Madhara ya Awamu ya Tano yanayofumbiwa Macho

Waumini waaminifu wa mwendazake kama alivyo SABAYA mnafanana kwa kila kitu.

Mnafikiri mna uelewa kumbe pumba tupu.
Pumba ni huu uzi mkuu. Awamu ya tano ni historia tayari. Wajanja wanaona mbali hawagandi jana huzipeleka akili zao kesho.
 
Pumba ni mawazo ya waumini wa mwendazake. Hawaamini awamu ile ndiyo imewatupa mkono. Hawaamini wamebakia wakiwa.

Wengi wao ni wapiga debe, vibaka, boda boda, machinga nk hasa hasa the brainwashed.

Upo kundi gani wewe hapo?
 
Pumba ni mawazo ya waumini wa mwendazake. Haamini awamu ile ndiyo imewatupa mkono.

Wengi wao ni wapiga debe, vibaka, boda boda, machinga nk.

Upo kundi gani wewe hapo?
Kundi la waliousoma uzi wako na kuona akili ni zile zile za kutafuta likes kwa kumponda mtu ambaye hawezi kujitetea.
 
Hahaahaaa! Kwamba options hukuziona kuleta zako? Hata computer ingekutaarifu - invalid option 😂😂😂😂😂!

Nyuzi za kutaka likes huzijui? Kuna za kula mananihii kimaskhara, likes huko za kumwaga.

Wapi kapondwa asiyeweza kujitetea? Hukuona lolote kuhusu ilichorithi awamu ya sita tokea awamu iliyopita?

Awamu iliyopita haikuitwa ya wanyonge? Wanyonge hawakutanabaishwa kuwa ni wapiga debe, boda boda, machinga, sungu sungu, mama lishe na wa namna hiyo?

Awamu iliyopita haikuwaaminisha watu mengi, baadhi yakiwamo ya kupiga nyungu, michai chai, malimao, nk katika kutibu Corona; wau mini wakuu wakiwa wanyonge hao?

Wanyonge hao hawakuaminishwa kuwa ugonjwa huu haupo bali ni vita vya kiuchumi?

Wanyonge hao hawakuaminishwa kuwa chanjo hii ni sumu ya kuwamaliza?

Kipi kimelenga kumponda mwendazake hapo?

Nisiache kukumbusha kwani ungali hujajibu. Kati ya wanyonge hao wewe ni kundi lipi?
 
Bandiko hili ni bora kabisa

Huu ndiyo ulio ukweli mchungu. Hata hao unaowaona humu JF na mafikara duni duni, ni mlolongo huo huo wa the brainwashed boda boda, wapiga debe, vibaka vibaka, sungu sungu na wa namna hiyo.

Inataka ujinga wa kutosha kuweza kujazwa ujinga wa kwenda kupiga nyungu na kuwabeza wataalamu wakiwamo wabobezi wa afya kwenye maeneo yao.
 
Mkuu kwani unadhani ile misungu sungu, boda boda, mipiga debe nk humu haipo?

Hilo jamaa ni moja ya hiyo mijamaa. Mijinga iliyo brainwashed. Haijui inataka nini au haitaki nini. Mama Samia ana kazi kubwa sana ya kuya accommodate pia haya.
una udhaifu mmoja mkubwa sana.

kujiona una akili kuzidi kundi fulani la watu.
hili ni tatizo la kisaikolojia ambalo madhara yake ni haya ambayo yanaonekana kwako.

1,kumfokea au kutukana kila aliye kinyume na mtazamo wako.

2,kuwa na dharau kwa kila mwenye mtizamo tofauti na wako.

3,kukosa adabu kwa watu wazima ambao ni viongozi inaonekana hata kwa wazee mtaani kwako hali ni hiyo.

haya yote yatakwisha siku utakapopata kipato cha uhakika kitakachoendana na kiwango cha elimu ulichonacho.vinginevyo hautakuja kupona.

tukirudi katika mada yako,magufuli hakuroga,wala kuchafua akili za watu.ndio maana hata mama unayetaka afanye jambo,kuna wakati anasahau barakoa ambayo anajua yeye anaivaa kwa lengo gani.yeye aliwekea tamko hali halisi iliyoko mtaani.unajua UG ina scandle ya kuzika majeneza tupu ili kukuza namba ya vifo vya hao wagonjwa wa covid!!!au huna taarifa?

itakuwa ngumu kuwashawishi watz kwamba mtaani kuna corona,si kwa sababu magufuli amesema(maana hayupo hata hivyo)bali sababu ni kwamba wanaona hakuna corona mtaani.
chanjo ilitangazwa kuagiza,sijui maendeleo ya UDUNGWAJI yamefikia wapi.
 
Hahaahaaa! Kwamba options hukuziona kuleta zako? Hata computer ingekutaarifu - invalid option 😂😂😂😂😂!

Nyuzi za kutaka likes huzijui? Kuna za kula mananihii kimaskhara, likes huko za kumwaga.

Wapi kapondwa asiyeweza kujitetea? Hukuona lolote kuhusu ilichorithi awamu ya sita tokea awamu iliyopita?

Awamu iliyopita haikuitwa ya wanyonge? Wanyonge hawakutanabaishwa kuwa ni wapiga debe, boda boda, machinga, sungu sungu, mama lishe na wa namna hiyo?

Awamu iliyopita haikuwaaminisha watu mengi, baadhi yakiwamo ya kupiga nyungu, michai chai, malimao, nk katika kutibu Corona; wau mini wakuu wakiwa wanyonge hao?

Wanyonge hao hawakuaminishwa kuwa ugonjwa huu haupo bali ni vita vya kiuchumi?

Wanyonge hao hawakuaminishwa kuwa chanjo hii ni sumu ya kuwamaliza?

Kipi kimelenga kumponda mwendazake hapo?

Nisiache kukumbusha kwani ungali hujajibu. Kati ya wanyonge hao wewe ni kundi lipi?
Mkuu Awamu ile imeweka rada nne zinazoimulika Tanzania nzima na zinakwenda kuongeza pato la taifa hii corona ikipungua makali.

Awamu ile imesomesha vijana zaidi ya 120 wanaoingia moja kwa moja kufanya kazi za uendeshaji wa shirika la reli Tanzania, ni Awamu iliyofufua usafiri huo baada ya miaka 25.

Ni Awamu iliyofufua usafiri wa maziwa yote, ni Awamu iliyojenga viwanda vya kuchakata dhahabu humu humu nchini.

Ukiwa mpiga soga wa mtandaoni huwezi kuielewa Awamu ile lakini ukiwa mtu mwenye mtazamo chanya wa kujadili masuala muhimu ya kitaifa hutaweza kufikiria kuendeleza roho za nongwa.
 
Mabibi na mabwana awamu ya tano imepita na sasa kazi inaendelea katika awamu ya sita chini ya Rais Samia.

Kwamba tupo awamu ya sita itakuwa kutojitendea haki mno kutoyaangazia kabisa madhara ya awamu ya tano kwa awamu ya sita yote chanya na hasi.

Kwa uzi huu itoshe kuyaangazia madhara hasi ya awamu ya tano kwa awamu ya sita.

Haikuwa ajali kwa awamu ya tano kujikita katika kujitanabaisha kwa nguvu zote kuwa ilikuwa ni ya wanyonge. Yaani wapiga debe, machinga, mama lishe, bodaboda na wa namna hiyo. Makundi haya yatoshe kuwakilisha aina ya philosophy iliyokuwa ikizisukuma agenda za serikali ya awamu ya tano.

Aina ya mafikara ya watu hao ndiyo yaliyokuwa yakiichezesha ngoma yote ya kiutawala tokea juu hadi chini. Ndiyo maana hadi leo, hata bungeni kunasikika wazi wazi sauti zenye kuhimiza kutambuliwa ubora wa wahitimu wa darasa la saba dhidi ya maprofesa au wasomi kwa ujumla.

Imani potofu zilizoambatanishwa na Corona zikiwamo upigaji nyungu, maombi, michai chai, malimao nk ni mwendelezo wa mafikara au philosophy ya watu wa makundi hayo.

Kwenye awamu ile, upepo wa mafanikio serikalini ulilihitaji zaidi kundi hilo la wasioelimika. Watendaji wakiwamo Mawaziri na wote wenye njaa zao walilazimika kuukana ukweli na hata kuzikana taaluma zao ili kuweza kukubalika kundini.

Ya akina Gambo leo na wote wanaoitisha kutolaumiwa kama wao binafsi, bali hali nzima ya utawala iliyokuwapo wakati huo ni mwendelezo wa matokeo hayo hayo.

Tulipo leo chanjo ya UVIKO ipo njiani kuja. Bila shaka jambo hili ni la kheri kabisa. Lakini si ajabu kuwa hii nalo litakutana sasa na kundi lile lililokuwa limeaminishwa kuwa ugonjwa haupo, bali ni vita vya kiuchumi tu dhidi ya Tanzania. Tena kuwa chanjo ni biashara na zaidi sana ni sumu dhidi ya Waafrika na hasa Watanzania.

Siyo siri tuko pabaya sana bila ya kuyashughulikia madhara haya yaliyopandikizwa kutokea awamu ya tano wakati ilipokuwa katika kujitafutia uhalali wa kuwepo kwake.

Matatizo tuliyo nayo kuhusiana na kundi hili yanapaswa kufahamika ili kuweza kupatiwa ufumbuzi kamili. Hii ikiwa ni wa muda mfupi na hatimaye wa kudumu.

Kuuishi ukweli na haki hata kama kwa kufanya hivyo pana machungu yake ni mambo yasiyoepukika.

Awamu ya sita imerithi kundi kubwa la wajinga na "the brainwashed to be catered for." Lenye mtizamo hasi katika elimu, sayansi na teknolojia. Kunatakikana jitihada kubwa za dhati na za pamoja katika kuyaweka mambo sawa.

Ni vizuri kufahamu kuwa tuna kundi kubwa la watu wasiojua nini wanataka au nini hawataki. Hii ikiwa ni kwa sababu tu ya kukosa elimu kulikokolezwa vilivyo na kupotoshwa kulikofanyika kwa makusudi.

Ya DC na DED Morogoro ni mwendelezo wa yatokanayo na mitizamo ya kundi hili ambayo hayajapatiwa suluhisho.

Kwa pamoja tunaweza kuyaweka mambo sawa hatimaye. Hata hivyo si haba kutambua kuwa pana mlima mkali kweli kweli wa kupanda.

Penye nia pana njia.

Ninawasilisha.
Wala sijasoma maana ni muendelezo wa kumchafua mpendwa wetu magufuli. Nyie bakini na vidonda na ufisadi wenu. Na bado mtakua dissapointed maana kwa akili yenu samia amekuja kuwarejeshea nafasi yenu kama wahujumu wa maendeleo ya umma. Ngoja tuone maana hata magufulists hawana confidence na samia kwa sasa.
 
Kwamba huwa husomi ila unatoa maoni? Hahaahaaa haa 😂😂😂😂😂😂! Kwamba?

"Ngoja tuone maana hata magufulists hawana confidence na samia kwa sasa."

Endeleeni kuwa na confidence na huyo bwana, atawavusha.
 
Mkuu Awamu ile imeweka rada nne zinazoimulika Tanzania nzima na zinakwenda kuongeza pato la taifa hii corona ikipungua makali.

Awamu ile imesomesha vijana zaidi ya 120 wanaoingia moja kwa moja kufanya kazi za uendeshaji wa shirika la reli Tanzania, ni Awamu iliyofufua usafiri huo baada ya miaka 25.

Ni Awamu iliyofufua usafiri wa maziwa yote, ni Awamu iliyojenga viwanda vya kuchakata dhahabu humu humu nchini.

Ukiwa mpiga soga wa mtandaoni huwezi kuielewa Awamu ile lakini ukiwa mtu mwenye mtazamo chanya wa kujadili masuala muhimu ya kitaifa hutaweza kufikiria kuendeleza roho za nongwa.

Mkuu umeandika madhara chanya ya awamu ya tano?

IMG_20210617_232107_602.jpg

Hukuona kuwa uzi ulitambua uwepo madhara yote chanya na hasi? Kwamba uzi huu ulijikita kwa yaliyokuwa hasi, ilielezwa wazi kuwa ungeweza kujikita kwa yaliyo chanya na kuyaacha hasi, kwa uzi mwingine! Kwamba huu ulijikita kwa yaliyo hasi, kwa nini wewe usianzishe uzi wako wa yaliyo chanya?

Au ulichotaka ni kunichagulia ni madhara yapi tu niyaangazie?

Kumbuka hadi sasa umeshindwa kuunga mkono au kukanusha hata jambo moja katika niliyoyaandika. Kwa maana nyingine hadi sasa umekuwa ukiandika utopolo mtupu.

Kwa kujifanya kukomaa nje ya mada huna kundi kweri linalokuhusu kama ilivyo kwenye huu uzi hapo chini japo wengine wamesingiziwa humo?

Haya ndio ya makundi ya watu wa JF na tabia zao

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mabibi na mabwana awamu ya tano imepita na sasa kazi inaendelea katika awamu ya sita chini ya Rais Samia.

Kwamba tupo awamu ya sita itakuwa kutojitendea haki mno kutoyaangazia kabisa madhara ya awamu ya tano kwa awamu ya sita yote chanya na hasi.

Kwa uzi huu itoshe kuyaangazia madhara hasi ya awamu ya tano kwa awamu ya sita.

Haikuwa ajali kwa awamu ya tano kujikita katika kujitanabaisha kwa nguvu zote kuwa ilikuwa ni ya wanyonge. Yaani wapiga debe, machinga, mama lishe, bodaboda na wa namna hiyo. Makundi haya yatoshe kuwakilisha aina ya philosophy iliyokuwa ikizisukuma agenda za serikali ya awamu ya tano.

Aina ya mafikara ya watu hao ndiyo yaliyokuwa yakiichezesha ngoma yote ya kiutawala tokea juu hadi chini. Ndiyo maana hadi leo, hata bungeni kunasikika wazi wazi sauti zenye kuhimiza kutambuliwa ubora wa wahitimu wa darasa la saba dhidi ya maprofesa au wasomi kwa ujumla.

Imani potofu zilizoambatanishwa na Corona zikiwamo upigaji nyungu, maombi, michai chai, malimao nk ni mwendelezo wa mafikara au philosophy ya watu wa makundi hayo.

Kwenye awamu ile, upepo wa mafanikio serikalini ulilihitaji zaidi kundi hilo la wasioelimika. Watendaji wakiwamo Mawaziri na wote wenye njaa zao walilazimika kuukana ukweli na hata kuzikana taaluma zao ili kuweza kukubalika kundini.

Ya akina Gambo leo na wote wanaoitisha kutolaumiwa kama wao binafsi, bali hali nzima ya utawala iliyokuwapo wakati huo ni mwendelezo wa matokeo hayo hayo.

Tulipo leo chanjo ya UVIKO ipo njiani kuja. Bila shaka jambo hili ni la kheri kabisa. Lakini si ajabu kuwa hii nalo litakutana sasa na kundi lile lililokuwa limeaminishwa kuwa ugonjwa haupo, bali ni vita vya kiuchumi tu dhidi ya Tanzania. Tena kuwa chanjo ni biashara na zaidi sana ni sumu dhidi ya Waafrika na hasa Watanzania.

Siyo siri tuko pabaya sana bila ya kuyashughulikia madhara haya yaliyopandikizwa kutokea awamu ya tano wakati ilipokuwa katika kujitafutia uhalali wa kuwepo kwake.

Matatizo tuliyo nayo kuhusiana na kundi hili yanapaswa kufahamika ili kuweza kupatiwa ufumbuzi kamili. Hii ikiwa ni wa muda mfupi na hatimaye wa kudumu.

Kuuishi ukweli na haki hata kama kwa kufanya hivyo pana machungu yake ni mambo yasiyoepukika.

Awamu ya sita imerithi kundi kubwa la wajinga na "the brainwashed to be catered for." Lenye mtizamo hasi katika elimu, sayansi na teknolojia. Kunatakikana jitihada kubwa za dhati na za pamoja katika kuyaweka mambo sawa.

Ni vizuri kufahamu kuwa tuna kundi kubwa la watu wasiojua nini wanataka au nini hawataki. Hii ikiwa ni kwa sababu tu ya kukosa elimu kulikokolezwa vilivyo na kupotoshwa kulikofanyika kwa makusudi.

Ya DC na DED Morogoro ni mwendelezo wa yatokanayo na mitizamo ya kundi hili ambayo hayajapatiwa suluhisho.

Kwa pamoja tunaweza kuyaweka mambo sawa hatimaye. Hata hivyo si haba kutambua kuwa pana mlima mkali kweli kweli wa kupanda.

Penye nia pana njia.

Ninawasilisha.
Are you terming the citizens with challenging views that they are ignorant? Pardon, are you, aliens, boasting yourself as intelligent and brainstorm cultivated?

Hii sentensi yako itakugharimu wewe na wafuasi wako

Nukuu: "Awamu ya sita imerithi kundi kubwa la wajinga na "the brainwashed to be catered for." Lenye mtizamo hasi katika elimu, sayansi na teknolojia. Kunatakikana jitihada kubwa za dhati na za pamoja katika kuyaweka mambo sawa"
 
People in self-denial aren't people with challenging views.

IMG_20210718_063455_991.jpg

Accordingly and rightly so, I called them by their actual names. A spade is not a big spoon.

Weren't these people fighting Covid-19 not both ignorant and brainwashed?

IMG_20210614_192655_399.jpg

Was this not part of that calculated brainwashing?

IMG_20210806_053407_437.jpg

How about what you see here?

IMG_20210725_012351_122.jpg

Don't threaten me. Don't threaten us. Don't threaten any of whom you call my followers.

Should it be that you were part of it:

"rest assured, we hold all of you responsible for all the deaths and consequences resulting out of your ill motives of concealing facts that you well knew on this pandemic."

#COVID19 - Chanjo: Wanaopotosha Kuwajibishwa kwa Vifo wanavyoendelea Kusababisha

Habari yenyewe ndiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom