Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vipi kuhusu Stoney tangawizi....nayo ni sumu???
Ata kushabikia manchester pia ni sumu
We umaakin tu ndo unakusumbua bibi zetu walikunywa soda miaka hyo mpaka leo wapo wanaish hayo madhara yanawapata kna nan?
We umaakin tu ndo unakusumbua bibi zetu walikunywa soda miaka hyo mpaka leo wapo wanaish hayo madhara yanawapata kna nan?
Hahaaaaa ningekuwa marehemu siku mingi sanaaaa

Aaaakunaa kituu awaa wanaojiitaa wasomii wakishaa somaa sanaa wanakujaa nakututishaa nilishaa sikiaa kuna doktaa nani sijui yule anasemaa ugalii nisumuu?mmmh tusitishanee bana hakuna cha nini walaa nini kufaa ni mipangoo ya muunguu watu wanahemea mipiraa mwaka watanoo huu hajafaa ndoo ujee uniambiee ninywe sodaa tu nifee kaaahvinginee banaa hatakama misio Dakota ivo ivo hakuna kitu ambachoo hakina madhara
Kila kitu ni sumu
Kunywa Soda ukiwa unajua Madhara yakeduh haya mambo haya.makala nzuri
Nadhan ushapata jibu
Bado mkuu
sio kweli,baadhi zilizopo hapo ni za uongo na zimekaa kisda sana,hazina ushahd wa kisayansi,ziko kwa kufikirika,acheni kudanganya watu.
SOURCE: MTANZANIA
ISSN: 0856-5678, Na. 7310
DATE: TODATE
PAGE: 03
HEADLINE: SODA NI SUMU
*******
Mamilioni ya watanzania wanaotumia vinywaji aina ya soda ipo hatarini baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo, MTANZANIA jumatano linaripoti.
Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa habari Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania-IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya duniani umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji sigara inayosabisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.
Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.
Utafiti umeonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji cha soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu.
IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji kuwa makampuni yanayotengeneza soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo.
Utafiti wa IJUTA umeonyesha kuwa utamu wa kupindukia uliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya acid iliyomo ndani ya soda.
IJUTA imegundua kuwa kiwango cha acid kilichomo ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa sababu ya kuhofia kuwa watu wakibaini wataacha kutumia kinywaji hicho.
Inaelezwa kuwa madini ya cola yaliyomo yana kilevi cha aina ya kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.
Dr. Mercola wa Marekani amekaririwa na tafiti mbalimbali akieleza kuwa soda ni hatari kwa binadamu sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi.
...Soda yenye chembe za cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya acid na chemicals zinazofichwa vipimo vyake kwa watumiaji.
Wakati utafiti huo ukidhihiriksha hayo, Taasisi ya chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.
*******
MY TAKE:
1: Nani atakayebaki salama?
2: Wabunge wetu mmeiona hii habari wakati mko hapo bungeni?
IMPORTANT CONTACTS:
TFDA:
Tel:
+255787555527
+255754772220
+255222450512
+255222450751
+255222452108
Email: info@tfda.or.tz
Web: www.tfda.or.tz
TBS:
Tel:
+255222450206
+255222450298
+255222450949
Email: info@tbstz.org
Web: www.tbstz.org