Ni mfanyabiashara gani anayekwepa kodi unayemfahamu wewe? Watu wanapenda sana kuropoka. Ukimwuliza hajui chochote.
Kuna uhuni aliuanzisha marehemu. Aliyalazimisha mabenki kupeleka kwake majina ya watu wenye pesa nyingi bank. Akijisikia kumpora pesa mtu, wanamfungia account halafu ndiyo wanamwandikia kuwa apeleke uthibitisho wa kulipa kodi zote kwa miaka 10 iliyopita. Tena waliokuwa wakipelekewa barua, unakuta miaka yote ya huko nyuma walikuwa na tax clearance tayari. Ulikuwa ni uhuni, na kinyume cha sheria, lakini kwa sababu ulikuwa ni uongozi wa kidikteta, alifanya alivyotaka.
Huwezi kumdai mtu risiti za kulipa kodi miaka 10 iliyopita wakati tayari kwa miaka hiyo alikwishapata tax clearance.
Wajinga wanafikiri ni rahisi kukwepa kodi. Wanaoweza kukwepa kodi kiurahisi, labda wafanyabiashara wa maduka, lakini siyo wawekezaji wakubwa.