Madhara ya uchumba wa muda mrefu kupita kiasi

Madhara ya uchumba wa muda mrefu kupita kiasi

Amran Mpogole

Member
Joined
Oct 2, 2022
Posts
29
Reaction score
26
1. Uchumba wa mda mrefu Hufungua mlango wa uasherati.

Uchumba wa mda mrefu kupita kiasi hufungua mlango wa dhambi ya kufanya mapenzi kabla ya ndoa kati yenu, kwasababu mtakuwa mmetumia muda mwingi mrefu kuwa pamoja na kujihalalishia uhalali wa kushiriki tendo la ndoa kwa kujiona tayari mmeshazoeana na kujihisi ni kama mke na mume tayari.

2. Uchumba wa muda mrefu Hupunguza kasi yenu katika mambo ya Mungu.

Kukaa sana katika uchumba kupita kiasi kunaweza kushusha kiwango chenu cha Imani kwasababu nguvu kubwa ya vipaumbele vyenu na muda wenu mmewekeza kwenye mambo ya mahusiano zaidi kuliko kuwekeza kwa Mungu.

3. Uchumba wa mda mrefu Unanyonya kiwango kikubwa sana cha nguvu zako za kihisia.

• Muda mwingi unautumia kumuwaza mchumba wako.

• Huna uhakika huko aliko kama yupo salama?

• Utataka ujue kila anachofanya na kwa muda gani.

• Utataka kujua yupo wapi, anafanya nini, anakula nini, amevaa nini, amepaka mafuta gani n.k.

• Anachukua mawazo yako kwa sehemu kubwa sana na wakati mwingine hata ufanisi kazini kwako unapungua.

4. Uchumba wa mda mrefu Unaweza kupelekea mawazo yasiyofaa na ya upinzani kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki.

• Uchumba unapokaa kwa muda mrefu sana kupita kiasi unawafanya wanandugu kuanzisha maneno maneno ambayo yanaweza kuharibu na kila kitu katika mahusiano hayo.

• Kuna msemo wa kiswahili unasema kuwa "bata ukimchunguza sana huwezi kumla" kama mmekaa katika uchumba kwa muda mrefu sana, inaweza kuwafanya wanandugu kumfuatilia mchumba wako kwa ukaribu kwa muda mrefu na kuanza kugundua vikasoro vidogo vidogo ambavyo hata kama vilikuwa vinaweza kurekebishika wao wanavishikilia na kusema huwezi kuoana na yule kwasababu ya hivyo vikasoro kasoro wanavyoviona kwake.

5. Uchumba wa mda mrefu unaweza kusababisha uchumba kuvunjika kabla ya kuoana.

• Kukaa katika mahusiano ya uchumba kwa muda mrefu kunaweza kupelekea hata uchumba wenyewe kuvunjika.

• Kukaa katika uchumba muda mrefu kunaweza kuwafanya hata ile shauku mliyokuwa nayo ya kuoana iweze kuisha kabisa na kuwafanya mjikute mkivunja na ujumba wenyewe kati yenu.

6. Utaleta majeraha makubwa sana baina yenu hasa baada ya uchumba kuvunjika, kutakuwa na majuto na maumivu sana kwasababu zifuatazo:

• Kupotezeana muda miongoni mwenu.

• Kupoteza pesa na vitu mbalimabli mlivyopeana wakati wa uchumba.

• Maumivu ya kumwaga siri zako hata zile za ndani kabisa ambazo usingependa mtu mwingine azijue, sasa unakuwa huna uhakika kama hatamweleza mtu mwingine huko nje.

• Aibu kwa ndugu, jamaa na marafiki na jamii kwa ujumla.

• Hupelekea historia mbaya kwa wachumba watakao fuata kwako na hasa kama uchumba ujao hautafanikiwa pia.

7. Kuendesha uchumba wa muda mrefu ni gharama kubwa.

• Safari za mara kwa mara kwaajili ya kuonana na mchumba wako.

• Mitoko "outing" za mara kwa mara pamoja na mchumba wako.

• Mawasiliano ya kila dakika na mchumba wako.

• Kutumiana zawadi za mara kwa mara na mchumba wako.

Mwisho​

Tuzidi kujifunza na tusichoke kujifunza.
 
Hiyo namba moja hapana aiseeh

Hata tukutane Leo na kesho kutwa tunaoana yaan lazima unipe,mechi haiwezi kuanza 1-0
 
Vile navykenzo ( Aika & nahreel ) wanavyoutizama huu Uzi [emoji1787][emoji1787]
20221109_084847.jpg
 
Mbona ninae huu mwaka wa 4sasa ila kayataka mwenyewe anajifanya mlokole sana nimemwambia kama sijaona kama yaliomo yamo siendi kwao akasema anafikiria jibu ndio namsikikizia pote la mbali nina mpango wa kumwacha maana msimamo wake unanitilia shaka.ila nje ya hapo kuna mmoja huko naserereka nae kila wiki nikitaka anaileta bila wasiwasi
 
Back
Top Bottom