Rogie
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 7,586
- 6,697
Any
substance can be poisonous if too much is
taken
Merry christmas
Water?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Any
substance can be poisonous if too much is
taken
Merry christmas
Huu ndio ukweli.Nashangaa wengine ndo tunasikia leo habari hizi! acha kunywa soda utaona utakavyopunguza matumizi ya kuto kwenda hospitali. kiwango kikubwa cha sukari kilichopo ndani ya soda kina leta madhara makubwa sana kiafya. Kinywaji salama ni maji tu! ndani ya mwili wanasema kunatakiwa kusafishwe, kama vyombo unasafisha kwa maji safi, je mwili wako ndo unausafisha kwa soda? kama mmea unaupa maji ili ukue na si soda, kwa nini wawapa wanao soda? tafakari
Mazoezi mazuri ni mazoezi ya kufikiri ayo ya kutanua kifua sijui kukimbia sio halisi.Kila kitu kina madhara mwilini endapo kikizidi,Hata maji yenye PH 7 yana madhara yakizidi,CHa msingi tufanye mazoezi kuweka mwili fiti,kuondoa sumu tunazokula na kunywa.
Oops, sorry nilimaanisha kunywa energy drink ila usome tahadhari iliyowekwa kabla ya kufakamia!Ninyeee[emoji107] [emoji107] [emoji107]
Kunywa juice ya azam au ya kutengeneza mwenyewe
Namshukuru Mungu alinisaidia kuuacha ulevi wa soda miaka mingi iliyopita. Nikipita sehemu nikamwona mtu akinywa soda huwa nnasikitika sana. Anyway, Mungu atusaidie kuujua huu ukweli kuwa: "soda is a sweet poison"
A lot of blah blah without facts. Any credible research must identify the ingredients responsible for certain health conditions and their threshold. You must know that, anything you eat is potentially dangerous but its danger depends on its threshold. Even what you call poison is harmless below threshold.Soda ni SUMU
AFYA za mamilioni ya Watanzania wanaotumia vinywaji vya aina ya soda ipo hatarini, baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo, MTANZANIA Jumatano linaripoti.
Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya ya umma duniani, umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.
Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.
Utafiti huo unaonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji aina ya soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu.
IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa binadamu.
Kwamba matangazo hayo yanayogharimu mamilioni ya fedha ndiyo yanayokifanya kinywaji hicho kuwa maarufu zaidi duniani, licha ya kuwa na madhara makubwa katika mwili wa binadamu.
Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa umaarufu mwingine wa kinywaji aina ya soda ni utamu wa kupindukia ulio ndani ya soda.
Utafiti wa IJUTA unaonyesha kuwa utamu wa kupindukia iliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya asidi iliyomo ndani ya soda.
IJUTA imegundua kuwa kiwango cha asidi kilicho ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa walaji kwa sababu ya kuhofia kuwa wakibaini wataacha kikutumia kinywaji hicho.
Inaelezwa pia kuwa madini ya cola yaliyo ndani ya soda yana kilevi aina kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.
Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi, ugonjwa wa ini na mengineyo.
Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa soda huwekewa ‘fructose’ (sukari) nyingi kupitia mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.
Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala nchini Marekani, amekaririwa na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini humo akieleza kuwa kinywaji aina ya soda ni hatari kwa binadamu, sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi, jambo alilosisitiza kuwa siyo la kutia chumvi, bali ukweli halisi.
Watumiaji wa vinywaji aina ya soda wanaelezwa kuwa wamekuwa wakinywa kiasi kikubwa cha kaboni, kafeini (dawa ya kulevya), sukari ya kupundukia na asidi kali ambayo huvuruga afya ya mtumiaji kwa kiwango cha juu.
Soda pia imebainika kutokuwa na lishe ya aina yoyote zaidi ya maji na sukari.
Uchunguzi wa IJUTA na utafiti ya wanasayansi mbalimbali duniani, umeonyesha kuwa watu wengi hawajui kuwa unywaji wa soda huwaongezea kiasi kikubwa cha madini joto.
Chupa moja ya soda yenye ujazo wa mililita 330 husababisha unene kwa kiwango cha paundi moja kwa mwezi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kisukari Tanzania (TDA), Ramadhan Mongi, amepata kukaririwa na vyombo vya habari hapa nchini akieleza kuwa ugonjwa wa kisukari Tanzania umeongezeka mara sita katika siku za hivi karibuni.
Alisema miaka kumi iliyopita, hali ya kisukari ilikuwa asilimia tatu (3), lakini katika miaka ya karibuni umeongezeka mara sita.
“Tunastahili kuongeza jitihada ya kupambana na gonjwa hili la kisukari kwa gharama zote kwa sababu kisukari ni moja ya magonjwa manne yanayomaliza Watanzania,” alisema.
Utafiti uliofanyika Mkoa wa Dar es Salaam ulibaini kwamba kati ya watu watano waathirika wa kisukari, mmoja tu ndiyo hupata matibabu ya serikali.
Unywaji kwa mpigo wa kabohaidrets iliyo na sukari nyingi kwenye soda hudhoofisha seli zinazozalisha vimeng’enya tofauti na vyakula vingine na pia imebainika kuwa sukari ikiingia kwa wepesi kwenye mzunguko wa damu husababisha kongosho kuzalisha vimeng’enya vingi mwilini.
Uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya wanawake ya Boston nchini Marekani na katika Chuo cha Kitabibu cha Harvard umeonyesha wanawake 51,000 hawakuwa na kisukari mwanzoni mwaka wa 1991, lakini miezi minane baadaye wanawake 741 waligundulika na kisukari.
Ripoti ya utafiti huo ilionyesha kuwa wanawake waliokuwa wakitumia kinywaji aina ya soda moja ama mbili kwa siku waliongezeka uzito maradufu na walikuwa hatarini kupata ugonjwa wa kisukari.
Pia ilionyesha kuwa soda hudhoofisha mifupa na husababisha hali ya mifupa kupuputika, hali inayomuweka mtumiaji kuwa katika hatari ya kuvunjika mifupa kirahisi.
Madhara mengine yaliyobainika kusababishwa na unywaji soda ni kupukutika kwa meno na ama kuoza. Pia soda husababisha matatizo ya figo.
Soda yenye chembe ya cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya asidi na kemikali mbalimbali zinazofichwa vipimo vyake kwa walaji.
Madaktari bingwa wa wanamichezo wanaeleza madhara yanayosababishwa na soda mwilini kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, uharibifu wa ini, huvurugu mfumo wa kumeng’enya chakula tumboni kutokana asidi ya kiwango cha juu iliyo kwenye soda.
Wanashauri kuwa soda haistahili kutumika kama kishawishi kwenye mchezo, kwa sababu ina madhara makubwa kwa wanamichezo kwa sababu hunyonya maji kwenye mwili na kudhoofisha mwili.
Wakati utafiti huo ukidhihirisha hayo, Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.
Mama yangu ana miaka 91, halali bila kupata Coca 2 baridi. Hana sukari, presha, cancer wala figoUrongo mtupu! Tunyweni soda baridi wandugu,, hii ni vita ya kibiashara kati ya pombe na soda!
Mbona Whisky, vodka, viroba havisenwi! Ni wivu tuu wa kibiashara wa kuua soko la Coca.Watu wengi wanafahamu ukweli kwamba soda sio kinywaji kizuri ila wanachukulia poa.
Majuto ni Mjukuu.
Kila kitu kina sumu... acheni tule maisha, hivyo mnavyosema vina sumu kila siku sasa wazungu wangekua wanakufa wiki moja baada ya kuzaliwa maana ndo vyakula vyao vya kila siku
kunyweni azam juice na ful sana na juic na take away zote za mo na bakharesa
Pombe sinywi, maji siyapendi ntakunywa nini sasa wai!
Kila kitu kina sumu... acheni tule maisha, hivyo mnavyosema vina sumu kila siku sasa wazungu wangekua wanakufa wiki moja baada ya kuzaliwa maana ndo vyakula vyao vya kila siku
MBEGEPombe sinywi, maji siyapendi ntakunywa nini sasa wai!
go ahead mr mwaga point na watu wanywe kila siku na biashara iendeleee....Usidanganye wenzio mkuu.Hakuna tofauti ya misoda au mijuisi ya Azam na soda zingine.Zote ni watoto wa baba mmoja.Mimi sigusi madudu hayo,na nawashauri watu wengine wafanye vivyo hivyo.Ndio tutakufa,lakini tusife kijinga na tufe kwa muda aliotupangia Mungu.