Madereva wa Subaru Mna Matatizo Gani?

Madereva wa Subaru Mna Matatizo Gani?

Unajua kuna kipofu alipata nafasi ya kuona kwa sekunde chache akaona punda,basi kila akisikia mtu anasema kaona kitu kizuri yeye huuliza kama punda? Ndio kama wewe unaamini hamna gari inaweza kuishinda subaru.

Ngoja nikwambie subaru is just quick from 0-60mph (0-100) ila kuna magari mengi tu yanakimbia kuliko subaru, najua kuna rafiki yangu ana subaru alikuwa anaenda moshi alikutana na beast moja la euro lilimnyanyasa mpaka akatafuta hela akanunua hilo gari.

Kwahio msikariri nyinyi ndio mnaendesha gari zinazokimbia kuliko wengine,wenzenu wako responsible ingawa wana powerful cars, kuna watu wana ferrari,lamborghini,aston martin,porsche carrera 911 gt ushawahi kuziona zinafurumushwa hapa mjini? Unajua speed zake hizo gari?

Btw jaribuni MITSUBISHI EVO10.

Hivyo visubaru vyote haviingii kwenye products za BMW au VW au AUDI.

Mi naziita ni Cheap Sports Cars, ingekuwa wana uwezo wa kumiliki ferrari au lamborghini au McLaren ndo wangejua maana ya sports car.
 
Jamani mimi najiuliza madereva wa subaru(wengi wao) wana matatizo gani? Nasema wana matatizo kwa sababu wana fujo zisizo na msingi barabarani. Unakuta mtu na subaru yake anapita barabara ndogo na 100kph kwa nini?

Hamuwezi kuendesha gari kistaarabu? Madereva wa subaru wamesababisha ajali na vifo vingi sana hususan Dar es salaam kwa uendeshaji wao wa sifa. Na nimechunguza nikakuta ni watu wa umri kati ya miaka 24-35 lakini wanatabia kama za watu wa 16-20 barabarani, mliruka hatua za ukuaji?

Jaribuni kujiheshimu barabarani watu mna watotona wategemezi kibao lakini mnafanya mchezo na vyombo vya moto, fujo zisizo na mpango hazina faida yoyote.
Arusha kuna umoja unaitwa "SUBARU GENERATION" huwa wanashiriki Rally nafikiri kila baada ya miezi mi3, ni wasumbufu sana hao watoto na ukiwa na subaru nzuri wanakuja kukodi kwako.

Ni sifa na mbwembwe tu kitaani.
 
Sasa lini tunaenda kuendesha.........?.....nyie woooooote hapa wenye Subaru.......tunaomba tuwaalike (ambao hampo Chugga) mechi ya kirafiki na Subaru Kaskazini.......ili tudumishe uJF wetu........

Mmmmh Preta wewe
 
Siku hali ikiruhusu nitahamia VW ya mjerumani au BMW
 
Spare usipime last time tulinunua set moja ya break pads kwa 160000 original lakini
Ukimiliki ile gari ule na mbavu za kuiendesha na kuihudumia ipasavyo...
Spare parts zake ni exoensive kwa kweli...
Nimenunua juzi set zote OG za legacy kwa 550,000
 
Mbabe wa Subaru ni Mitsubishi Evo VII na kuendelea hapo Subaru inakaa, Tanzania Subaru ni mengi sana sababu ni bei rahisi zaidi ya EVO...
 
Mbabe wa Subaru ni Mitsubishi Evo VII na kuendelea hapo Subaru inakaa, Tanzania Subaru ni mengi sana sababu ni bei rahisi zaidi ya EVO...
Natamani sana niifahamu vizuri hii gari aina ya POSCHE
 
Subaru killed my aunt. fake witnesses say the driver was driving "slowly". woe to them!
 
Back
Top Bottom