Madereva wa mabasi za abiria na malori wapatao 200 wamefutiwa leseni zao kuanzia Agosti hadi Novemba

Madereva wa mabasi za abiria na malori wapatao 200 wamefutiwa leseni zao kuanzia Agosti hadi Novemba

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama barabarani nchini limewafutia leseni madereva wa mabasi za abiria na malori wapatao 200 kuanzia mwezi Agosti hadi Novemba 2024 kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani.

Hayo yamebainishwa leo Desemba 12, 2024 na Mkuu wa Idara ya Elimu ya Usalama Barabarani kwa umma ACP. Michael Dereli wakati wa mafunzo kwa afisa usafirishaji (madereva wa bajaji na pikipiki) wilayani Shinyanga.

Wakizungumza wakati wa mafunzo hayo maafisa usafirishaji wameeleza changamoto wanazokumbana nazo katika kazi zao huku wakiziomba mamlaka husika kuwachukulia hatua baadhi ya madereva wa mabasi na magari makubwa wanaovunja sheria.

Akitoa mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya Elimu ya Usalama Barabarani kwa umma ACP. Michael Dereli amewataka afisa usafirishaji wa bajaji na pikipiki kufuata sharia za usalama wawapo barabarani ili kuepukana na ajali zisizo za lazima.

Aidha ACP. Dereli amewasihi madereva hao kutojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa abiria wao pindi wanapowabeba kwani kwa kufanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria.





Mwenyekiti wa madereva pikipiki (bodaboda) wilaya ya Shinyanga Mohammed Juma alishukuru jeshi la polisi usalama barabarani kwa kutoa elimu hiyo huku Mwenyekiti wa usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Seif Nassor akitoa wito kwa maderva kutoa taarifa pindi wanapokutana na vitendo vya uvunjifu wa sheria.
 
Back
Top Bottom