Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Hiyo ndio faida ya kunywa soda anitafute mimi kwa pesa nyingi nipate kumtibu wakiambiwa waache kunywa soda hawataki sasa ngojea wapatwe na maradhi ya ajabu tupate pesa na tuwatibu.
 
Aunty yangu amefanya kazi pepsi miaka 25 kila siku anakunywa pepsi mbili
 
Mwili huo m1 unaupangia masharti kibaaaaaao mwenyewe utakufa na mengine tuu wala sio hayo ya soda. Jiachie kifo kipo tuu
 
Binafsi nimefurah Mkuu kutuletea somo zuri aseeee
 
Aya makatazo siku hizi yamekua mengi sana.mara usile ichi mara kile,mara usinywe hichi wala kile.siku moja nimekuta jamaa kakusanya watu anawaambia wakila mayai yakuku wakisasa watakua mashoga.kachanganya changanya hapo matakataka yake akalitumbukiza yai kwenye condom yenye maji yenye ayo matakataka baada ya muda akalipasua lile yai akalionyesha uku akisema ile rangi yamaji ndo iyo iko kwenye yai na tumbon kwetu kuko ivyo.alafu akasema kwawale mliokula ayo mayai nauza dawa zakusafisha iyo sumu kwa elfu 10 tu.Nikamuuliza kati ya hizo dawa zake zamiti tusiyoijua na ayo mayai kipi kitakua hatari kwa afya zetu akaanza kua mkali.kwaiyo ayo makatazo yanayoenda sambamba nakuuzia watu madawa yamiti shamba yasiyothibitishwa muache.
 
Soda ni Soda ikiwa Soda ya Diet au soda ya kawaida ili mradi ni Soda sio nzuri kiafya kula matunda fresh toka shambani.Tengeneza juisi ya matunda nyumbani kwako kwa fya yako achana na sumu inayo kuuwa wewe taratibu bila ya wewe kujijuwa kama unakufa taratibu. (Silent Killer)
 

Ukila unakufa
Usipokula unakufa
Ukinywa unakufa
Usipokunywa unakufa

Either way,we are eating to survive kwa muda mfupi tu...
 
Chukua coca au Pepsi (350ml) weka kwa sufuria halafu chemsha jikoni hadi mwisho. Kitakachotokea utaamua mwenyewe.

Au hiyo coca Fanya kama unaoshea nyama mbichi(beef or pork). Utakachopata ndiyo chenyewe. Then endelea na ratiba yako
 
Matisho tu haya.
Hata ukifakamia bondo kwa miaka 50 linakuzeesha na unakongoloka kama ng'ombe aliyekosa majani.
 
Dah, kweli kabisa. Mi ni mlevi wa azam cola, nifanye nini ili niziache? Asubuhi siwezi kunywa chai kabisa, kifungua kinywa changu ni azam cola, usiku siwezi lala bila azam cola . Natamani kuachana na soda kabisa lakini siwezi. Je nifanyaje ili niweze kuacha? Sitaki maradhi na kifo cha kujitakia maana bado naupenda ugali.
 
Ujumbe mwanana kwenye hizi chupa....hebu tusome wote kwa sauti!!!!
 
Chukua coca au Pepsi (350ml) weka kwa sufuria halafu chemsha jikoni hadi mwisho. Kitakachotokea utaamua mwenyewe.

Au hiyo coca Fanya kama unaoshea nyama mbichi(beef or pork). Utakachopata ndiyo chenyewe. Then endelea na ratiba yako
Mikwala mingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…