Madereva wa Subaru Mna Matatizo Gani?

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
55,727
Reaction score
123,094
Jamani mimi najiuliza madereva wa subaru(wengi wao) wana matatizo gani? Nasema wana matatizo kwa sababu wana fujo zisizo na msingi barabarani. Unakuta mtu na subaru yake anapita barabara ndogo na 100kph kwa nini?

Hamuwezi kuendesha gari kistaarabu? Madereva wa subaru wamesababisha ajali na vifo vingi sana hususan Dar es salaam kwa uendeshaji wao wa sifa. Na nimechunguza nikakuta ni watu wa umri kati ya miaka 24-35 lakini wanatabia kama za watu wa 16-20 barabarani, mliruka hatua za ukuaji?

Jaribuni kujiheshimu barabarani watu mna watotona wategemezi kibao lakini mnafanya mchezo na vyombo vya moto, fujo zisizo na mpango hazina faida yoyote.
 

Ntajirekebisha mkuu tatizo ni kuwa it gives confidence in motion whenever u press it..
 
Unachosema ni kweli kabisa. Hata mimi wakati mwingine nafikiri labda sijui hizi Subaru ndo watu wanadhani ni sport cars huku kwetu! Sijui! Ila nackia Ulaya watu wanasemaga kuwa madereva wa BMW mara nyingi wanaendesha kipumbavu(labda kwasababu gari zao ni ghali), labda hizi Subaru ni version yao nyingine huku Bongo
 
Subaru ni gari maarufu sana hasa kwwnye mashindano ya magari ya East Africa safari rally,kuna Subaru imprezzer iliwahi kutia fora sana na hua zinashiriki mashindano mengi ya magari na labda zimeboreshwa sana ndiyo hata mtu akiwa nayo mtaani anaiendesha kama vile yupo kwenye mashindano ya magari.
 
Muundo wa injini ya magari haya nitofauti na magari mengine kwa hiyo inazifanya ziwe zinatoa sauti ambayo mtu kama sio makini inakupa hamasa ya kuikamua zaidi.
 
Its true,bmw drivers europe ndio wako arrogant na fujo kiania, ila huko ukileta ujinga ukibananishwa ni driving ban au jela au vyote kwa pamoja.
 
Reactions: Lee
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…