- Thread starter
- #21
Heshima kwako pia Mkuu 🙏🏾. Ngoja tusubiri lakini alipokula kiapo huku akiwa ameshika kitabu kitakatifu cha dini yake na kutamka atailinda na kuitetea Katiba ya nchi halafu huu mwezi wa tatu sasa anajua fika kwamba kuwepo Bungeni kwa COVID-19 ni uvunjwaji wa katiba kwa Wabunge FAKE kuendelea kulipwa billions of taxpayers money na yeye yuko kimya ni UNAFIKI wa hali ya juu kuhusu kwenda kinyume na kiapo chake.
Na wahenga walisema siku njema huonekana asubuhi na asubuhi inazidi kuyoyoma ni 11:00am now she is fast approaching 12 noon.
Tusubiri ila mimi machale YAMESHANICHEZA pamoja na kuwa baadhi ya mambo aliyoyafanya hadi sasa nayafurahia na kuyaunga mkono.
Mkuu BAK heshima kwako tena. Covid 19 bungeni ni ukakasi mkubwa. Ila kumtegemea mama kuwa angelivalia hili njuga dhidi ya Jobo na mhimili wake, itakuwa ni kusubiri dodo kwenye mnazi.
Hili labda tusubiri Chadema itakapokutana naye angalau kusikia maoni yake pamoja na mengi mengine yaliyo fyongo na hata muhimu zaidi.
Wapongezwe Chadema kwa msimamo wao kuhusu wabunge wale. Kwa Chadema wale wamefukuzwa. Si wanachama tena na Chadema haipokei ruzuku kuwahusu wala michango ya wasiokuwa wanachama wake. Kwa hili, kwa mujibu wa Chadema - this is a closed case.
Mawili yafuatayo ni ya muhimu zaidi kwetu kama watanzania:
1. Kushughulikia UVIKO kisayansi - hili ni dharura kweli kweli. Mzee Kaunda ndiyo hivyo tena.
2. Kuhitaji haki kurejelewa - hili lahitaji uwepo wa katiba mpya.
#1 Mama aliteua tume ya wataalamu wabobezi. Na sasa tuko njiani kupata chanjo.
#2. Lisemwalo lipo kama halipo laja. Tumpe mama muda wakati as we reserve our right to push.
Au nasema uongo ndugu zangu?