Madereva wa Subaru Mna Matatizo Gani?

Hakuna mtu anataka kufa ila kweli, ukiketi penye kiti cha dereva kwenye subaru, kuna raha yake. Uwe umetoka kwenye magari mengine halafu uendeshe subaru. Halafu uwe mefunga vioo huku uwe umekamata high way. 160 inakuhusu baada tu ya km 5 za take off. Naipenda subaru. Ile gari, breki yake waliisomea.
 
Bravo mkuu, confidence in motion.[emoji106]
 
Nimeipenda forester sti
2.5lt
Gear 6 manual
Bei yake tu ndo mauaji
Bei ya kununulia ni 11,000$
Tsh 24,000,000
Kodi 9,600,000
Jumla 33,600,000
Mil 34 zahitajika hapo
Bado hapo hujaweka chochote kile
 
Hahaahhaahaha nilishamaliza 180km/hr na ikawa inaenda kwenye zero, sitakaa niendeshe namna ile tena, zile gari ni za shetani. Tulikua tunakwenda Lushoto kumzika rafiki yangu Mohamed Mtoi....
 
Kuna wawili wako barabara ya Nyerere...acha tu...mawazoni nahisi wako kwenye v8 new new model...
 
hyo forester mil 34 mpya au used kdogo
Hamna mwenye ujanja wa kununua mpya hapa...fujo zote hizo gari zenyewe zina miaka zaidi ya kumi...chochote kinaweza kutokea!
 
kuna sehem nimeona ya blue ata namba aina ni mil 20
 
Umenena mkuu inata u smart hii kitu ila tamu mkuu
 
Sasa lini tunaenda kuendesha.........?.....nyie woooooote hapa wenye Subaru.......tunaomba tuwaalike (ambao hampo Chugga) mechi ya kirafiki na Subaru Kaskazini.......ili tudumishe uJF wetu........
 
hvo vi forester vikileta kelele dawa yao mistubish evo 9 generation torque 392nm ,280hp speed 280
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…