Madhara ya Kuwadharau Watumishi wa Mungu

Mwampo naye yumo?
 
Ni lazima kuwadharau kwa kuwa wanawadanganya watu watoe sadaka ili wao washibishe matumbo yao. Tena wengine wanatumia nguvu za giza, kupata umati wa watu wanaokusikiliza ni lazima ushirikina utumike.
 
wacha watukanwe wengi wamekuwa matapeli
 
Ni lazima kuwadharau kwa kuwa wanawadanganya watu watoe sadaka ili wao washibishe matumbo yao. Tena wengine wanatumia nguvu za giza, kupata umati wa watu wanaokusikiliza ni lazima ushirikina utumike.
Kimaandiko, sio sahihi kumdharau mtu yeyote, hata Mtumishi wa Mungu anayeenda kinyume na mapenzi ya Mungu(Mithali 14:21).

Daudi hakumdharau Mfalme Sauli hata wakati Sauli alipokuwa amepotoka na kumfuatilia kwa uovu.
1 Samweli 24:6 SRUV
"Daudi akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA."

Mtume Paulo alipotambua Petro amekwenda kinyume na injili, hakumdharau bali alimkemea ana kwa ana (Wagalatia 2:11-14).

Maandiko hayo yanatufundisha kwamba kama Mtumishi wa Mungu anapotosha mafundisho au anaishi maisha yasiyompendeza Mungu, hatupaswi kumdharau bali tunapaswa kumuonya kwa staha, upendo na hekima ili kumrejesha kwenye njia sahihi.

Na kama ni Mtumishi wa Mungu mzee, yaani anayekuzidi umri, usimkemee bali umuonye kama baba (1 Timotheo 5:1-2).

Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu katika eneo hilo.
 
wacha watukanwe wengi wamekuwa matapeli
Usiwaunge mkono wanaowatukana. Kutukana ni dhambi.
Wakolosai 3:8
"Bali sasa yawekeni haya yote mbali nanyi, hasira, ghadhabu, uovu, matukano, matusi vinywani mwenu."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…