Kwa reply hii unaonekana umri wako bado mdogo uongozi wa mwinyi haukuukuta Yule ni kiongozi aliye leta mabadiliko makubwa sana nchini hapa
Siku nikiwa na mood nitakupa ABC 😀
Nchi inaingia kwenye vyama vingi mimi niko .
Sikiliza Broo acha kushikisa akili na mafisadi na Mabeberu wabinafsi .
Unafikiri Mwinyi angeweza kuiongoza nchi katika vita ya Uganda kwa miaka miwili usiku na mchana kwa nchi ille ya Ruksa iliyojaa rushwa na kupotea kwa uzalendo kwa kiwango cha juu.
Mwanyi atakumbukwa kwa Ruksa iliyotoa nafasi ya demokrasia na kukosoana lakini sio kujenga taifa moja wala mifumo .
Niwe mkweli bila unafiki .
Mwinyi alishindwa kuongoza nchi alikaa kama Imamu wa msikiti anayesubiri misaada ya Nyama ya ngamia toka Uarabuni.
Enzi za mwanyi majeshi yalibaki kidogo kuwa kama Yale ya Kongo ,Wanajeshi na mapolisi yalihusishwa sana na ujambazi mkubwa wa silaha za moto mchana kweupe .
Wanajeshi na polisi na magereza hawakuwahi kuwa na uniform mpya wala kulipwa mishahara inayokidhi hata matumizi ya wiki moja .
Mfumuko wa bei ulikua juu sana .
Uhuni na biashara ya kuchapisha fedha ukaanza ,kila kukicha fedha zinachapishwa mpya na kuwekwa nyingine na kushika thamani kwa kasi ya ajabu .
Wahuni walianza kuhujumu kwa kasi mashirika ya umma .
Miaka ya kwanza ya Mwanyi palikua na kitu kinaitwa Fagio la Chuma ,alianza vizuri kupambana na rushwa lakini lengo lake lilikuwa ni kuweka watu alioendana nao kwenye mifumo wake.
Elimu ya Mwanyi ilikua ni ya kawaida ,akakutana na mapropessa kama akina Kigholma Ali malima na Lipumba waliojaa ubinafsi na chuki kubwa kwa watu wa imani nyingine . Hawa walimpotosha sana badala ya kujenga nchi kwa misingi ya kizalendo wakawaza Udini zaidi na kila kitu kitawekwa kwenye mizania ya Udini .
Waarabu kama kawaida yao wakatafuta uchochoro wa kupenyeza harakati za Kibeberu zilizokua zinasasisiwa na Wamarekani kuingiza misaada ya kidini ,mabilioni yakamwagwa kwa agenda za kuiunganisha Tanzania na umoja wa nchi za kiislam . Matajiri wakaibuka kama uyoga kwa kupitia pesa za magaidi wa alioshirikiana na Nchi za magharibi .
Pakaonekana kama vile **** vile kuna mzunguko mkubwa wa pesa lakini pesa ikawa haina thamani kabisa maana ni madola yaliyokuwa yanaingizwa kinyemela
la kwa ajili ya harakati na ujenzi wa misikiti ,huku wakiwa wanajipanga kwa ajili ya kuifanya Tanzania kujiunga na umoja wa nchi za kiislamu kwa ahadi ya kupata misaada isiyokuwa na riba .
Yaani nchi yenye madini ya dhahabu,gesi,mafuta ,wanyama ,ardhi ,wetu wenye nguvu na uwezo wa kufanya kazi za nguvu ,nchi yenye mitano ,maziwa na milima na wanyama halafu ikataka kugawanyika kidini kwa sababu ya misaada kutoka nchi na watu wakaanza kugawanyika .
Pakaibuka migawanyiko mpaka ndani ya Dini ya kiislam ,pakaibuka taasisi tofauti na Bakwata . Hawa wanaonekana wana imani kali ,wakawa wanapata nguvu kubwa zaidi ya misaada ya fedha kutoka nje ,misikiti mingi ikawa inajengwa chini yao . Mwinyi alijua kila kitu na alikua nyuma ya haya yote . Uislama ukaanza kuwa na makundi yenye hulka ya kigaidi na chuki kubwa kwa Bakwata na dini nyingine .
Pesa ni sabuni ya roho na sio dini . Yote haya yalikua yamejikenga kutokana na pesa kutoka uarabuni .
Loliondo ikauzwa kwa Familia ya mfalme wa nchi za kiarabu . Mpaka leo hatujui aliyeuza yeye alipewa nini huko Uarabuni ! Au ni mapenzi tu kwa waarabu na mila na dini zao ! Kosa kubwa sana lilifanyika . Haya ni madhaifu makubwa sana ya kiuchumi na kijamii kwa vizazi na vizazi .
Wanafunzi wakaanza kugawanyika kwenye mashule ,wengine wanasema sisi tunafuata mila na desturi za kiarabu na dini yetu na wengine watajua wenyewe . Hapakuwahi kuwa na mjadala wa kujadili vazi la mtanzania na utu na heshima ya mwafrika ili tuondokane na mavazi ya wakoloni wakiwemo waarabu . Yaani vazi ni la mkoloni mzungu .Anakuja kiongozi badala ya kuondokana na ukoloni anaturudisha nyuma zaidi kwa kuenzi mavazi ya mkoloni ambaye hakuwahi kujenga taasisi yoyote ya pamoja kama shule ,hospitali , wala mfumo wa ajira kwa kutangaza kuwa war
mafunzi wa dini moja wavae uniform kwatindo wa Wakoloni tena.
Tulidhani angekuja na wazo la kubuni vazi la kiafrika na kuachana na mavazi yote ya wakoloni bila kujali dini ili tuwe na taifa moja lenye upendo na mshikamano zaidi .
Watu wakaua kabisa mali za umma kwa ufisadi na rushwa kisha wakajijenga binafsi na familia zao .
Baadhi ya watu wasiojali vizazi vijavyo kwa maslahi mapana zaidi wakatumia vyombo vya habari kufurahia mapesa mengi mifukoni kama ilivyo kule Kinshasa .Miji kama Dar es salaam ,Arusha ,Mwanza , Mbaya n.k Uhalifu ukawa mkubwa wa sana . Arusha ukawa ni mji wa kihalifu ,risasi zinapigwa mchana kweupe watu wanaoporwa na kuuawa kama Kolombia ,biashara ya madawa na kutorosha madini ikawa ni halali kabisa . Kodi haikuwa inalipwa . Hapakuwa na mfumo wa kiuchumi zaidi ya Mwenye nguvu mpishe.
Harakati za Mwembe chai zikaanza . Misikiti ikawa ni Sehemu ya kuandaa wanaharakati waliokua wanasema kuwa Mfumo wa nchi ni wa kikristo hivyo ni lazima ukomeshwe na kuwekwa mifumo ya kisharia kwa kanzianzisha mahakama ya kadhi na eti waislam walikua wanabaguliwa .
Huku nje mwanyi alikua anaonekana anayakemea lakini hakuziba mianya ya ukuaji wa hao waliokua wanayaasisi hayo ambao walikua wanafadhiliwa na magaidi kutoka nje kupitia taaisisi za dini.
Nilishuhudia Waumini wa kiislam wakipigana kwa kugombea misikiti kwa sababu ya misaada .
Mbali na taaisisi za kiislam lakini pia hali ya ubinafsi na misaada ya fedha toka nje iliibua pia vurugu kwa baadhi ya madhehebu ya dini ya kikristo kama vile KKKT kule Meru kwa sababu ya kuwa na serikali iliyoweka ruksa bila kuweka mikakati ya kujenga taifa kupitia katiba imara yenye kujenga uzalendo ili kuendana na uongozi uliotaka kujipambanua kama ruksa . Ruksa isiyofuata sheria ni vurugu na uhuni .
Kiongozi aliyekua shemeji wa wanafunzi wa Jangwani . Hatari kabisa . Nchi ikakosa maadili kabisa .
Mrema akajaribu kupingana na rushwa na ufisadi lakini akapata cha mtema kuni kwa kufukuzwa ndani ya Baraza la mawaziri.
Lakini pamoja na mabaya ya yule Mzee ruksa (Mungu ampe pumziko la milele huko Ahera ) lakini alikua na mazuri yake .
Alikua mpole sana ,
Alipenda sana kuswali swala tano .
Alikwenda kuhiji mara kwa mara ili kuondoa dhambi zake.
Alikua mkarimu sana kwani wageni walipomtembelea aliwapa zawadi za wanayama .
Alikua hana chuki za wazi na hakupenda shari .
Hakumsema vibaya mtangulizi wake na alimheshimu sana .
Hakuwa mbaguzi wa wazi wazi wa kikabila wala dini .
Aliwapa kipaombele wawekezaji wa Kihindi na kiarabu kununua mashirika ya Umma na hata ardhi kubwa kama ardhi ya kilimo cha mkonge japo palikua na Kashafa nyingi katika uwekezaji huo .
Aliruhusu Mitumba kuingia kwa kasi nchini japo iliua viwanda vya nguo kwa sababu haikutozwa kodi ipasavyo.
Alisaidia watu kutajirika haraka haraka kutokana na biashara ya magendo .
Aliruhusu mawazo ya Mwalimu Nyerere ya kukubali mfumo wa vyama vingi uanze japo kura za maoni zilizojaa vitisho na mizengwe zilionyesha kubwa watu wengi hawakukubaliana na mfumo wa vyama vingi. Nyerere akashauri wachache wasikilizwe kulingana na ukweli kuwa wengi walikua na elimu ndogo sana ya masuala ya demokrasia na mifumo ya utawala wa kidemokrasia.
Mabaya ya Mwinyi yaliibua Madai ya Nchi ya Tanganyika tena ndani ya bunge . Kama sio Nyerere Mwinyi angemaliza muda wake na Zanzibar yake na Tanganyika ingekuwa imerejea.
Mabaya ya Mwanyi yalisababisha Mrema kupata kura nyingi sana ambazo kama sio Nguvu ya Nyerere leo hii CCM tungekua tunaisoma kwenye magazeti ya zamani na vitabu vya zamani .
CCM ilikua imeshindwa vibaya sana katika uchaguzi wa kwanza kabisa wa vyama vingi kwa sababu watu walikua wamechoka kabisa utawala wake na vitendo vya kifisadi , rushwa na kukosekana kwa mifumo ya kitaasisi ndani ya nchi zaidi ya watu wachache wauza magendo na mawakala wa taasisi za kidini kunufaika na pesa zisizo rasimi na biashara holela .
Bila shaka watu wanaelewa nini hua kinaendelea utawala unapokua wa kifisadi . Bila shaka ni kundi la wenye fedha kutumia fedha kupamba mifumo mibaya kwa manufaa yao huku wakiua kabisa mifumo imara ya kitaasisi.
Uganda waliingia kwenye mabadiliko makubwa ya kuitawala kama ilivyo Rwanda lakini walisimamia misingi ya kitaifa na kujenga uchumi sio kuruhusu wageni kunyonya na kumiliki mali na rasilimali zote za umma kwa sababu ya misaada kama alivyofanya Mwinyi .
Kama Nyerere alikosea basi hatukutegemea kuona nchi inauzwa kwa watu wachache wakwepa kodi,wanaharakati kidini n.k kwa sababu ya kutegemea misàda. Alipaswa ajenge mifumo ya kusimamia rasilimali za umma kwa ukali na kuwafukuza wote wanaojaribu kuhujumu na kujimilikisha mali za umma kwa maslahi yao eti ni Ruksa . Hakuna duniani nchi inayoendeshwa kwa kuruhusu kila mtu kufanya anachotaka bila sheria mahususi . Matokeo yake ni waliofuata kama Mkapa kuonekana kuwa anafilissi matajiri kumbe ni utamaduni waliozoea wa kufanya biashara za magendo na kukwepa kodi na mihadarati na pesa za bure toka nje kwa migongo ya dini .
Mfumo wa mwali mpaka kesho ukisimamiwa vizuri ndio utakaoinua uchumi wa nchi hii na kujenga umoja na mshikamano na pia kujenga siasa zenye utawala bora na uzalendo na kulinda rasilimali za umma zinazotekelezwa kwa kasi na mafisadi kama vile kiama kinakuja kesho.
Binafsi nilikua nampenda sana Mwingi kwa uungwana wake ,upole wake , ukimya wake na uvumilivu wake na huruma yake lakini pia kwa sababu ya sura yake yenye Tabasamu na furaha na mifano yenye busara muda wote .
R.I.P Mzee Ruksa.