoezi hili lipo serious lakini baadhi ya madereva wamekimbia, unapokimbia kimbia inaonekana umepiga maji jana na unashindwa kuja kupimwa lakini hautatoka humu ndani tutaruhusu madereva waliopimwa ulevi waliokimbia hatutakubaliana nao" amesema Sunday

Dkt. Elizabeth Makamba ni Daktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure anaeleza umuhimu wa kuwapima macho madereva, "Tumeamua kufanya zoezi hili ili kuangalia afya ya macho ya madereva sababu tunahisi kwamba mojawapo ya sababu ya ajali ni matatizo ya macho hivyo tupo hapa kwa ajili ya kuwapima macho kama dereva haoni vizuri ni rahisi kupata ajali".

Source: EATV

Ueleweke ubinafsi wa watanzania. Nimerejea kuangalia mwendelezo wa comments hapa. Si ajabu kuwa kwa uzi uliokuwa ukikimbia vile zaidi ya masaa 12 Sasa hakuna jipya baada ya #18.

Mtanzania anashangilia vikwazo na magumu kwa wengine lakini SI kwake. Ubinafsi uliopitiliza!
 
Back
Top Bottom