Shemtibuko
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 728
- 1,014
Mkuu asante kwa ushauri mzuri, ingawa wajinga wanaponda na kuleta jokes, bt tupo pua ambao tumeelewa na tunashukuru, hao wapuuzaji kesho na keshokutwa watakutafuta kwa tiba yakishawakuta, wapige shekeli za kutosha, eti paulo na silla hawakunywa bt nao wamekufa[emoji22]View attachment 473413
HIZI NDIO SABABU KUMI KWANINI UACHE KUNYWA SODA KUANZIA LEO.
inawezekana una bahati sana kuiona hii makala na itakujenga sana kiafya...tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa
mwaka. japokua kuna watu wamekiri kunywa hata zaidi ya soda moja kwa siku amabayo huenda wanakunywa zaidi ya hicho kipimo. biashara ya soda inalipa sana duniani kwani ni kinywaji cha pili
kinachoongoza kunywewa duniani baada ya maji.
sasa ukiangalia mahusiano ya unywaji mdogo wa soda kila siku kiafya una madhara makubwa kuliko unywaji mdogo wa pombe kila
siku. yaani ni bora unywe chupa moja ya bia kila siku kuliko chupa moja ya soda kila siku. yafuatayo ni madhara ya soda ambayo yatakufanya ufikirie mara mbili kunywa soda tena.
1.Ugonjwa wa kisukari; kunywa soda moja ni sawa na kunywa vijiko 10 vya sukari, baada ya kunywa sukari hupanda sana mwilini na kongosho hutoa homoni ya ili insulini nyingi kushusha sukari. muda unavyozidi kwenda insulini huendelea kuishiwa nguvu[insulin resisitance] na hali hii husababisha wewe kupatwa na ugonjwa wa kisukari.
2. Unene na kitambi; utafiti ulofanywa na chuo kikuu cha havard umegundua kwamba watu wanaokunywa soda hunenepa mara mbili zaidi ya wale ambao hawanywi hivyo kama uko busy unapunguza uzito na pia mnywaji wa soda basi unapoteza muda.
3. upungufu wa madini muhimu mwilini; soda ina kemikali inayoitwa phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya calcium kwenye chakula ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kweye mwili wa binadamu.
4. ugonjwa wa kansa; soda ina kemikali inayoitwa caffeine ambayo imehusishwa na cancer mbalimbali za mwili mfano kansa ya kongosho, kansa ya utumbo na magonjwa mengine kama presha ya damu na kansa ya matiti.
5. huongeza sumu mwilini; soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu hivyo huongeza kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambacho ni hatari sana kwa afya mtumiaji.sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa presha, na kuua figo.
6. hubadilisha rangi ya meno; kila mtu anataka kua na meno masafi na meupe lakini baadhi ya soda zina kiasi kikubwa cha tindikali ambacho hushambulia na kuharibu meno kwa muda mfupi.hivyo kama unasumbuliwa na meno basi huu ni muda mzuri wa kuachana nayo.
7. addiction (Uteja); soda nyingi zina tabia ya kumfanya mtu apate ulevi wa soda husika yaani kuna watu unakuta anapenda sana soda fulani na asipoinywa kwa siku atahisi kama amepungukiwa kabisa na kitu fulani mwilini.hii itakufanya uwe mtumwa wa mwili wako mwenyewe.
8. huongeza kasi ya uzee; sumu ambazo unazipokea kwenye soda zinazeesha mtu mapema sana yani kijana mdogo wa miaka 20 hujikuta anaonekana kama miaka 35.
9. Hupunguza sana maji mwilini ; soda ina kiwango kikubwa cha madini ya sodium ambayo humfanya mtu abaki na maji kidogo na kwa muda mrefu atapata matatizo mengine ya kiafya kama mawe ya kwenye figo[kidney stone] na mawe kwenye nyongo ya binadamu.
10.Mwisho; ni vizuri kubadili mfumo wako wa maisha na kuanza kunywa vitu haviharibu mwili yaani badala ya kunywa soda basi tumia juice za Matunda ambayo ni mbadala mkubwa wa soda, lakini pia unaweza kunywa maziwa na kadhalika.
Nunuwa Machungwa kwa wingi kisha tengeneza jusi yake uwe unaweka ndani ya Friji ukijihisi unataka kunywa soda kunywa juisi ya machungwa utaacha kunywa soda mimi nimeiacha Soda huu ni mwaka 20 sijanywa soda.Dah, kweli kabisa. Mi ni mlevi wa azam cola, nifanye nini ili niziache? Asubuhi siwezi kunywa chai kabisa, kifungua kinywa changu ni azam cola, usiku siwezi lala bila azam cola . Natamani kuachana na soda kabisa lakini siwezi. Je nifanyaje ili niweze kuacha? Sitaki maradhi na kifo cha kujitakia maana bado naupenda ugali.
On a long enough timeline everybody's survival rate falls to 0%Mwisho wa siku nitakufa tu
Ni suala la muda
MziziMkavu kasema tunywage BIA tatu hadi nane kwa "thiku"...Kwahiyo tunywe nini mkuu?
Blaza hata muda unakuuwa taratibu(silent killer)Soda ni Soda ikiwa Soda ya Diet au soda ya kawaida ili mradi ni Soda sio nzuri kiafya kula matunda fresh toka shambani.Tengeneza juisi ya matunda nyumbani kwako kwa fya yako achana na sumu inayo kuuwa wewe taratibu bila ya wewe kujijuwa kama unakufa taratibu. (Silent Killer)
View attachment 473441
Blaza Fanya update fanta mpya yenye ladha ya berriesNunuwaMachungwa kwa wingi kisha tengeneza jusi yake uwe unaweka ndani ya Friji ukijihis unataka kunywa soda kunyw ajuis ya amchungwa utaacha kunywa soda mimi nimeiacha Soda huu ni mwaka 20 sijanywa soda.
Kama Paulo na Silla hawakunywa soda na wameshakufa unaamini nisipokunywa nitaishi milele?
Uwepo wa kifo usitufanye kukikimbilia kwa nguvu eti kwa sababu tu hakiepukiki.kila kitu kina madhara hata hayo maji. mwisho ni kufa tu kama wengine. why pasua kichwa.
Duh aisee ni balaa! usiombe yakukute mkuu wangu.Kuna rafiki yangu mmoja mwuza mitumba anasema awali alikuwa anakunywa soda aina ya Sprite mara tatu kwa siku baada miezi mitatu alihisi haja ndogo mara kwa mara, viungo vinalegea. Alipopima akakutwa anakisukari ambayo sahivi ni mwaka wa 3 anapambana nayo kwa miti shamba lakini hakijapona. Mwili umeisha hadi nywele zimenyonyoka pia
Sawa unahisi kila mmoja anakufa kisa soda ? Osama alikufa kisa soda ? Vipi kuhusu Saddam Hussein ,Nyerere,Mandela nk.Uwepo wa kifo usitufanye kukikimbilia kwa nguvu eti kwa sababu tu hakiepukiki.
Ni vizuri kujaribu kukiepuka pale unapoweza hata kama kitakunasa kwa njia nyingine. Jamii bado inakuhitaji na haitaki kukupoteza kizembe, ndiyo maana mleta uzi kaamua kutoa somo hili.
Pia kama alivyoeleza, kuna shida na taabu za kutosha katika magonjwa hayo kabla hujakifikia hicho kifo.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] wapi hiyo mkuu? nadhani ndo yule rafiki yake Dr. Ndodi niliwahi kumwona akifanya hilo zingaombwe mitaani tabora.. dah kwamba watu watakuwa mapunga [emoji23] [emoji23]Aya makatazo siku hizi yamekua mengi sana.mara usile ichi mara kile,mara usinywe hichi wala kile.siku moja nimekuta jamaa kakusanya watu anawaambia wakila mayai yakuku wakisasa watakua mashoga.kachanganya changanya hapo matakataka yake akalitumbukiza yai kwenye condom yenye maji yenye ayo matakataka baada ya muda akalipasua lile yai akalionyesha uku akisema ile rangi yamaji ndo iyo iko kwenye yai na tumbon kwetu kuko ivyo.alafu akasema kwawale mliokula ayo mayai nauza dawa zakusafisha iyo sumu kwa elfu 10 tu.Nikamuuliza kati ya hizo dawa zake zamiti tusiyoijua na ayo mayai kipi kitakua hatari kwa afya zetu akaanza kua mkali.kwaiyo ayo makatazo yanayoenda sambamba nakuuzia watu madawa yamiti shamba yasiyothibitishwa muache.
hahahaaaaa!!Kwanini usile na sumu ya panya Sasa!
Tatizo la juisi hazina msisimkoSoda ni Soda ikiwa Soda ya Diet au soda ya kawaida ili mradi ni Soda sio nzuri kiafya kula matunda fresh toka shambani.Tengeneza juisi ya matunda nyumbani kwako kwa fya yako achana na sumu inayo kuuwa wewe taratibu bila ya wewe kujijuwa kama unakufa taratibu. (Silent Killer)
View attachment 473441
[emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu naskia hizo kUjumbe mwanana kwenye hizi chupa....hebu tusome wote kwa sauti!!!!
View attachment 473460
Ongeza na pilipili kidogoTatizo la juisi hazina msisimko
Ongeza na pilipili kidogoTatizo la juisi hazina msisimko