Madhara ya kupanda bei kiholela kwenye uchumi na namna mfumo wa kiutawala wa Tanzania unavochangia uwepo wa hili tatizo

Madhara ya kupanda bei kiholela kwenye uchumi na namna mfumo wa kiutawala wa Tanzania unavochangia uwepo wa hili tatizo

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Wasalaam Wanazengo,

Kwenye uchumi kuna concept huwa tunaiita kwa kiingereza ‘Demand destruction’ ambapo hii huwa hutokea pale ambapo mlaji au consumer anapungukiwa nguvu ya kuweza kufanya manunuzi ya biadhaa au huduma zinazotengenezwa kwenye uchumi kwa sababu aidha, bei za bidhaa hizo ni kubwa ama zimepanda kwa kiasi kikubwa kushinda uwezo wa kipato cha mnunuzi.

Chukulia huu mfano hapa chini, huu ni utafiti hai nilioufanya kwa takribani watu watatu tofauti ambao wana kipato cha wastani wa mshahara wa milioni 1 kwa mwezi au shilingi 33,333 kwa siku na ambao wanafamilia ya watoto wawili na mke mmoja. Kulingana na utafiti wangu, suala la bei kupanda kwa haraka ndani ya miezi 12 iliyopita, kumesababisha kuongozeka kwa matumizi katika wakati wa sasa ukilinganisha na wakati uliopita. Ukichukulia ya kwamba, kipato ama mshahara bado hakijaongezeka, kuongozeka kwa matumizi maana yake kunapunguza kipato ambacho huwa kinawekwa kama akiba kitu ambacho huwa kina madhara makubwa kwenye mfumo wa uchumi.

Household ya Mr. XYZ

mr. XYZ.png


Ukiisoma vizuri hiyo chart hapo juu, utaona ya kwamba hii household ya Mr. XYZ mwaka jana, ilikuwa na uwezo wa kufanya matumizi na kuitosheleza familia yake na hapo hapo aliweza kubakiwa na akiba (savings) ya kiasi cha shilling 3,163,680 kwa mwaka mmoja.

Kiuchumi, savings au akiba ina maana kubwa sana na ndio haswa kichocheo cha ukuaji wa uchumi wowote ule duniani, kuanzia kwenye level ya wananchi. Kwasababu Mr. XYZ akishakuwa na akiba ya shilingi 3,163,680 maana yake atakuwa na uwezo wa kuanza ujenzi wa nyumba yake, au anunue usafiri, au afungue biashara kwa ajili ya mke wake, au ampeleke mtoto wake shule bora zaidi, au alime shamba kijijini kwao, au aende kufanya utalii kwenye mbuga za Serengeti, au akanunue picha za ukutani, au anunue makochi mapya, au anunue TV, au akajiendeleze kielimu etc etc.. kwahiyo hapo hizo shughuli zote huwa zinakuwa zinaleta matokeo chanya kwenye uchumi na zinachangia kuongeza mzuko wa pesa na pia ndio chachu ya kukuza uchumi wa nchi.

Lakini ukiangalia upande wa pili wa chart, baada ya bei kupanda na kipato chake kipo vile vile, ina maana huyu Mr. XYZ ili kuweza kuhudumia familia yake kama ilivokuwa awali bila kuathiri consumption bundle per day, itambidi aongeze matumizi kwa sababu ya bei kupanda. Kitendo cha bei kupanda ndicho haswa kitasababisha kuanguka kwa uwezo wa huyu mtu kujiwekea akiba (Decline in savings) ambacho ndicho kitu kinachosababisha hiyo niliyoiita ‘Demand destruction.

Ukiangalia, baada ya bei kupanda huyu bwana Mr. XYZ atakuwa na uwezo wa kuweka akiba ya shilingi 155,880 tu kwa mwaka ikiwa ni karibu anguko la asilimia 95 kutoka kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Sasa ukiangalia kiuchumi, hii akiba ya 155,880 labda sana sana itamuwezesha huyu mtu kununua simu moja kama zawadi kwa mkewe na kutulia zake kimya. Maana yake ni kwamba zile fujo alizokuwa anaweza kufanya wakati kipato kipo shilingi 3,163,680 zitakuwa haziwezekani tena kufanyika. Na maana yake ni kwamba zile biashara ambazo zilifaidika kwa kipato chake kuwa shilingi 3,163,680 hazitaweza kunufaika tena kwa sababu huyu mtu mfukoni hana kitu.

Maana yake pia tegemea kuona biashara nyingi zikipoteza mapato kwa miezi 12 ijayo kwa sababu mifuko ya watu wa aina ya Mr. XYZ itakuwa haimudu kufanya matumizi tena kwa sababu savings au hazina zao hazitoshi mfukoni. Na hichi kitu ndiyo hatari kubwa nnayoiona inaenda kutokea Tanzania. Mdororo mdogo wa uchumi ambao utasababisha na bei kupanda kwa haraka.

Sasa kiuchumi, hii demand destruction pia ni lazima itakuwa na athari kwenye sekta zote za uchumi wa nchi, maana yake, watu wanavopunguza kununua mahitaji kwasababu ya mifuko kuwa mitupu, kuna baadhi ya biashara pia zitaanza kudorora kwa sababu zitakuwa hazipati wateja wa kutosha. Taasisi za kifedha pia ni lazima zinaweza kujikuta kwenye misukosuko maana ikiwa watu hawana savings ina maana na wao deposits pia zitapungua kwenye mabenkin na pia hata utoaji wa mikopo utapungua. Kiufupi, ‘hakuna hatari mbaya kwenye uchumi kama upandaji wa vitu bei kiholela’

Serikali ya Tanzania haiwezi kukwepa lawama ya kinachotokea kwa sasa. “Nchi isiyokuwa na ukomo wa matumizi wala utambuzi kwamba matumizi makubwa ni tatizo kwenye uchumi haitafanikiwa lolote kwenye kuinua uchumi”


Mfumo mzima wa hii nchi umeoza, na kadri mda unavozidi kwenda kuna mambo yatazidi kuibuka moja baada ya lingine ambayo yatakuwa yanadidimiza uchumi wetu na watu wakiendelea kudhani ya kwamba yanasababishwa na mtu mmoja mmoja na kuacha kuongea kuhusu mfumo uliopo ambao hautakaa uwe rafiki kwa maendeleo ya hii nchi milele.

Fikiria haya mambo yafuatayo na kuna mengine mengi sana yapo kwenye nchi yetu

  • Tanzania ina wabunge karibu 390 ambao wametokana na uchaguzi ulioibwa. Ukiangalia payroll ya hawa watu wanaojiita wabunge ambao mimi binafsi naona ni wengi wanalipwa karibu Bilioni 100 kwa mwaka kama mshahara ukiondoa marupurupu. Ukiweka marupurupu unaweza kuongelea kitu kama Bilioni 150 kila mwaka kwa wabunge.
  • Nchi ina mawaziri na manaibu mawaziri wa kutosha --- bajeti zao za kutisha
  • Nchi ina wakuu wa mikoa, wilaya, DED wakutosha --- wana bajeti za kutisha
Hawa watu binafsi sijawahi kuona michango yao kwenye hii nchi, zaidi imekuwa ni chaos kila mahali.

Kwa ufupi mfumo uliopo Tanzania, ni kama mtu mwenye kitambi kikubwa sana ambae huwa muda wote anahitaji kula. Maana yake ni kwamba, mtu wa aina hii kwake kupata chakula ni suala la kipaumbele kuliko kitu chochote kile. Ndo mana watu utawasikia kila kona wananuambia, mafuta ukiyafikisha bandari ya Dar es salaama gharama yake ni sh 1,700 kwa lita lakini ni vipi bei iende mpaka 3200? Ni kwanini serikali isisamehe tu kodi?

Serikali ya Tanzania haina uwezo wa kusamehe kodi wala kufuta kodi, sio kwamba hawataki, ni kwasababu kuna mfumo tayari una exist kwenye nchi ambao unafanya serikali iwe ina uhitaji mkubwa wa pesa kama kipaumbele kuliko kuangalia mahitaji ya wananchi. Kwahiyo solution huwa mara nyingi, ni kutoza kodi zaidi ili serikali iweze kuhudumia mfumo uliopo wa matumizi yasiyo na ukomo.

Ndo mana unaona tu wabunge na mawaziri hawaji na solution yeyote kwenye hizi mifumuko za bei ambazo nyuma yake zinatokana na matokeo ya kodi za serikali, kwasababu wanajua ya kwamba solution ya kweli kuvunja huu mfomo wa utawala uliopo.

Lakini kwa sababu, kwa mazingira ya sasa na mwelekeo ulivo, huu mfumo uliopo nauona ukiendelea kuishi kwa mda mrefu zaidi na utazidi kuwa na matokeo yasiyopendeza kwenye masuala mazima ya kiuchumi. Naona mambo yanayotokea sasa hivi bado yatazidi kutokea pia kwa kipindi kirefu zaidi kijacho, mpaka pale watapopatikana watu wenye utashi wa ku correct huu mfumo uliopo.

The problem is not Samia, wala usifikiri the solution was Magufuli. These are just there to reinforce the already existing system kwa minajili hiyo hakuna mwenye tofauti na mwenzake kama unataka kujaribu kufannaisha ufanisi wao. Na hakuna guarantee kwamba angekuwepo Magufuli hii tozo ya mafuta ingefutwa.

Solution ya mwisho ni kubadili mfumo, na kubadilisha mfumo lazima kuwe na policy disruptions ambazo bado sioni dalili kama hicho kitu kitawezekana kwa sasa Tanzania ukiangalia pia mazingira ya siasa yalivo.

Kwa maana hiyo, wacha tuendele kuwa watazamaji wa haya masuala yanavokwenda.

Wasalaaam!

N.Mushi
 
Tumepigwa na kitu kizito sana chenye ncha kali kichwani..
 
Back
Top Bottom