Tena ni hawa wenye majina na wanasiasa wana ukwasi wa kutisha, na hata biashara zao hazilingani na mapato yao. TRA hawakurupuki kama wengi wanavyodhani, ninavyojua kwanza wakina kuna kasoro kwenye kodi zako hukupigia simu ili ufike ofisini sasa wengi hawaendi na wnakuwa na kibri wanasahau EFD machine haziongopi,pia akaunti zao zote zinasomeka na mtoza ushuru, kwa hiyo huwa anjaua chochote kinachofanyika. Utasikia tunataka maendeleo lakini hao hao hawalipi kodi. Hii ya kukimbilia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ili uonewe huruma sidhani kama inasaidia. Ila yote haya tumeyataka wenyewe,enzi za unanijua mimi nani zimerudi. Wakwepa kodi wamerudi kwa kasi.