Hapana siyo kweli kuhusu mahari or posa kubwa inategemea na familia yenyewe, ila kuhusu mahari kugawanywa hadi kwa majirani ni kweli,sisi tunaamini jamii nzima inahusika katika malezi ndiyo maana jirani anaweza akakuadhibu kama kama mzazi wako, ikitokea kuna kitu kibaya umefanya amekuona, so yes wanahusika kwenye mgao hata kama watapata kiasi kidogo( nilishawahi kushuhudia majirani wamegawana sh 3000 3000 za mahari ya binti, ni kwa furaha tu wanafanya hivo na wanapiga vigelegele na kushangilia sana kama kumpa baraka binti yao huko aendako).
Pia mama kuwa na sauti mmh hapana hivi unawajua mashangazi na kaka yao(baba binti) mkuu ? Wao ndiyo wenye sauti, Mama anakua anasikiliza tu hana say sana.
Karibuni muoe unyakyusani, tuna roho nzuri mno siyo wabishi( najipigia promo kidogo😃🥰 )