Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Nashangaa wengine ndo tunasikia leo habari hizi! acha kunywa soda utaona utakavyopunguza matumizi ya kuto kwenda hospitali. kiwango kikubwa cha sukari kilichopo ndani ya soda kina leta madhara makubwa sana kiafya. Kinywaji salama ni maji tu! ndani ya mwili wanasema kunatakiwa kusafishwe, kama vyombo unasafisha kwa maji safi, je mwili wako ndo unausafisha kwa soda? kama mmea unaupa maji ili ukue na si soda, kwa nini wawapa wanao soda? tafakari
Huu ndio ukweli.
 
Kila kitu kina madhara mwilini endapo kikizidi,Hata maji yenye PH 7 yana madhara yakizidi,CHa msingi tufanye mazoezi kuweka mwili fiti,kuondoa sumu tunazokula na kunywa.
Mazoezi mazuri ni mazoezi ya kufikiri ayo ya kutanua kifua sijui kukimbia sio halisi.
 
Namshukuru Mungu alinisaidia kuuacha ulevi wa soda miaka mingi iliyopita. Nikipita sehemu nikamwona mtu akinywa soda huwa nnasikitika sana. Anyway, Mungu atusaidie kuujua huu ukweli kuwa: "soda is a sweet poison"
 
Kunywa juice ya azam au ya kutengeneza mwenyewe


Yaani unalinganisha juice ya kiwandani na juice fresh natural??!!

Mkuu ningekukuta live unamshauri mtu anywe juice ya azam, ningekuchapa makofi mengi sana walai.

-Kaveli-
 
Namshukuru Mungu alinisaidia kuuacha ulevi wa soda miaka mingi iliyopita. Nikipita sehemu nikamwona mtu akinywa soda huwa nnasikitika sana. Anyway, Mungu atusaidie kuujua huu ukweli kuwa: "soda is a sweet poison"

Watu wengi wanafahamu ukweli kwamba soda sio kinywaji kizuri ila wanachukulia poa.

Majuto ni Mjukuu.
 
Soda ni SUMU

AFYA za mamilioni ya Watanzania wanaotumia vinywaji vya aina ya soda ipo hatarini, baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo, MTANZANIA Jumatano linaripoti.

Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya ya umma duniani, umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.

Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.

Utafiti huo unaonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji aina ya soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu.

IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa binadamu.

Kwamba matangazo hayo yanayogharimu mamilioni ya fedha ndiyo yanayokifanya kinywaji hicho kuwa maarufu zaidi duniani, licha ya kuwa na madhara makubwa katika mwili wa binadamu.

Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa umaarufu mwingine wa kinywaji aina ya soda ni utamu wa kupindukia ulio ndani ya soda.

Utafiti wa IJUTA unaonyesha kuwa utamu wa kupindukia iliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya asidi iliyomo ndani ya soda.

IJUTA imegundua kuwa kiwango cha asidi kilicho ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa walaji kwa sababu ya kuhofia kuwa wakibaini wataacha kikutumia kinywaji hicho.

Inaelezwa pia kuwa madini ya cola yaliyo ndani ya soda yana kilevi aina kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.

Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi, ugonjwa wa ini na mengineyo.

Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa soda huwekewa ‘fructose’ (sukari) nyingi kupitia mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala nchini Marekani, amekaririwa na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini humo akieleza kuwa kinywaji aina ya soda ni hatari kwa binadamu, sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi, jambo alilosisitiza kuwa siyo la kutia chumvi, bali ukweli halisi.

Watumiaji wa vinywaji aina ya soda wanaelezwa kuwa wamekuwa wakinywa kiasi kikubwa cha kaboni, kafeini (dawa ya kulevya), sukari ya kupundukia na asidi kali ambayo huvuruga afya ya mtumiaji kwa kiwango cha juu.

Soda pia imebainika kutokuwa na lishe ya aina yoyote zaidi ya maji na sukari.
Uchunguzi wa IJUTA na utafiti ya wanasayansi mbalimbali duniani, umeonyesha kuwa watu wengi hawajui kuwa unywaji wa soda huwaongezea kiasi kikubwa cha madini joto.

Chupa moja ya soda yenye ujazo wa mililita 330 husababisha unene kwa kiwango cha paundi moja kwa mwezi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kisukari Tanzania (TDA), Ramadhan Mongi, amepata kukaririwa na vyombo vya habari hapa nchini akieleza kuwa ugonjwa wa kisukari Tanzania umeongezeka mara sita katika siku za hivi karibuni.

Alisema miaka kumi iliyopita, hali ya kisukari ilikuwa asilimia tatu (3), lakini katika miaka ya karibuni umeongezeka mara sita.

“Tunastahili kuongeza jitihada ya kupambana na gonjwa hili la kisukari kwa gharama zote kwa sababu kisukari ni moja ya magonjwa manne yanayomaliza Watanzania,” alisema.

Utafiti uliofanyika Mkoa wa Dar es Salaam ulibaini kwamba kati ya watu watano waathirika wa kisukari, mmoja tu ndiyo hupata matibabu ya serikali.

Unywaji kwa mpigo wa kabohaidrets iliyo na sukari nyingi kwenye soda hudhoofisha seli zinazozalisha vimeng’enya tofauti na vyakula vingine na pia imebainika kuwa sukari ikiingia kwa wepesi kwenye mzunguko wa damu husababisha kongosho kuzalisha vimeng’enya vingi mwilini.

Uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya wanawake ya Boston nchini Marekani na katika Chuo cha Kitabibu cha Harvard umeonyesha wanawake 51,000 hawakuwa na kisukari mwanzoni mwaka wa 1991, lakini miezi minane baadaye wanawake 741 waligundulika na kisukari.

Ripoti ya utafiti huo ilionyesha kuwa wanawake waliokuwa wakitumia kinywaji aina ya soda moja ama mbili kwa siku waliongezeka uzito maradufu na walikuwa hatarini kupata ugonjwa wa kisukari.

Pia ilionyesha kuwa soda hudhoofisha mifupa na husababisha hali ya mifupa kupuputika, hali inayomuweka mtumiaji kuwa katika hatari ya kuvunjika mifupa kirahisi.

Madhara mengine yaliyobainika kusababishwa na unywaji soda ni kupukutika kwa meno na ama kuoza. Pia soda husababisha matatizo ya figo.

Soda yenye chembe ya cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya asidi na kemikali mbalimbali zinazofichwa vipimo vyake kwa walaji.

Madaktari bingwa wa wanamichezo wanaeleza madhara yanayosababishwa na soda mwilini kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, uharibifu wa ini, huvurugu mfumo wa kumeng’enya chakula tumboni kutokana asidi ya kiwango cha juu iliyo kwenye soda.

Wanashauri kuwa soda haistahili kutumika kama kishawishi kwenye mchezo, kwa sababu ina madhara makubwa kwa wanamichezo kwa sababu hunyonya maji kwenye mwili na kudhoofisha mwili.

Wakati utafiti huo ukidhihirisha hayo, Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.
A lot of blah blah without facts. Any credible research must identify the ingredients responsible for certain health conditions and their threshold. You must know that, anything you eat is potentially dangerous but its danger depends on its threshold. Even what you call poison is harmless below threshold.
 
Urongo mtupu! Tunyweni soda baridi wandugu,, hii ni vita ya kibiashara kati ya pombe na soda!
Mama yangu ana miaka 91, halali bila kupata Coca 2 baridi. Hana sukari, presha, cancer wala figo
Anasoma biblia bila miwani. Anakumbuka enzi za ukoloni, Uhuru, ujamaa na majina yote. Mbona hamsemi Viroba?
 
Watu wengi wanafahamu ukweli kwamba soda sio kinywaji kizuri ila wanachukulia poa.

Majuto ni Mjukuu.
Mbona Whisky, vodka, viroba havisenwi! Ni wivu tuu wa kibiashara wa kuua soko la Coca.
 
Na maji ya ruvu tunayokunywa dar na zile maiti zilizookotwa, achilia mbali tunaona wanaoogelea humu
 
Kila kitu kina sumu... acheni tule maisha, hivyo mnavyosema vina sumu kila siku sasa wazungu wangekua wanakufa wiki moja baada ya kuzaliwa maana ndo vyakula vyao vya kila siku

Mkuu wewe unajua kinacho endelea katika nchi za Ulaya na Merikani?

Kwa nini wazungu mara nyingi uwakumbusha Waafrika kwamba linapokuja suala la vyakula na vinywaji/soda na life style tusijaribu kuiga mifumo yao, tukipuuzia basi na sisi tutaanza kukumbwa na magojwa kama yanayo wasumbua sana wao mfano: cancer na shinikizo la damu.

Na kweli walicho onya kwa siku nyingi ndiyo kimeanza kutukabiri sisi Wafrika kwa kasi ya ajabu.
 
Huwezi epuka sumu Kwa vyakula tulavo hewa nk cha msingi ni kula viondoa sumu mwilini Kwa wingi mfano MAJI,juice ya limao au NDIMU,matango nk
 
Usidanganye wenzio mkuu.Hakuna tofauti ya misoda au mijuisi ya Azam na soda zingine.Zote ni watoto wa baba mmoja.Mimi sigusi madudu hayo,na nawashauri watu wengine wafanye vivyo hivyo.Ndio tutakufa,lakini tusife kijinga na tufe kwa muda aliotupangia Mungu.
kunyweni azam juice na ful sana na juic na take away zote za mo na bakharesa
 
Tengeneza natural juice yako nyumbani kunywa,acha uvivu. Wenzenu wamepanga kwa makusudi kabisa kuwamaliza.Huu ni mkakati wa Illuminati wa kupungua wanadamu in what they call Depopulation Agenda.Soda ni mbinu moja wapo kati ya nyingi.Jamani ndio tutakufa lakini tufe kwa wakati aliopanga Mungu na tusife kijinga.
Pombe sinywi, maji siyapendi ntakunywa nini sasa wai!
 
Mkuu Illuminati si wajinga kama unavyofikiria.Sumu hizo zingekuwa zinauwa mara moja wewe na mimi tungestuka na hakuna ambaye angekunywa.Kinachotokea ni athari za pole pole,slow death na hatimaye kifo.Ndugu zangu hivi hamuoni magonjwa ya figo,cancer,kisukari,ini na hypertension yalivyo ongezeka sana siku hizi?Jamani zindukeni,wanawamaliza wenzenu.
Kila kitu kina sumu... acheni tule maisha, hivyo mnavyosema vina sumu kila siku sasa wazungu wangekua wanakufa wiki moja baada ya kuzaliwa maana ndo vyakula vyao vya kila siku
 
Usidanganye wenzio mkuu.Hakuna tofauti ya misoda au mijuisi ya Azam na soda zingine.Zote ni watoto wa baba mmoja.Mimi sigusi madudu hayo,na nawashauri watu wengine wafanye vivyo hivyo.Ndio tutakufa,lakini tusife kijinga na tufe kwa muda aliotupangia Mungu.
go ahead mr mwaga point na watu wanywe kila siku na biashara iendeleee....
 
Back
Top Bottom