Duh, hapo tena inabidi turudi darasa la kwanza tujifunze Kiswahili:
Kudharau na
kutokutii ni maneno yenye maana zinazokaribiana lakini maana hizo hazifanani:
- Kudharau ni hali ya kutoonyesha heshima au kutojali thamani ya kitu au mtu. Ni hali ya kuona jambo fulani au mtu sio wa maana au sio muhimu. Mfano: Anawadharau wazazi wake.
- Kutokutii ni hali ya kukosa kutii amri, maagizo, au sheria. Ni kufanya kinyume cha kile unachoamriwa au kuelezwa. Mfano: Mtoto alikataa kutii agizo la wazazi wake.
Mtu anaweza
kutokutii bila kudharau, yaani kama hatimizi maagizo lakini bado ana heshima kwa anayemwamuru. Vilevile, mtu anaweza
kudharau bila kutokutii, yaani, anaweza kutekeleza amri, maagizo, au sheria
sio kwa sababu anamheshimu aliyetoa maagizo, bali kwa sababu analazimika kufanya hivyo kwa sababu fulani, kama vile hofu ya adhabu, matarajio ya faida, au kushinikizwa na mazingira. Tuko pamoja?