Haya ndio madhara ya kiuchumi ya gonjwa hili ambapo sasa kuna chuo kikuu kimoja cha binafsi kimewapa watumishi wake likizo ya dharura kuanzia tarehe ya leo na kutangaza kuwalipa nusu mshahara wafanyakazi wake mwezi huu wa April kutokana na akiba ya ndani chuo husika waliyonayo.
Vile vile, kwa mujibu wa nyaraka ya siri ya chuo hicho kwa wafanyakazi wake,chuo kinakusudia kuomba mabenki yasitishe makato ya mikopo kwa watumishi wenye mikopo katika kipindi hiki kigumu.
Chuo pia kimetangaza kufunga shughuli zake zote isipokuwa zile za dharura tu.
My take:
Hapa ndipo umuhimu wa hoja za wabunge wa upinzani kutaka kujadili Bungeni madhara ya kiuchumi ya huu ugonjwa unaponza kuonekana na kwa hakika huko mbeleni umuhimu huu utajitokeza zaidi katika maeneo mengi na hata serikali yenyewe ni wazi itaguswa tu.
Time will tell.