Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Hata kahawa zina caffeine. Hata chai (majani ya chai) nayo ina caffeine.

Je, hunywi kahawa wewe? Hunywi chai wewe?

Sinywi chai wala kahawa unless ni Decaffeinated.

Nikikosa ni Soya kwa kwenda mbele
 
Katazeni vilaji vyoooteee ila kwenye maneno hii 'majani' a.k.a mmea wa kondeni sitawaelewa kabisaaaaaa hata mfanyeje
 
1001358_520283921359711_418174972_n.jpg

SODA NI SUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU.

AFYA za mamilioni ya Watanzania na watu Duniani kwa ujumla wanaotumia vinywaji vya aina ya soda ipo hatarini, baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo,

Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanyw
a na wataalamu waliobobea katika afya ya umma duniani, umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.

Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.

Utafiti huo unaonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji aina ya soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu.

IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa binadamu.

Kwamba matangazo hayo yanayogharimu mamilioni ya fedha ndiyo yanayokifanya kinywaji hicho kuwa maarufu zaidi duniani, licha ya kuwa na madhara makubwa katika mwili wa binadamu.

Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa umaarufu mwingine wa kinywaji aina ya soda ni utamu wa kupindukia ulio ndani ya soda.

Utafiti wa IJUTA unaonyesha kuwa utamu wa kupindukia iliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya asidi iliyomo ndani ya soda.

IJUTA imegundua kuwa kiwango cha asidi kilicho ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa walaji kwa sababu ya kuhofia kuwa wakibaini wataacha kikutumia kinywaji hicho.

Inaelezwa pia kuwa madini ya cola yaliyo ndani ya soda yana kilevi aina kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.

Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi, ugonjwa wa ini na mengineyo.

Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa soda huwekewa ‘fructose’ (sukari) nyingi kupitia mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala nchini Marekani, amekaririwa na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini humo akieleza kuwa kinywaji aina ya soda ni hatari kwa binadamu, sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi, jambo alilosisitiza kuwa siyo la kutia chumvi, bali ukweli halisi.

Watumiaji wa vinywaji aina ya soda wanaelezwa kuwa wamekuwa wakinywa kiasi kikubwa cha kaboni, kafeini (dawa ya kulevya), sukari ya kupundukia na asidi kali ambayo huvuruga afya ya mtumiaji kwa kiwango cha juu.

Soda pia imebainika kutokuwa na lishe ya aina yoyote zaidi ya maji na sukari.

Uchunguzi wa IJUTA na utafiti ya wanasayansi mbalimbali duniani, umeonyesha kuwa watu wengi hawajui kuwa unywaji wa soda huwaongezea kiasi kikubwa cha madini joto.

Chupa moja ya soda yenye ujazo wa mililita 330 husababisha unene kwa kiwango cha paundi moja kwa mwezi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kisukari Tanzania (TDA), Ramadhan Mongi, amepata kukaririwa na vyombo vya habari hapa nchini akieleza kuwa ugonjwa wa kisukari Tanzania umeongezeka mara sita katika siku za hivi karibuni.

Alisema miaka kumi iliyopita, hali ya kisukari ilikuwa asilimia tatu (3), lakini katika miaka ya karibuni umeongezeka mara sita.

“Tunastahili kuongeza jitihada ya kupambana na gonjwa hili la kisukari kwa gharama zote kwa sababu kisukari ni moja ya magonjwa manne yanayomaliza Watanzania,” alisema.

Utafiti uliofanyika Mkoa wa Dar es Salaam ulibaini kwamba kati ya watu watano waathirika wa kisukari, mmoja tu ndiyo hupata matibabu ya serikali.

Unywaji kwa mpigo wa kabohaidrets iliyo na sukari nyingi kwenye soda hudhoofisha seli zinazozalisha vimeng’enya tofauti na vyakula vingine na pia imebainika kuwa sukari ikiingia kwa wepesi kwenye mzunguko wa damu husababisha kongosho kuzalisha vimeng’enya vingi mwilini.

Uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya wanawake ya Boston nchini Marekani na katika Chuo cha Kitabibu cha Harvard umeonyesha wanawake 51,000 hawakuwa na kisukari mwanzoni mwaka wa 1991, lakini miezi minane baadaye wanawake 741 waligundulika na kisukari.

Ripoti ya utafiti huo ilionyesha kuwa wanawake waliokuwa wakitumia kinywaji aina ya soda moja ama mbili kwa siku waliongezeka uzito maradufu na walikuwa hatarini kupata ugonjwa wa kisukari.

Pia ilionyesha kuwa soda hudhoofisha mifupa na husababisha hali ya mifupa kupuputika, hali inayomuweka mtumiaji kuwa katika hatari ya kuvunjika mifupa kirahisi.

Madhara mengine yaliyobainika kusababishwa na unywaji soda ni kupukutika kwa meno na ama kuoza. Pia soda husababisha matatizo ya figo.

Soda yenye chembe ya cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya asidi na kemikali mbalimbali zinazofichwa vipimo vyake kwa walaji.

Madaktari bingwa wa wanamichezo wanaeleza madhara yanayosababishwa na soda mwilini kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, uharibifu wa ini, huvurugu mfumo wa kumeng’enya chakula tumboni kutokana asidi ya kiwango cha juu iliyo kwenye soda.

Wanashauri kuwa soda haistahili kutumika kama kishawishi kwenye mchezo, kwa sababu ina madhara makubwa kwa wanamichezo kwa sababu hunyonya maji kwenye mwili na kudhoofisha mwili.

Wakati utafiti huo ukidhihirisha hayo, Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.

Kwa ushauri zaidi tuwasilie, pia matatizo yakizidi muone daktari kwa matibau zaidi.

Hakuna kisicho na madhara dunia ya leo acha watu wafanye yao. BTW in the end tutakufa tu tunywe au tusinywe soda
 
Mzizi Mkavu, makala yako ni nzuri, lkn hujatuambia aina gani za soda unazozizungumzia. Ina maana soda aina zote madhara yake yanafanana? Unatuambiaje kuhusu 'diet soda' au soda zinazodaiwa hazina sukari kama 'coca cola zero'? Vipi kuhusu 'soda water' kama vile tonic, evervese na za aina hiyo?
 
Kuhusu kufa hilo halina shaka, lkn kwa kuwa zekano wa kuchelewesha kifo au kukiharakisha, basi unaweza kuchukua hadhari, ndio maana una ambiwa 'dont drink and drive' au 'speed kills'.
 
Dr. wangu MziziMkavu asante sana kwa kuendelea kutoa elimu ya kuboresha afya zetu. Binafsi familia yangu ilishaachana na soda muda mrefu. Tunafurahia juice za asili tu ikiwemo za matunda, ubuyu, ukwaju na ninaona hata afya inaboreka!!! Hakika soda zote zina sukari, hata wao wanaosema eti zero coca siamini kama ni kweli maana ina sukari kama ulishawahi ionja. Ninafikiri wanaounguza tu sukari. Ukitaka kujua madhara ya soda hasa coca cola, utakuwa jutia sana mifupa yako kukosa nguvu sana uzeeni, inakula mifupa sana!!!! Sukari tena ukianza kuwa 40s ni bora kabisa uachane na vitu vya sukari. Kwa nini usinywe maji wakati unajua 75% 0r 3/4 ya mwili wa mwanadamu/animals ni maji maji!!!! Keep it up Dr. MM.
 
Mzizi Mkavu, makala yako ni nzuri, lkn hujatuambia aina gani za soda unazozizungumzia. Ina maana soda aina zote madhara yake yanafanana? Unatuambiaje kuhusu 'diet soda' au soda zinazodaiwa hazina sukari kama 'coca cola zero'? Vipi kuhusu 'soda water' kama vile tonic, evervese na za aina hiyo?

Wimana

Kama unaharakisha kifo tumia tu hizo sukari sumu.
Usititishike bana, jisomee hapa links Discovery Health "Avoid Artificial Sweeteners" link 2. Aspartame is, By Far, The Most Dangerous Substance on The Market That is Added to Foods. link3. Dr. Joseph Mercola: America's Deadliest Sweetener Betrays Millions, Then Hoodwinks You With Name Change
 
MziziMbichi,

Vipi kuhusu BIA (BEER)? Wine, Maji yasiyo salama (ambayo asilimia 90 ya waTanzania wanatumia)?
 
Bia haina sumu maana km ni sumu my dad angeshakufa mapema..coz ni mwaka wa 40 na zaidi sasa anakunywa bia kila siku ktk mwaka I mean siku 365 zoote haachi ht siku moja .now he is 62 haumwi presha., figo wala sijui nini..very fit and strong
 
1001358_520283921359711_418174972_n.jpg

SODA NI SUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU.

AFYA za mamilioni ya Watanzania na watu Duniani kwa ujumla wanaotumia vinywaji vya aina ya soda ipo hatarini, baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo,

Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanyw
a na wataalamu waliobobea katika afya ya umma duniani, umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.

Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.

Utafiti huo unaonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji aina ya soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu.

IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa binadamu.

Kwamba matangazo hayo yanayogharimu mamilioni ya fedha ndiyo yanayokifanya kinywaji hicho kuwa maarufu zaidi duniani, licha ya kuwa na madhara makubwa katika mwili wa binadamu.

Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa umaarufu mwingine wa kinywaji aina ya soda ni utamu wa kupindukia ulio ndani ya soda.

Utafiti wa IJUTA unaonyesha kuwa utamu wa kupindukia iliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya asidi iliyomo ndani ya soda.

IJUTA imegundua kuwa kiwango cha asidi kilicho ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa walaji kwa sababu ya kuhofia kuwa wakibaini wataacha kikutumia kinywaji hicho.

Inaelezwa pia kuwa madini ya cola yaliyo ndani ya soda yana kilevi aina kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.

Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi, ugonjwa wa ini na mengineyo.

Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa soda huwekewa ‘fructose’ (sukari) nyingi kupitia mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala nchini Marekani, amekaririwa na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini humo akieleza kuwa kinywaji aina ya soda ni hatari kwa binadamu, sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi, jambo alilosisitiza kuwa siyo la kutia chumvi, bali ukweli halisi.

Watumiaji wa vinywaji aina ya soda wanaelezwa kuwa wamekuwa wakinywa kiasi kikubwa cha kaboni, kafeini (dawa ya kulevya), sukari ya kupundukia na asidi kali ambayo huvuruga afya ya mtumiaji kwa kiwango cha juu.

Soda pia imebainika kutokuwa na lishe ya aina yoyote zaidi ya maji na sukari.

Uchunguzi wa IJUTA na utafiti ya wanasayansi mbalimbali duniani, umeonyesha kuwa watu wengi hawajui kuwa unywaji wa soda huwaongezea kiasi kikubwa cha madini joto.

Chupa moja ya soda yenye ujazo wa mililita 330 husababisha unene kwa kiwango cha paundi moja kwa mwezi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kisukari Tanzania (TDA), Ramadhan Mongi, amepata kukaririwa na vyombo vya habari hapa nchini akieleza kuwa ugonjwa wa kisukari Tanzania umeongezeka mara sita katika siku za hivi karibuni.

Alisema miaka kumi iliyopita, hali ya kisukari ilikuwa asilimia tatu (3), lakini katika miaka ya karibuni umeongezeka mara sita.

“Tunastahili kuongeza jitihada ya kupambana na gonjwa hili la kisukari kwa gharama zote kwa sababu kisukari ni moja ya magonjwa manne yanayomaliza Watanzania,” alisema.

Utafiti uliofanyika Mkoa wa Dar es Salaam ulibaini kwamba kati ya watu watano waathirika wa kisukari, mmoja tu ndiyo hupata matibabu ya serikali.

Unywaji kwa mpigo wa kabohaidrets iliyo na sukari nyingi kwenye soda hudhoofisha seli zinazozalisha vimeng’enya tofauti na vyakula vingine na pia imebainika kuwa sukari ikiingia kwa wepesi kwenye mzunguko wa damu husababisha kongosho kuzalisha vimeng’enya vingi mwilini.

Uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya wanawake ya Boston nchini Marekani na katika Chuo cha Kitabibu cha Harvard umeonyesha wanawake 51,000 hawakuwa na kisukari mwanzoni mwaka wa 1991, lakini miezi minane baadaye wanawake 741 waligundulika na kisukari.

Ripoti ya utafiti huo ilionyesha kuwa wanawake waliokuwa wakitumia kinywaji aina ya soda moja ama mbili kwa siku waliongezeka uzito maradufu na walikuwa hatarini kupata ugonjwa wa kisukari.

Pia ilionyesha kuwa soda hudhoofisha mifupa na husababisha hali ya mifupa kupuputika, hali inayomuweka mtumiaji kuwa katika hatari ya kuvunjika mifupa kirahisi.

Madhara mengine yaliyobainika kusababishwa na unywaji soda ni kupukutika kwa meno na ama kuoza. Pia soda husababisha matatizo ya figo.

Soda yenye chembe ya cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya asidi na kemikali mbalimbali zinazofichwa vipimo vyake kwa walaji.

Madaktari bingwa wa wanamichezo wanaeleza madhara yanayosababishwa na soda mwilini kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, uharibifu wa ini, huvurugu mfumo wa kumeng’enya chakula tumboni kutokana asidi ya kiwango cha juu iliyo kwenye soda.

Wanashauri kuwa soda haistahili kutumika kama kishawishi kwenye mchezo, kwa sababu ina madhara makubwa kwa wanamichezo kwa sababu hunyonya maji kwenye mwili na kudhoofisha mwili.

Wakati utafiti huo ukidhihirisha hayo, Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.

Kwa ushauri zaidi tuwasilie, pia matatizo yakizidi muone daktari kwa matibau zaidi.

Wewe ni noma kaka
 
Some time Preventive measures is the best than Curetive measures. Kunauwezekano mkubwa haya mambo yanaukweli lakini serikali haiwezi ku-interverne wenyewe wanaangalia zaidi revenue, but your heath is up to you, kama unavyoweza kuvuka road kwa umakini sana ndo afya yako inabidi uitunze hivyo kama unajua dhamani yako.
Tafiti kama hizi zimeshafanyika sana, ndani ya mwaka huu kuna Seneta mmoja Kule USA 'jimbo nimesahau'' alipendekeza vinywaji vya aina hii vizuiliwe jimboni kwake sababu ya athari zake kukithiri maana asilimia ya watu wenye unene wa kubindukia imezidi kuongezeka, lakini pia haikuweza kufanikiwa maaa wanasiasa waliingilia kati.
 
Mzizi Mkavu, makala yako ni nzuri, lkn hujatuambia aina gani za soda unazozizungumzia. Ina maana soda aina zote madhara yake yanafanana? Unatuambiaje kuhusu 'diet soda' au soda zinazodaiwa hazina sukari kama 'coca cola zero'? Vipi kuhusu 'soda water' kama vile tonic, evervese na za aina hiyo?
punit-soni-Hhu-blog-23331.jpeg
 
Bia haina sumu maana km ni sumu my dad angeshakufa mapema..coz ni mwaka wa 40 na zaidi sasa anakunywa bia kila siku ktk mwaka I mean siku 365 zoote haachi ht siku moja .now he is 62 haumwi presha., figo wala sijui nini..very fit and strong

[h=2]Mwakyusa😛ombe ina uhusiano na saratani, moyo na magonjwa ya akili[/h]
KWA Miaka mingi watu wamekuwa wakitumia pombe kama sehemu ya kiburudisho huku wengine wakiamini kuwa inasaidia kupunguza mawazo. Pamoja na imani hizo, wataalamu wa afya wanabainisha kuwa matumizi ya pombe katika mwili wa binadamu yana madhara makubwa.

Akizungumza katika mkutano wa pili wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa anasema pombe ina uhusiano wa moja kwa moja na magonjwa kama saratani, magonjwa ya akili na Ukimwi.

Vilevile pombe inachangia kwa kiwango kikubwa kuwepo kwa vipigo kwa wanawake... "Mtu aliyekunywa pombe huwa hana uchaguzi katika kufanya mambo, ndiyo unakuta wengine wanatukana, wanapigana na wengine kudiriki hata kujikojolea. Vitendo vyote hivi mtu hawezi kuvifanya akiwa hajalewa."

Anasema pamoja na serikali kuzitoza kodi kubwa kampuni zinazotengeneza pombe lakini bado watu wanaendelea kunywa kama kawaida na yote hiyo ni kutokana na kutokujua madhara yake.

Mtaalamu kutoka Chama cha Afya ya jamii (TPHA), Dk Ali Mzige anasema pombe ina madhara ya aina mbili. Kwanza ni kuathirika kwa mishipa ya fahamu mwilini kote kwa kupunguza uwezo kufanya kazi na pili ni kuungua baadhi ya ogani za mwili hasa tumbo pindi mtu anapokunywa.

Kuathirika huko ni kwa aina nne za wanywaji, hatua ya kwanza ni ile ya kuchangamka, hapa mtu hujisikia mzima zaidi ya kawaida moyo unapiga haraka, tumbo linameng'enya chakula haraka na hamu ya chakula kuongezeka.

Hatua ya pili, mtu akiendelea kunywa anachanganyikiwa na kuzungumza sana, kukosa aibu, utu kubadilika, kutawala tabia za kimwili, hamu ya chakula kuongezeka na hapo ndipo walevi wanapoagiza nyama choma kwa wingi.

"Tunaposema kutawala tabia za kimwili ina maana kuwa mtu anakuwa hana maamuzi sahihi katika maamuzi. Mnywaji akiendelea kunywa pombe hucharuka kutokana na neva zake za ubongo kushindwa kumiliki mwili na mambo yote anayoyafanya huwa hayana utaratibu."

Dk Mzige anasema mnywaji huwa mkorofi na anaongea maneno yasiyo na maana. Baadhi ya wanywaji huchukulia hatua hii kama raha yao. Kinachojitokeza ni kupoteza hamu ya kula.

Hatua ya nne mtu akilewa kupita kiasi huwa hajijui analala fofofo. Huenda akajikojolea au kutapika, inategemea na kiasi cha pombe alichokunywa.

Kwa upande wa ogani, pombe huathiri zaidi viungo vinavyopata pombe nyingi kila wakati. Mfano wa viungo hivyo ni mdomo, koo na tumbo, ambavyo vyenyewe hufikiwa na pombe nyingi.

"Pombe yote mtu anayokunywa hupita katika seli za ini huku zikijaribu kuliondoa ini hilo lakini nazo zinalewa chakari na baadhi zina kufa," anasema Dk.Mzige.

Anasema mtu akinywa sana seli nyingi zinakufa na mtu akinywa kidogo chache zinakufa kisha nafasi yake inajazwa na nyuzi nyuzi za kovu. Ini huwa na mabilioni ya seli ambazo ni imara, hata mtu akinywa pombe nusu, seli zake bado zitaendelea na maisha, kama inafikia kikomo ini linashindwa kufanya kazi na kusababisha njia za nyongo na mishipa ya damu inaziba. Kila ogani ya mwili inaumia kivyake, lakini tumbo na ini ni mifano wazi.

Dk Joseph Mbatia kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anasema pamoja na madhara yake, mpaka sasa hakuna takwimu sahihi za wangapi wameathirika au wamepata madhara kwa kuwa unywaji wa pombe ni jambo lililokuwepo tangu enzi na enzi.

"Upatikanaji wa takwimu ndiyo utakaosaidia kuionyesha jamii madhara halisi ya pombe, kuliko hali ilivyo hivi sasa maana watu wengi wanaona kunywa pombe ni jambo ambalo lipo na limezoeleka," anasema na kuongeza:

"Zikiwepo takwimu sahihi zitawasaidia watunga sera kuandaa miswada bora ambayo baadaye inaweza kuwa sheria zitakazotekelezwa katika kudhibiti matumizi ya pombe."

Anasema hii haina maana kwamba sasa hivi hakuna sheria, la hasha, zipo ila utekelezaji wake si madhubuti ni kama hakuna kabisa huo utekelezaji wa sheria ya pombe. Kama ilivyo kwa sigara.

Dk Mbatia anasema, vifo, ulemavu au hasara ya mali inayotokana na pombe ni kubwa ingawa kwa sasa hakuna anayefahamu, kwa kuwa hakuna utafiti unaofanyika.

Kwa upande wake, Dk Bertha Maegga anayeshughulikia masuala ya utafiti kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road anasema pombe ni ugonjwa sugu ambao tiba yake ni sawa na ile ya kisukari, ambapo mgonjwa anatakiwa kufuatiliwa kwa karibu.

Anasema ulevi wa wataalamu wa sekta mbalimbali nchini ni tatizo kubwa hali inayosababisha kushuka kwa imani ya wananchi wanaotegemea huduma kutoka kwao.

Anasema utafiti mdogo uliofanyika kwenye kitengo chake umeonyesha kwamba asilimia kubwa ya viongozi wa maeneo wanaolalamikiwa kwa ulevi ni wa jinsi ya kiume.

Utafiti huo unaonyesha idadi ya walevi kuwa ni asilimia 24 ya watawala kwenye ofisi za umma, asilimia 27 ya wafamasia, madaktari asilimia 20 ambao waliripotiwa kuwa walevi zaidi hali inayotishia usalama wa maisha ya wagonjwa wao.

Anasema kuwepo kwa utafiti wa kina kutasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza madhara ya pombe, ingawa duniani kote hakuna sheria inayombana raia kutotumia kilevi kabisa.
Mwakyusa😛ombe ina uhusiano na saratani, moyo na magonjwa ya akili. chanzo. https://www.jamiiforums.com/jf-doct...no-na-saratani-moyo-na-magonjwa-ya-akili.html
 
Bia haina sumu maana km ni sumu my dad angeshakufa mapema..coz ni mwaka wa 40 na zaidi sasa anakunywa bia kila siku ktk mwaka I mean siku 365 zoote haachi ht siku moja .now he is 62 haumwi presha., figo wala sijui nini..very fit and strong

naomba niwe mnafki Dr. wangu
1456682_233083340191144_1463152640_n.jpg
 
Back
Top Bottom