Madhara ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango huku wanawake wakisahau njia bora ya kupanga uzazi ni kutumia kondom na kalenda tu

Kizuio

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
845
Reaction score
521
MADHARA YA KUTUMIA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO

Serikali huwa haiwaambii ukweli wanawake hasa pale matangazo kuhusu uzazi wa mpango yanaposhika kasi kwenye Tv na Radio

Ili kuepuka kupata ujauzito, wanawake hutumia njia mbalimbali za kupanga uzazi wao ikiwa ni pamoja na utumiaji wa vidonge, vitanzi, vijiti na wengine wachache hutumia mipira wakati wa tendo la ndoa.

Njia hizi kila moja ina athari chanya na hasi na mara nyingi hutegemea na hali ya mtu anayezitumia kwani akitumia mmoja anaweza kuona madhara kadhaa lakini mwingine asione.

Katika kuchambua madharaya ya njia hizi za kupanga uzazi, tutaelezea madhara ya matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi kwa wanawake.

Kupata kichefuchefu.

Mtumiaji anayetumia dawa hizi kwa mara ya kwanza ana uwezekano mkubwa wa kupatwa na kichefu chefu ambacho hudumu kwa muda mfupi hadi mwili utakapozoea dawa hizo. Ukitumia dawa hizi wakati wa chakula, au muda mfupi kabla ya kulala huenda ikakusaidia kupunguza hali hiyo.

Aidha, unashauriwa kuwa, endapo utaona hali hiyo imeendelea kwa muda mrefu, muone mtaalamu wa afya kwa ushauri zaidi.

Kuongeza hamu ya kula

Wakati mfumo wa homoni za oestrogen na progesterone unapobadilishwa kwa kutumia vidonge humfanya mtumiaji kuwa na njaa sana na hivyo kukufanya ule sana hali inayoweza kupelekea kuongezeka uzito. Lakini hakuna ushahidi madhubuti unaoonyesha uhusiano wa moja kwa moja kuwa dawa hizo zenyewe huongeza uzito.

Kubadilika kwa hisia (mood)

Wanawake ambao hukumbwa na matatizo ya kubalika kwa hali/hisia zao kama kuwa na hasira, kutotaka kusemeshwa, hali hiyo huongezeka pale anapotumia vidonge vya kupanga uzazi. Wanawake wa aina hii wanashauriwa kujadiliana na wenza wao kabla ya kuanza kutumia dawa hizi.

Maumivu ya kichwa

Mabadiliko ya homoni katika mwili wa mwanamke anayetumia vidonge hivi, hupelekea maumivu ya kichwa na kipandauso. Mabadiliko tofauti ya homoni hupelekea dalili tofauti tofauti za maumivu ya kichwa. Lakini maumivu na dalili hizo zitaendelea kupungua kadiri ya muda.

Kuganda wa damu

Mtumizi ya vidonge hivi wakati mwingine huwaweka wanawake katika hatari kubwa kutokana na kupelekea damu zao kuwa mabonge mabonge. Wanawake wenye matatizo haya ya damu kuwa mabonge wanashauriwa kutotumia dawa hizi kwani zitawasababishia madhara zaidi. Lakini pia kabla hujaanza kutumia dawa, unashauriwa kumuona mtaalamu wa afya.

Maziwa kuongezeka ukubwa

Vidonge hivi vinaweza kukusababishia maziwa yako kuongezeka ukubwa au kupata maumivu ya maziwa madhara ambayo yataanza kutoonekana baada ya kutumia dawa hizi kwa wiki kadhaa. Hata hivyo, kama utaona maziwa yako hayapo sawa, au maumivu yamedumu kwa muda mrefu, utahitaji kumuona mtaalamu wa afya haraka.

Kutokwa na uchafu ukeni

Baadhi ya wanawake hukumbwa na tatizo la mabadiliko ya utoaji uchafu ukeni hali ambayo huathiri kujamiiana kwao kutokana na kupungua au kuongezeka kwa muda na kiasi cha utoaji uchafu. Utoaji wa uchafu kwa njia ya uke si tatizo kwa wanawake, lakini kama utahisi kuna hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda hospitali.

Athari hizo za vidonge tulizozitaja hap juu sio zote ni mbaya. Madhara mengine kubwa za kutumia vidonge hivyo ni pamoja na kuumwa sana na kichwa, Maumivu ya nyonga, maumivu ya kifua, uono hafifu pamoja na maumivu ya miguu au mapaja.

Endapo moja ya haya madhara makubwa tuliyoyataja hapo yatatokea, unatakiwa kumuona daktari haraka ikiambatana na kusitisha matumizi ya videonge hivyo.

Maumivu hayo yanaweza kuashiria matatizo katika kibofu, ini, damu kuwa mabonge, shinikizo la damu au hata ugonjwa wa moyo.

Vijiti, vidonge, sindano kwa ajili ya uzazi wa mpango ni hatari kwa afya ya mwanamke

Mbaya zaidi hata wanaume wanaitwa huku wakiaaminisha watu njia ya hizo si kwa ajili ya wanawake tu
 
Ukienda clinic wanakushauri na kukupa side effects za Kila njia,
Kisha unachagua njia unayoona ni nafuu.
Kwa Sasa wanashauri zaidi kitanzi kwa kuwa kina madhara kidogo kulinganisha na mengineyo
 
Ukienda clinic wanakushauri na kukupa side effects za Kila njia,
Kisha unachagua njia unayoona ni nafuu.
Kwa Sasa wanashauri zaidi kitanzi kwa kuwa kina madhara kidogo kulinganisha na mengineyo
Mi nikija kutumia hizo mambo sidhani kama nitasubutu kitanzi naogopa
 
Ukienda clinic wanakushauri na kukupa side effects za Kila njia,
Kisha unachagua njia unayoona ni nafuu.
Kwa Sasa wanashauri zaidi kitanzi kwa kuwa kina madhara kidogo kulinganisha na mengineyo
Hakuna madhara kidogo siku zote hutaambiwa ukweli wa hivyo vitanzi
Hizo ni biashara za watu
Tumia kondom au fuata kalenda yako
 
Ni bora kutumia njia hizo kuliko kutoa mimba.
Na kitanzi naona ndio njia bora zaidi kwa sasa coz Haina vichocheo.
 
Hamu ya kula tutaongeza idadi ya mikate.

Kichwa kuuma tutanunua panadol.

Damu ikiganda tutatafuta vitamin k.

Kichefu chefu ndimu italambwa.

Maziwa kua makubwa am gon enjoy that.

Uchafu kutoka ukeni subirini uzi jf.
 
Ni bora kutumia njia hizo kuliko kutoa mimba.
Na kitanzi naona ndio njia bora zaidi kwa sasa coz Haina vichocheo.
Ndio maana wanaoruhusiwa kusex ni wanandoa sasa kwa kuwa sex Mpaka watoto wanasex basi tumia kondom au fuata kalenda
 
Hamu ya kula tutaongeza idadi ya mikate.

Kichwa kuuma tutanunua panadol.

Damu ikiganda tutatafuta vitamin k.

Kichefu chefu ndimu italambwa.

Maziwa kua makubwa am gon enjoy that.

Uchafu kutoka ukeni subirini uzi jf.
Hakuna msaada hapo zaid ni maumivu kwa wanawake tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…