Madhara ya dhambi ya uzinzi

Madhara ya dhambi ya uzinzi

Ninayo mengi juu ya suala la uzinzi Ila maarifa haya hayatowafaa ikiwa hamna Kristo Yesu ndani yenu. Mnajua ni kwa nini Bwana Yesu akiwauliza wale jamaa waliomleta Mwanamke mzinifu kwake kuwa yu wapi mwanamume aliyezini naye?. Bali aliwasambalatisha kwa swali?.
Eleza kwa kirefu

Dhambi ya uzinzi inahesabika pale mtu alipolala na mke wa mtu na sio vinginevyo. Ikimaanisha kuwa adhabu ilitolewa kwa mke aliyechepuka na kama angekamatwa na mwanamume huyo wangeuwawa wote wawili. Ila kwa mwanamume kutembea na binti hata kama ameoa sheria haiwi uzinzi hivyo ni kusema aliyefungwa ni mke aliyeolewa huyu hapaswi kuingiliwa kamwe na ukimwingilia ndipo Methali inakuita wewe ( mwanamume) mjinga usiye na akili kwa ni ni? Maana umekosa wanawake mpaka ukaenda kujitia unajisi kwenye shahawa za mwanamume mwenzako?. Inaendelea kusema.....
Mithali 6
33. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;
Wala fedheha yake haitafutika.
34. Maana wivu ni ghadhabu ya mtu;
Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi.
35. Hatakubali ukombozi uwao wote;
Wala hatakuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi.
Yaani hata kufirwa inakuwa haki yako ukiingilia mke wa mtu.

Ila kuhusiana na mwanamwali ukimuingilia ukadakwa waweza toa mahari akawa mkeo au ikiwa baba mzazi haridhii umuoe itatoa mahari kisha ataenda zake. Hii ni kibiblia kabisa
Una hoja

Kumbe

Vipi sadaka za mtu alie zaliwa kwa hicho mnachokiita uzinzi mnachukua?
Non sense Questions...
Kuzaliwa uzinzin ni kosa la Alie zaliwa au alie zalisha na kuzalishwa.??
Ni kwa vip Sadaka yake isikubalike kwa kosa ambalo akulifanya yeye..??

asante kwa swali zuri nitakuelezea kwa msaada wa MUNGU
Mungu alipomuumba adamu na Hawa ,alimpa mamlaka ya kutawala , kuongezeka na kukua zaidi,
na huu ndo ulikuwa urithi wa vizazi vyote, inamaana binadamu alikuwa na acess ya moja kwa moja na Mungu, dhambi ilipoingia kupitia wazazi wetu wa mwanzo, ile nguvu ambayo walipewa iliisha au ilipotea, Mungu aliahidi au aliweka agano kuwa ile nguvu ya kutiisha, utawala na mamlaka angeirejesha kwa wanadamu, kumbuka kila binadamu anayezaliwa anazaliwa chini ya laana, hivyo Mungu alimtoa mwana wa pekee ambaye ni YESU( Hii ndo Neema ) ili aje aishi maisha ya duniani, kwa mfano wa mwa ,mwandamu, ili kila binadamu amwamini YEYE ili kurejesha nguvu ya asili ambayo tuliporwa na shetani, hivyo ukimwamini Yesu umeyapata yote
Samahani mtumishi nje ya mada kdoogo,,,,inatakiwa tubatizwe kwa maji kidogo au mengi?,na tukiwa wakubwa au wadogo?,au muhimu ubatizwe tu?.

Non sense Questions...
Kuzaliwa uzinzin ni kosa la Alie zaliwa au alie zalisha na kuzalishwa.??
Ni kwa vip Sadaka yake isikubalike kwa kosa ambalo akulifanya yeye..??
Hakukua na sababu ya kujibu kama ni non sense questions. Nyie sio ndio mnasema kupata watoto ni mapenzi ya Mungu kosa lipo wapi huyo Mungu akitengeneza hao watoto kwa njia ya uzinzi?

1. Huangamiza nafsi.
"Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake." (Mithali 6:32)

Mtu hufa kiroho, kama ilivyo dhambi yoyote ile humuondoa mtu katika uwepo wa Mungu, na pia huondoa uwepo wa Mungu
kwa mtu na hicho ndicho kifo cha kiroho.

2. Huondoa ufahamu wa mwanadamu.
"Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu." (Hosea 4:11)
Mtu anakuwa hana uwezo wa kuwa na ufahamu wa mambo mema ya kumpendeza Mungu, maana anakuwa hawezi kulitafakari Neno la Mungu, kila
wakati anakuwa anatafakari uzinzi tu.

3. Huchafua hekalu la Roho Mtakatifu.
"Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe." (1Wakorintho 6:18)
a) Uzinzi unahusisha viungo vya mwili, hivyo dhambi ya uzinzi inahusisha mwili moja kwa moja na ambalo ni hekalu la Roho Mtakatifu, (1Wakorintho 6:19)
Na Mungu anasema atamuharibu anayeliharibu au kulichafua hekalu la Roho Mtakatifu, (1Wakorintho 3:17)
b) Pia mwili ni kiungo cha Kristo,
"Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!" (1Wakorintho 6:15)
Swali la kujiuliza ni hili, Kama miili yetu ni viungo vya Kristo, Je, Yesu Kristo atakubali kuuwa na kiungo kichafu? Jibu ni hapana bali atakiondoa na kukitupilia mbali hadi kitakaposafishwa, mtu asipoomba toba ni lazima ataangamia kabisa maana anasema
tawi lisilozaa atalikata na kulitupa katika moto, (Yohana 15:6)

4. Humuunganisha mtu na madhabahu, miungu na ibada za mtu aliyezini naye, ukoo, kabila, nk.
"Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.”
(1Wakorintho 6:16)

Inawezekana kwa macho ya kawaida mtu asione, bali kiroho anakuwa ameshahama katika uwepo wa Mungu na kuungamanishwa na miungu ya yule mtu aliyezini naye, maana tayari wanakuwa mwili mmoja.

Anakuwa hana uwezo wa kumwabudu Mungu wa kweli, hata akiwepo
ibadani anakuwa hawezi kuunganishwa na Mungu kiroho, maana anakuwa tayari ana ibada za kishetani.

Kwa ujumla dhambi ya uzinzi kama zilivyo dhambi nyingine zote humuondoa mtu katika uwepo wa Mungu.
Hivyo tunapaswa kuepuka sana dhambi hii pamoja na dhambi zote ili Mungu asituache, maana Mungu akituacha shetani anachukua nafasi na kuanza kutuendesha.

Omba toba, tubia dhambi zote pamoja na uovu wote, naye Mungu atakusamehe maana anasema atazisafisha dhambi zetu zote,
(Isaya 1:18)Mungu akubariki sana! Mungu atusaidie tukae kwenye kusudi lake🤝🙏
Ubarikiwe sana...

Back
Top Bottom