Madhara ya Marufuku Siasa kwa miaka 5 imesababisha CCM kukosa uvumilivu wa kisiasa

Madhara ya Marufuku Siasa kwa miaka 5 imesababisha CCM kukosa uvumilivu wa kisiasa

Uongozi wa Magufuli kwa ujumla wake umekuwa na faida ndogo sana ukilinganisha na hasara.

Watu wengi wanamshabikia kwa mambo yenye madhara makubwa kwa Taifa. Kuna siku watu watajuta kwa kukubali kuukumbatia ujinga. Hakuna kiongozi mbaya kabisa kuzidi yule asiyefuata katiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
15 August 2020
Moshi, Tanzania
Msafara wa Tundu Lissu Wavurugwa Mbele ya Polisi, David DJumbe asimulia


Asimulia hali halisi ilivyokuwa Boma ya Ngombe , Hai Kilimanjaro na walichoona
Source : swahili villa
 
16 August 2020

"YULE UNAYEMDHARAU NDIO ANAKUWA MSAADA WAKO, TUMUOMBE MUNGU" - PADRE
Tutendeane vizuri na tunapokwenda katika mchakato mzima wa kuelekea katika uchaguzi tumuombe Mungu tupate viongozi walio wazuri
 
16 August 2020

Sisi tunataka Rais wa Nchi tu | OCD, RPC dhibiti wote awe wa CCM, CHADEMA au CUF



Waziri wa Mambo ya ndani Mh. George Simbachawene amevitaka vyombo vya usalama kusimamia demokrasia ili kudhibiti vikundi vya watu wanaotaka kuzuia watu wasifanye shughuli za siasa na kampeni kipindi hiki cha mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020.
Source: EastAfricaRadio
 
15 Aug 2020
Dar es Salaam, Tanzania

SIRRO: TUTAFANYA HAYA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA



Jeshi la Polisi nchini limetaja hatua nne litakazochukua kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu ikiwamo kukutana na viongozi wa dini, maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na vyama vya siasa.

Pia, jeshi hilo limesema lipo tayari kuruhusu maandamano ya wafuasi wa chama chochote cha siasa endapo litajiridhisha na mazingira ya wakati huo.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Jeshi hilo nchini IGP Simon Sirro katika mahojiano na gazeti hili yaliyofanyika juzi ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Katika mahojiano hayo, Sirro aliulizwa jinsi polisi walivyojipanga kuelekea uchaguzi huo na masuala mengine ya kudhibiti matukio ya uhalifu.

Akijibu swali kuhusu walivyopjipanga, alisema miongoni mwa hatua watakazochukua ni kutoaji mafunzo ya uelewa wa sheria na kanuni za uchaguzi kwa maofisa wa jeshi hilo, mafunzo ya kuzuia na kukabiliana na makundi yatakayofanya uhalifu wakati wa uchaguzi na nne ni kutumia polisi jamii kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa amani kwenye uchaguzi huo.

Source : Mwananchi digital
 
14 August 2020
Hai, Kilimanjaro
Tanzania

Madhara ya Marufuku ya Siasa kwa miaka 5 imesababisha CCM kukosa uvumilivu wa kisiasa na kutishia machafuko nchini
Kufuatia kupigwa marufuku shughuli
za kisiasa Tanzania sasa tunaona madhara yake katika maeneo fulani. Na athari zake zimekuwa kubwa kabisa kwa upande wa CCM kwa wanachama, makada, wafuasi na wapenzi wake kukosa kufuata sheria, jadi , kawaida ya waTanzania kushindanisha hoja kwa kutumia ushawishi na kubaki na ulemavu wa kifikra kuamua kutumia nguvu na mabavu.

Video : Tukio la wanaCCM jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro
​


Shughuli za kisiasa zilitumika kutoa elimu ya kiuraia kuwajenga Watanzania kuamini katika kupiga kura ndiyo njia sahihi ya kumkataa mwanasiasa fulani baada ya kusikiliza hoja zake.

Lakini sasa tunaona baada ya viongozi wa juu wa nchi mwaka 2016 kuamua kuachana na haki hiyo ya msingi kabisa ya kikatiba kwa kupiga marufuku shughuli za kisiasa sasa baadhi ya waTanzania nao wameonesha wamekosa uvumilivu na kupoteza ufahamu kuwa huwezi kumpiga marufuku mwanasiasa fulani kufika eneo lako kisa mnatofautiana ktk mitizamo ya kiitikadi na mpo chama tofauti.

Tuliyoyaona kule wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ni matunda ya serikali ya CCM Mpya kupiga marufuku viongozi wa vyama vya upinzani kufika maeneo fulani kwa miaka 5 sasa, sababu watawala wa CCM wanadai mbunge wa chama fulani siyo eneo lake la kibunge au kuwa uchaguzi umeisha hivyo hakuna kuendelea kufanya siasa za hoja kujenga ushawishi.

Katiba ya nchi iliona mbali kuwa ruhusa ya kufanya siasa ni afya kwa utulivu wa nchi ili ikifikia kipindi cha kampeni waTanzania wasiwe wabaguzi wa kisiasa au kimaeneo bali wawe na ufahamu wa kufanya maamuzi kupitia sanduku la kura.

Tumeona wanaojiita wanaomtetea Magufuli kuwa hawataki kuona watu wengine wanafika maeneo yao kwa kuwa hawajawaona kufika huko kwao, bila kufahamu kuwa wanasiasa hao wa upinzani walipigwa marufuku.

Na kuthibitisha wanaigiza tabia za viongozi wa juu wa serikali ya CCM Mpya wamejaribu na wao kufanya jaribio la mwendelezo haramu wa marufuku kwa kufunga barabara, kufanya vurugu na kupandisha mabango ya shutuma kuwa wanasiasa wa vyama vingine ni mabeberu, vibaraka wa wazungu n.k

Hii siyo afya nzuri kwa siasa za Tanzania kwa wananchi kuacha kutumia sanduku la kura kufanya uamuzi na kuamua kutumia njia zingine sisizotambulika kupeleka ujumbe hawataki uchaguzi, wagombea wa vyama vingine na kampeni za kisiasa.

Kama nilivyojaribu kufafanua haya ndiyo matunda na matokeo ya kuminya siasa kufanyika, kuzuia midahalo, kuzuia kutoa maoni ktk vyombo vya habari, asasi za kiraia NGO, kuwaumiza wapinzani na sasa vikundi vya watu huko Hai Kilimanjaro wameamua kuiga vitendo vya serikali na watawala wa CCM Mpya kujichukulia sheria mikononi, kupuuza haki za mtanzania na mwanasiasa kujumuika na waTanzania wa mikoa, wilaya na majimbo mengine kufanya shughuli za kisiasa.

Hali hii isipodhibitiwa na serikali ya CCM nchi itakuwa haifuati utawala wa sheria na katiba kuanzia ngazi za viongozi waliopo ktk nafasi za uongozi wa dola na mpaka mitaani kama tulivyoona kwa baadhi ya wananchi wa wilaya ya Hai.

Nadhani hili tukio la watu kukosa uelewa wa haki za kiuraia za kwao na za wengine kufanya shughuli za kisiasa, wasomi na wazoefu kama Mzee Pius Msekwa wataona walikosea kuunga mkono kuzuia shughuli za kisiasa na kuwa ni hatari kwa usalama wa nchi pia kinyume na vile walivyofikiria wakati walipounga mkono marufuku ya kufanya siasa baada ya uchaguzi kuisha 2015.

Published on 10 Jul 2018
Video hii ikimuonesha mmojawapo wa thinktank ya CCM Mpya ikimuunga mkono Magufuli kupiga marufuku shughuli za kisiasa
Pius Msekwa: Hauoni kwamba kuzuia mikutano ya hadhara ni kuuwa upinzani?, Sumaye alinihoji

​
Very logical and standardized.

Na ipo siku na wao yatawakuta kwa kuzuiwa kuingia maeneo ya ngome za upinzani.

Ngoja wayapalilie
 
14 August 2020
Hai, Kilimanjaro
Tanzania

Madhara ya Marufuku ya Siasa kwa miaka 5 imesababisha CCM kukosa uvumilivu wa kisiasa na kutishia machafuko nchini
Kufuatia kupigwa marufuku shughuli
za kisiasa Tanzania sasa tunaona madhara yake katika maeneo fulani. Na athari zake zimekuwa kubwa kabisa kwa upande wa CCM kwa wanachama, makada, wafuasi na wapenzi wake kukosa kufuata sheria, jadi , kawaida ya waTanzania kushindanisha hoja kwa kutumia ushawishi na kubaki na ulemavu wa kifikra kuamua kutumia nguvu na mabavu.

Video : Tukio la wanaCCM jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro
​


Shughuli za kisiasa zilitumika kutoa elimu ya kiuraia kuwajenga Watanzania kuamini katika kupiga kura ndiyo njia sahihi ya kumkataa mwanasiasa fulani baada ya kusikiliza hoja zake.
...
Tuliyoyaona kule wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ni matunda ya serikali ya CCM Mpya kupiga marufuku viongozi wa vyama vya upinzani kufika maeneo fulani kwa miaka 5 sasa, sababu watawala wa CCM wanadai mbunge wa chama fulani siyo eneo lake la kibunge au kuwa uchaguzi umeisha hivyo hakuna kuendelea kufanya siasa za hoja kujenga ushawishi.

Katiba ya nchi iliona mbali kuwa ruhusa ya kufanya siasa ni afya kwa utulivu wa nchi ili ikifikia kipindi cha kampeni waTanzania wasiwe wabaguzi wa kisiasa au kimaeneo bali wawe na ufahamu wa kufanya maamuzi kupitia sanduku la kura.


Nawe unawakilisha hoja mufu, hafifu na za kitoto (kulalamika tu) badala ya kuleta hoja za Sera mbadala tynapoelekea Uchaguzi Mkuu.

Katika utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano ni wendawazimu kusema Haki na Uhuru wa kufanya siasa uliminywa. Vyombo vya habari (ambavyo vya binafsi ni vingi kuliko vya Serikali) na mitandao ya kijamii, vimetumika sana kuikashifu Serikali, na hasa Rais, kwa kisingizio cha kuikosoa, kuliko wakati wote wa utawala wa Tanzania huru. Vingetumika kuelimisha jamii (kwa jinsi unavyotaka wewe), jamii ingenufaika zaidi. Ila vimetumika kujenga chuki kati ya jamii na Serikali ambayo imeendelea kutekeleza ahadi za Chama chake kuhusu maendeleo.

Hivyo basi, kilichotokea na kutendeka huko ni ujumbe tosha kwa upinzani kuwa ifikapo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, wagombea watambue kwamba Tanzania kabla na baada ya vyama vingi vya siasa, siyo ya leo. Tanzania ya sasa mwanasiasa atapimwa kwa matendo yake chanya kwa jamii na siyo maneno ya mdomoni mwake km "nitawafanyia hiki mkinichagua".
 
18 Julai 2020
Ofisi za CCM Wilaya
Dodoma, Tanzania

VURUGU ZAIBUKA UTEUZI WA WAGOMBEA UDIWANI CCM DODOMA MJINI

Vurugu zimeibunka katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Dodoma baada ya Makada wa CCM wanaodai Majina ya Wagombea Udiwani yaliyopitishwa yamebadilishwa bila Sababu za Msingi katika baadhi ya kata za Wilaya hiyo na kuamua kuweka kambi katika ofisi hizo.
Source : millard ayo
 
Madhara ya kufanya siasa za umimi kwa miaka mitano bila kushirikisha jamii

Mkapa aliionya CCM Mpya kwa kutengeneza taswira ya kufikirika ikaleta picha kuwa kila kitu kimefanywa kuonekana umimi wa uwezo wa "ajabu" wa Magufuli kutatua changamoto zote pekee yake.

Na mzee Mkapa kuonya kuwa itawaletea tabu CCM kwa mgombea wao kubebeshwa lawama badala ya chama na serikali yake maana Rais atakuwa ametengwa kichama na kiserikali kuonekana anafanya mambo kibinafsi bila kushirikisha wengine : video ya angalizo la Mkapa hii hapa chini na sasa Magufuli anaonekana kisiasa na kiserikali mpweke kuelekea Oktoba 2020

6 Julai 2018
Mkapa: Napenda Serikali yetu ikijitambulisha kuwa ni Serikali ya CCM

 
Mkuu

Kupiga malufuku wapinzani kufanya siasa katika kipindi cha miaka 5 ,kimeleta faida kwa wapinzani.

CCM walisahau kuwa,ili kupiga malufuku wapinzani ,lazima kwanza uwauwe wananchi wote ili utawale peke yako,

Sababu upinzani siyo chama Bali ni WANANCHI.

Cc.upinzanisiyo cham,Bali ni WANANCHI.

Kwa hiyo kupiga malufuku kwa shughuli za kisiasa ndani ya miaka 5 kimeleta faida kwa vyama vya upinzani na WANANCHI.
Na kupiga malufuku kwa shughuli za kisiasa ndani ya miaka 5 kumeleta hasala kwa CCM.
 
Yapo tuliyoyaahidi kuyatekeleza kwa wananchi katika kipindi cha miaka mitano, nisingependa kuona mtu yeyote ananichelewesha kutekeleza hayo niliyoahidi kwa kipindi cha miaka mitano,”
Haya kayatekeleza sasa?? Hahahaha
 
Musoma, Mara
Tanzania

MGOMBEA AKOSA UVUMILIVU



Mgombea wa CCM ngazi ya Urais akiongea na wananchi wa mkoa wa Mara nchini Tanzania katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2020
 
5 September 2020

HUU NDIO MPANGO WA YEREMIA K. MAGANJA WA NCCR-MAGEUZI KWA TUNDU LISSU, MAGUFULI , LIPUMBA NA MEMBE


YEREMIA MAGANJA NI NANI? - NCCR Mageuzi
Yeremia Kulwa Maganja na ni mkaazi wa Tegeta Jijini Dar es Salaam. Alizaliwa Disemba 24, 1967 huko Bunda Mkoani Mara. Ameoa na ni baba wa Watoto 4

Alipata elimu yake ya msingi shule ya msingi Balili iliyopo Bunda mkoani mara kwa miaka 6 tu na baadaye kuhamia Shule ya Msingi Mlimani iliyopo Bariadi Mkoani Simiyu akihitimisha elimu yake ya Msingi.

Mnamo mwaka 1983 alijiunga na shule ya Sekondari Ilboru iliyopo Mkoani Arusha kwa miaka minne kabla ya kujiunga na shule ya Sekondari ya Tosamaganga iliyopo Mkoani Iringa mwaka 1987 hadi 1989 kwa masomo ya kidato cha tano na sita (A-level).

Mwaka 1989 ndugu Yeremia Kulwa Maganja alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi 838 KJ katika programu ya chama kwa ajili ya kupata mafunzo kwa mujibu wa sheria kwa mwaka mmoja.

Alipata Shahada yake ya kwanza ya masuala ya usimamizi wa biashara toka Chuo kikuu cha Tumaini hapa Dar es Salaam.

Ndugu Yeremia Kulwa Maganja ana shahada ya uzamili ya Usimamizi wa Biashara kutoka chou kikuu cha Mzumbe Jijini Dar es salaam

Aidha ndugu Maganja amesoma masomo ya computer ngazi ya Stashahada (diploma) katika Kituo cha Taifa cha Computer (NCC-UK) cha Uingereza.

KAZI

Ndugu Maganja amefanya kazi mbalimbali hapa nchini na kimataifa. Amefanya kazi na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya -URT katika Kitengo cha Bajeti za Utawala na kitengo cha fedha na mikataba kwa Zaidi ya miaka 18.

Ndugu Maganja ni mmiliki wa kampuni ya Ushauri na Biashara katika uwekezaji (ANDEL Consultants) ambapo yeye ni Meneja Mkuu.

Lakini pia ndugu Maganja ni Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa taasisi isiyo ya kiserikali ya The Registered Trustees of Maganja Foundation

Ndugu Maganja amepata mafunzo mbalimbali katika nchi mbalimbali barani ulaya na afrika ikiwemo Ubeligiji na Kenya

JAMES MBATIA NA MUAFAKA WA KITAIFA

 
5 September 2020
Mbeya, Tanzania

Dr. Tulia awaonya wapinzani

 
Back
Top Bottom