Madereva wa mabasi ya abiria Tanzania hawana akili ya kuendesha usiku,tutakwisha

Siku hao wanaopewa za kubrashi wakiacha na kufanya kazi walizopewa naapa madereva wangenyooka

Ila tatizo hata mlevi anaachiwa kisa katoa buku 2
Halafu wanachukua chochote kama ombaomba
Yale maandamano mngekuwa mnaandamana kwa mambo kama haya
Buku 2 zimeondoka na roho za watu wengi sananchi hii
 
Tanzania watu wenye sifa ya kuitwa madereva ni wachache sana. Hii ni kwa sababu namna watu wanavyofundishwa kuendesha magari ni kama utani. Mtu anamfundisha rafiki yake siku mbili, siku ya tatu anamwachia gari aendeshe mwenyewe. Halafu sasa wabongo walivyo wabishi na wajuaji. Kila mtu ni mjuaji wa kuendesha wakati wengi hawajui sheria.
Basi la mamilioni na roho za watu unamuwachia rafiki yako,wanaita day waka
 
Safari za mabasi za usiku zilikuwepo kitambo,Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani akazifutilia mbali.
Alijua akili zetu watanzania,madereva wetu hawana uwezo wa kuendesha usiku,kichwa kimejaa bange,pombe,madeni,michepuko huku unabeba roho za watu.
Watatumaliza
Kwahiyo wakiendesha mchana: bangi, pombe, madeni na michepuko vinaisha!!?
 
Siku hao wanaopewa za kubrashi wakiacha na kufanya kazi walizopewa naapa madereva wangenyooka

Ila tatizo hata mlevi anaachiwa kisa katoa buku 2
Halafu wanachukua chochote kama ombaomba
Yale maandamano mngekuwa mnaandamana kwa mambo kama haya
Hello, tuangalie tatizo kwa upana. Kufeli kwa usalama barabarani ni tatizo la uongozi wa nchi kwa ujumla. Huwezi kuandamana kwa ''mambo kama hayo'' bali unaandamana kwa kilichosababisha ''mambo kama hayo'' i.e uongozi wa nchi! Kuanzia ubovu wa barabara (barabara kuwa na lami haimaanishi ni nzuri kama wengi wanavyodhani), rushwa barabarani, madereva kuendesha huku wamelewa, hayo yooooote chanzo chake ni serikali kushindwa kusimamia nchi.
 
Tanzania watu wenye sifa ya kuitwa madereva ni wachache sana. Hii ni kwa sababu namna watu wanavyofundishwa kuendesha magari ni kama utani. Mtu anamfundisha rafiki yake siku mbili, siku ya tatu anamwachia gari aendeshe mwenyewe. Halafu sasa wabongo walivyo wabishi na wajuaji. Kila mtu ni mjuaji wa kuendesha wakati wengi hawajui sheria.
Shida sana
 
Mrema alizikimbia changamoto badala ya kuzikabili
 
Hello, tuangalie tatizo kwa upana. Kufeli kwa usalama barabarani ni tatizo la uongozi wa nchi kwa ujumla. Huwezi kuandamana kwa ''mambo kama hayo'' bali unaandamana kwa kilichosababisha ''mambo kama hayo'' i.e uongozi wa nchi! Kuanzia ubovu wa barabara (barabara kuwa na lami haimaanishi ni nzuri kama wengi wanavyodhani), rushwa barabarani, madereva kuendesha huku wamelewa, hayo yooooote chanzo chake ni serikali kushindwa kusimamia nchi.
Ndio hivyo
Kama sheria zitafuatwa naona madereva wengi wangekuwa wako vijiweni wamekaa
Ila nobody cares
 
Kati ya yote haya ni nchi Gani madereva wao wanakosa hata Moja,,!???
Note! Sheria kutokufuatwa, uwajibikaji mbovu wa trafic police na miundombinu mibovu + ujinga wa abilia ndio sababu ya ajali na vifo,,dereva anatenga elfu hamsini dar to mwanza ili aende speed ya 120 road , trafic wote wanakula elfu tanotano, wakiingia ndani ya basi utasikia vipi mwendo, abilia sasa walivo mazuzu utasikia kwa kweli ni mzuri baba!!subiri wapate ajali Sasa, utasikia Ile mwendo nilijua tu tutaanguka,. !!!!
Yani sijui kuna shida gani tu kwakweli huwa inanikwaza sana hiyo kuna siku jamaa alikimbia sana ilikuwa dar - tabora mi nilinyanyuka nikamfata nikwambia hujabeba neti humu watu walinunia vibaya sana. Kwamba nataka wachelewe.
 
Hata nikiona mtu mzima na akili timamu anaenda kupanda basi usiku kwa madereva hawa watanzania ujue huyo mtu ana walkini

Kifo kipo lkn kusafiri usiku ni kujiwahisha kaburini kwa madereva hawa watanzania
 
Yani sijui kuna shida gani tu kwakweli huwa inanikwaza sana hiyo kuna siku jamaa alikimbia sana ilikuwa dar - tabora mi nilinyanyuka nikamfata nikwambia hujabeba neti humu watu walinunia vibaya sana. Kwamba nataka wachelewe.
Wa TZ ni tatizo kama hizi mvua za Sasa hivi
 
Ilikuwa ni kwa sababu ya ajali!!! Narudia tena: ilikuwa ni kwa sababu ya ajali.
Ni kweli ajali ulikuwepo ndiyo, sikatai. Lakini suala la usalama kutokana na vitisho vya ujambazi, utekaji na uporaji vilikuwa vingi sana. Hiyo ndiyo sababu iliyochagiza sana ktk kufutwa kwa safari za mabasi ya abiria kusafiri mida ya usiku hapa nchini Tanzania. Utekaji wa mabasi ulikuwa ni mkubwa Sana, ujambazi ulishamiri sana hali iliyomlazimu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi wa wakati huo Bw.Augustino Mrema kusitisha safari za usiku sambamba na kuanzisha Vito vya Polisi karibu kila Kata au Mitaa hapa Tanzania.
 
Barabara nzuri? Naona hujui maana ya barabara nzuri. Tena siku hizi ndiyo imekuwa hatari zaidi kwa sababu kwa vile barabara nyingi zina lami, madereva wanakimbia sana. Na hapa ndipo tunapokuja kwenye kiini cha tatizo: barabara ni nyembamba na zina kona nyingi. Matokeo yake ni magari kugongana au kupinduka.

Kimsingi kukimbiza gari sio chanzo kikuu cha ajali za barabarani; Sababu za ajali zipo nyingi ila kikubwa nikutokufuata sheria za barabarani na ubovu wa magari hasa MALORI unaopelekea yaachwe hovyo hovyo barabarani yakiwa yameharibika
 
Kati ya yote haya ni nchi Gani madereva wao wanakosa hata Moja,,!???
Note! Sheria kutokufuatwa, uwajibikaji mbovu wa trafic police na miundombinu mibovu + ujinga wa abilia ndio sababu ya ajali na vifo,,dereva anatenga elfu hamsini dar to mwanza ili aende speed ya 120 road , trafic wote wanakula elfu tanotano, wakiingia ndani ya basi utasikia vipi mwendo, abilia sasa walivo mazuzu utasikia kwa kweli ni mzuri baba!!subiri wapate ajali Sasa, utasikia Ile mwendo nilijua tu tutaanguka,. !!!!
Ndio wabongo tulivyo
 
Ni kweli ajali ulikuwepo ndiyo, sikatai. Lakini suala la usalama kutokana na vitisho vya ujambazi, utekaji na uporaji vilikuwa vingi sana. Hiyo ndiyo sababu iliyochagiza sana ktk kufutwa kwa safari za mabasi ya abiria kusafiri mida ya usiku hapa nchini Tanzania. Utekaji wa mabasi ulikuwa ni mkubwa Sana, ujambazi ulishamiri sana hali iliyomlazimu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi wa wakati huo Bw.Augustino Mrema kusitisha safari za usiku sambamba na kuanzisha Vito vya Polisi karibu kila Kata au Mitaa hapa Tanzania.
Narudia: Ni ajali. Kwanza mikoa iliyokuwa na utekaji wa mabasi mara nyingi ni huko kanda ya Ziwa. Barabara kama za Tanga-Dar, Arusha-Dar, Mbeya-Dar n.k. ilikuwa ni sehemu zisizo na matukio ya utekaji mengi au hakuna kabisa. Zilifululiza ajali mbaya kwa kipindi kifupi ndiyo wakapiga marufuku.
 
Back
Top Bottom