Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Any
substance can be poisonous if too much is
taken
what's too much if i may ask? taking 9-12 tea spoonful of sugar per bottle its too much, a bottle that can not even fill a glass! even a small amount can be too much..
 
Ngoja Waziri wa afya aje kukanusha. Asipokanusha nitaendelea dugong's soda kama kawa
 
tatizo letu wa Tz tulio wengi tunapenda kubeza vya kwetu, hawa waandishi wa habari za uchunguzi kuna mambo fulani wakiyaibua watu wengi hushangilia kwa nguvu zote. kwa mambo tusiyokuwa na maslai nayo tunawatolea kila aina ya kejeli, dharau na kuwapa kila aina ya majina.
ubishi wa asili unazidi kuchukua hatamu, na hivi wengi hatupendi kuwa wadadisi ndio kabisaa... kujua mambo haijalishi mtu ana elimu kiasi gani, kupenda kujifunza kunamtoa mtu gizani.
ukweli utabaki kuwa watu wamefanya soda kuwa kifungua kinywa, chakula cha mcha na usiku. soft drinks ukiachana na kemikali, sukari inayotumika ni kiasi kikubwa na ni sukari iliyosafishwa sana (refined sugar). wengi wanajua simple sugars huingia moja kwa moja kwenye mfumo wa damu. kuna wale walio hamia kwenye soda fulani kisa tu ni zero sugar... what a joke.!! gin, spirits, beer zote zinasukari kwa kiasi fulani. wengi humu tunabisha kwa nguvu zote, ('eti sijawahi kuhudhulia msiba wa mtu aliyekufa kwa kunywa soda') tumesahau kuwa mitaani, nyumbani tunawagonjwa wa kisukari, kwa bahati mbaya sana watoto wamekuwa wahanga wakubwa wa matumizi ya soda. kama hadi watoto wanapata kisukari na bado kuna watu wanabeza eti utafiti wa uongo, inasikitisha sana, inasikitisha zaidi kuona msomi ndio yuko gizani.
 
Mleta uzi na yeyote anayeamini kwamba soda ni sumu MSINYWE. Kila mtafiti anakuja na utafiti wake; mara nyama nyekundu haifai kwa afya, nguruwe wana minyoo, mbuzi wana uric acid, kondoo wana mafuta mengi, samaki wanavuliwa kwa mabomu, mboga za majani limestawishwa na dawa hatarishi, maziwa ya ng'ombe yana viini vya dawa hatarishi zilizotibu ng'ombe, au yana mimyoo, dagaa wana tegu, starch inapandisha sukari, chumvi inapandisha pressure, n.k; n.k.Kwa hiyo tusile na tusinywe? Fanyeni utafiti lakini mlete na mbadala wa hayo mbayoyaona yana kasoro. Humu duniani kuna chochote kisichokuwa na madhara kama kikipita kiasi? Tuweni tu na kiasi; lakini hata maji safi na salama yakizidi mwilini yanaweza kuleta madhara.
Mkuu mwenye jina gumu kutamka,, umegonga mulemule! Hata maji yenyewe ni sumu Ray aliwahi kusema kwamba kwa vile anakunywa maji mengi ndo maana amekuwa pepsi-mirinda! Kugegeda kwenyewe ikipita kiasi unaweza kufa, sasa wanataka kutuambia nini hawa! Wacha tujinywee soda zetu sisi!
 
*Je wajua kwamba?*
*1.ukila vizuri*

*2.ukafanya mazoezi*

*3.ukala matunda, maji ya kutosha.*

*4.ukaachana na anasa za ulevi wa pombe ,sigara,dawa za kulevya n.k*

*5.ukamrudia muumba wako.*

6. Ukaacha kunywa soda

*Ipo siku utakufa tu* [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Wakati utafiti huo ukidhihirisha hayo, Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.


Watakwambia tukitoa tamko tunaharibu biashara wakati kiuhalisia wakitoa tamko wataimarisha biashara
 
MADHARA YA KUNYWA SODA.jpg


HIZI NDIO SABABU KUMI KWANINI UACHE KUNYWA SODA KUANZIA LEO.

inawezekana una bahati sana kuiona hii makala na itakujenga sana kiafya...tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa

mwaka. japokua kuna watu wamekiri kunywa hata zaidi ya soda moja kwa siku amabayo huenda wanakunywa zaidi ya hicho kipimo. biashara ya soda inalipa sana duniani kwani ni kinywaji cha pili

kinachoongoza kunywewa duniani baada ya maji.
sasa ukiangalia mahusiano ya unywaji mdogo wa soda kila siku kiafya una madhara makubwa.

1.Ugonjwa wa kisukari;
kunywa soda moja ni sawa na kunywa vijiko 10 vya sukari, baada ya kunywa sukari hupanda sana mwilini na kongosho hutoa homoni ya ili insulini nyingi kushusha sukari. muda unavyozidi kwenda insulini huendelea kuishiwa nguvu[insulin resisitance] na hali hii husababisha wewe kupatwa na ugonjwa wa kisukari.

2. Unene na kitambi; utafiti ulofanywa na chuo kikuu cha havard umegundua kwamba watu wanaokunywa soda hunenepa mara mbili zaidi ya wale ambao hawanywi hivyo kama uko busy unapunguza uzito na pia mnywaji wa soda basi unapoteza muda.

3. upungufu wa madini muhimu mwilini; soda ina kemikali inayoitwa phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya calcium kwenye chakula ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kweye mwili wa binadamu.

4. ugonjwa wa kansa; soda ina kemikali inayoitwa caffeine ambayo imehusishwa na cancer mbalimbali za mwili mfano kansa ya kongosho, kansa ya utumbo na magonjwa mengine kama presha ya damu na kansa ya matiti.

5. huongeza sumu mwilini; soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu hivyo huongeza kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambacho ni hatari sana kwa afya mtumiaji.sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa presha, na kuua figo.

6. hubadilisha rangi ya meno; kila mtu anataka kua na meno masafi na meupe lakini baadhi ya soda zina kiasi kikubwa cha tindikali ambacho hushambulia na kuharibu meno kwa muda mfupi.hivyo kama unasumbuliwa na meno basi huu ni muda mzuri wa kuachana nayo.

7. addiction (Uteja); soda nyingi zina tabia ya kumfanya mtu apate ulevi wa soda husika yaani kuna watu unakuta anapenda sana soda fulani na asipoinywa kwa siku atahisi kama amepungukiwa kabisa na kitu fulani mwilini.hii itakufanya uwe mtumwa wa mwili wako mwenyewe.

8. huongeza kasi ya uzee; sumu ambazo unazipokea kwenye soda zinazeesha mtu mapema sana yani kijana mdogo wa miaka 20 hujikuta anaonekana kama miaka 35.

9. Hupunguza sana maji mwilini ; soda ina kiwango kikubwa cha madini ya sodium ambayo humfanya mtu abaki na maji kidogo na kwa muda mrefu atapata matatizo mengine ya kiafya kama mawe ya kwenye figo[kidney stone] na mawe kwenye nyongo ya binadamu.

10.Mwisho; ni vizuri kubadili mfumo wako wa maisha na kuanza kunywa vitu haviharibu mwili yaani badala ya kunywa soda basi tumia juice za Matunda ambayo ni mbadala mkubwa wa soda, lakini pia unaweza kunywa maziwa na kadhalika.
 
Back
Top Bottom