Kati ya yote haya ni nchi Gani madereva wao wanakosa hata Moja,,!???usiku,kichwa kimejaa bange,pombe,madeni,michepuko huku unabeba roho za watu.
Kwani mchana hazitokei ajali?!Umefanya tafiti wapi kuthibitisha hayo?, au umefanya generalization
Augustino Mrema alifuta safari za usiku ilikuwa ni kutokana na sababu za kiusalama, mabasi yalikuwa yanavamiwa na majambazi wenye silaha, kutekwa na abiria wote kuvuliwa nguo zote walizovaa mwilini na kisha abiria kubaki uchi wa mnyama. Nguo zote za abiria pamoja na mizigo yao yote ilikuwa inaporwa na majambazi na kutokomea nayo kusikojulikana.Safari za mabasi za usiku zilikuwepo kitambo,Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani akazifutilia mbali.
Alijua akili zetu watanzania,madereva wetu hawana uwezo wa kuendesha usiku,kichwa kimejaa bange,pombe,madeni,michepuko huku unabeba roho za watu.
Watatumaliza
Safari za mabasi za usiku zilikuwepo kitambo,Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani akazifutilia mbali.
Alijua akili zetu watanzania,madereva wetu hawana uwezo wa kuendesha usiku,kichwa kimejaa bange,pombe,madeni,michepuko huku unabeba roho za watu.
Watatumaliza
Ilikuwa ni kwa sababu ya ajali!!! Narudia tena: ilikuwa ni kwa sababu ya ajali.Augustino Mrema alifuta safari za usiku ilikuwa ni kutokana na sababu za kiusalama, mabasi yalikuwa yanavamiwa na majambazi, kutekwa na abiria wote kuvuliwa nguo zote walizovaa mwilini na kisha abiria kubaki uchi wa mnyama. Nguo zote za abiria pamoja na mizigo yao yote ilikuwa inaporwa na majambazi na kutokomea nayo kusikojulikana.
Barabara nzuri? Naona hujui maana ya barabara nzuri. Tena siku hizi ndiyo imekuwa hatari zaidi kwa sababu kwa vile barabara nyingi zina lami, madereva wanakimbia sana. Na hapa ndipo tunapokuja kwenye kiini cha tatizo: barabara ni nyembamba na zina kona nyingi. Matokeo yake ni magari kugongana au kupinduka.Kiongozi;
MAMBO YAMEBADILIKA sio kama enzi ya Mrema
1. Sikuhizi tuna barabara nzuri
2. Mabasi yamekuwa ya kisasa haswa (Yanachoo, yana camera, yana visibiti mwendo nk nk)
3. Uelewa umeongezeka kwa madereva na Abiria kujua wajibu wao (watu wengi wamesoma),
4. Vitu vingi kwa sasa ni Digital badala ya kutegemea traffic , mtu anaweza kufuatilia basi akiwa nyumbani/ofisini masaa 24
5. Usalama umeimarika sana hata kule maeneo ambayo Ilibidi kutemebea na askari enzi za Mrema
6. Watu wengi wame elimika (wanahitaji kufanya kazi) badala ya kushindwa kutwa kwenye mabasi (ni matumizi mabaya ya nguvu kazi)
Tanzania watu wenye sifa ya kuitwa madereva ni wachache sana. Hii ni kwa sababu namna watu wanavyofundishwa kuendesha magari ni kama utani. Mtu anamfundisha rafiki yake siku mbili, siku ya tatu anamwachia gari aendeshe mwenyewe. Halafu sasa wabongo walivyo wabishi na wajuaji. Kila mtu ni mjuaji wa kuendesha wakati wengi hawajui sheria.Mimi nalia na taa za booster sijui TBS, Polisi na Mamlaka zingine wapo wapi. Unakutana na mtu kawasha full light booster aisee anakupiga mwanga hadi gari ya nyuma nayo anaona full light.
Hizi ndio tatizo hasa ajali za usiku, zile taa ukutane nazo ghafla lazima uhame kidogo au sana, na kama umekunywa mtungi chenchi unaeza rudisha kabisa.
No biashara ila madereva wengi wa kitanzania hawajui matumizi ya full light. Mahali kuna taa za bara barani bado mjinga mmoja amewasha full light tena za booster.